Niulize chochote kuhusu ntakujibu nikitu Cha ukweli mkuu na kimeisha tayali
Hilo gereza ulilofungwa hali yake ilikuwa hivi?? Hili ni segerea (DSM) kwa mujibu wa Boni Yai.
Ndani ya gereza Kuu la Mahabusu Dar es Salaam - Segerea kuna sehemu kubwa na maarufu kama tano;
Sehemu ya kwanza; nje ya gereza, wageni hufika na kusubiri utaratibu wa kuingia ndani kuona ndugu zao. Kuna Canteen, Duka na eneo la kukaa wageni.
Sehemu ya pili; Jengo la Utawala ambalo ndiyo ofisi ya Mkuu wa Gereza maarufu “Bwana Jela” na askari wake wanasimamia wafungwa na mahabusu ndani ya gereza.
Sehemu ya tatu; “ujambazini”, huko kuna vyumba vya Jela 10 na kila Kimoja kina idadi maalum ya watu, mfano namba 10 inachukua watu zaidi ya 200 na zaidi.
Sehemu ya nne; Upande maalum (Special Wing) wanaishi mahabusu au wafungwa ambao ni watoto chini ya miaka 18, mahabusu, wafungwa wachache
Sehemu ya tano; “PC - Private Cell”. Huko hupelekwa watu watukutu au wanaotenda makosa wakiwa ndani ya gereza nje na makosa wanayopelekwa nayo gerezani.
Ujambazini selo zipo 10 zikiwa zina Mahabusu na Wafungwa wanaokadiriwa kuwa 600
katika hao 600 mahabusu pekee wapo 500 kule Ujambazini kote na Mahabusu 400 wote wanakabiliwa na mashitaka ya Ujambazi (armed robbery) na cha ajabu zaidi wote mashitakata yao yametokea zehemu moja, kwa "Dulla Ma-robbery" nitaeleza siku nyingine kwa upana hapa.
Kwanini wanaita special wing? Ni swali kila mtu anajiuliza ndani ya gereza na nje ya gereza lakini hakuna mwenye majibu kamili. Kwa sababu siku hizi hata Ujambazini kuna TV zenye ving'amuzi vya DSTV na AZAM kila Jengo.
Ujambazini kula chakula cha gerezani (ugali maharage umejitakia tu) sababu watu wa Ujambazini wanaruhusiwa kuweka order ya chakula cha canteen.
SALAMU KUTOKA UJAMBAZINI.. Najua ukisikia neno “ujambazini” lazima utashtuka kidogo. Nikutoe hofu neno kabisa. Neno ‘ujambazini’ ni jina la eneo kama ilivyo Posta, Masaki au Manzese. Nikupeleke sasa Ujambazini huko. Ujambazini ni Magharibi mwa Jiji la Dar es salaam, na kusini mwa Wilaya ya...
www.jamiiforums.com