Yajue Makabila Yanayopatikana Tanzania Visiwani ( Zanzibar )

Yajue Makabila Yanayopatikana Tanzania Visiwani ( Zanzibar )

jamani kuna taarifa kwanza zanzibar hakuna makabila kama ilivyo tanzania bara, je nini kimepelekea hivi au ndio mambo ya kutawaliwa na mwarabu? wazenji wote wanaongea kiswahili hila kwa lafudhi tofautitofauti. wakuu nini kimepelekea zanzibar kutokuwa na makabila kama bara?

Kuna mshikaj wang wa Zanzibar aliniambia kule hakuna makabila na hawana lugha ya kikabila wao ni kiswahil tu akasema anataman sana wangekua na lugha ya kikabila kama bara kwan inasaidia kuongea vtu wengine wacjue!
 
kabila waznz wote ni uislam tu, hatuna kabila jengine........izo fitna mnazotupandikiza za huyu muarabu, huyu mpemba na yule ni muunguja ni ili tufarikiane ni baada ya kuona huku hakuna anaeshughulika na kabila sababu sote ni wamoja
 
Mpaka sasa hakuna alieielewa mada..wote Dana dana tu...
What happen to the great thinkers jf ?
 
sasa si wapo laki nane Zanzibar yote huoni wachache,cye milioni 45
 
Mtoa mada huwezi amini jana nilikuwa na rafiki yangu mmoja wa unguja nilimuuliza kuhusu kama kuna kabila huko ambao wanaweza kuongea lugha mbali na kiswahili akanijibu hakuna. Kinacho watofautisha wao ni lafudhi tu.
 
Kuna mshikaj wang wa Zanzibar aliniambia kule hakuna makabila na hawana lugha ya kikabila wao ni kiswahil tu akasema anataman sana wangekua na lugha ya kikabila kama bara kwan inasaidia kuongea vtu wengine wacjue!

Mmmhu, mmakunduchi akiongea huoni ndani mkuu. Hata kama unakijua kiswahili. Anaweza akakusema Na wewe upo hapo hapo. Wenyewe wanaita kuchowea.

Kuna na wapemba wa shamba nao huko, hatari
 
Unaposema kabila katika uwanda wa
mwambao wa pwani lugha halisi ni
kiswahili lakini tofauti ni lahaja kwa
unguja kuna
kiunguja,kihadimu,kipemba bara huku
kuna kimtangata, kimrima, kiamu nk.
Kuna wengi suala la mabila hasa ya
wenyeji wa mwambao hawaelewi
pengine maelezo yafuatayo yatatoa
mwanga:-
Swahili ni Taifa la makabila yaliopo
katika Pwani ya Afrika ya Mashariki na
visiwa vyake tokea Barawa hadi Sofala.
Baadhi ya makabila hayo ni
Wabarawa, Wapate, Waamu,
Wagiriama, Wadigo, Waduruma,
Wakauma, Wakambe, Wachoni,
Warabai, Waribe, Wajibana,
Wakilindini, Wajomvu, Wamtwapa,
Wachangamwe, Watangana, Wamvita,
Wapokomo, Wavanga, Wamakunduchi,
Wapemba na Wangazija. Kabila hizi
zote zilikuwa zikizungumza lugha
ilokuwa ikijulikana kama Kingozi. Hata
hivyo, makabila yote haya yalikuwa na
ndimi (dialect) zao na miji yao; baadhi
yao bado wangali na ndimi zao na miji
yao. Ndimi zote hizi zina ukhusiano au
ukuruba mkubwa wa maneno na
maana zake. Kwa mfano, utakuta
kwamba kuna ukuruba fulani baina ya
Kipemba na Kiamu.
Kila kabila ina ndimi yake, dasturi
zake, mila zake, tungo zake, na
kadhalika. Haya yote ni kabla ya
Waarabu na Washirazi hawajaanza
kuhamia kimaisha katika Pwani ya
Afrika ya Mashariki - takriba karne
nane hadi kumi zilizopita (yaani baina
ya miaka 800 hadi 1000).
Washirazi hawakuathiri mno mila,
dasturi, mapisi, na lugha hiyo ya Watu
wa Pwani. Waarabu ndiyo walioathiri
sana, khususa Makabila ya Kati na
Kati (kwa mfano, Wamvita, Watangana
na Wakilindini). Makabila haya
yaliathirika mno hadi ya kuwa majina
haya yalipotea na ndimi zao za kiasili
zilipotea vilevile. Ndimi ambazo bado
zipo ingawa zimeazima maneno fulani
ya Kiarabu (kama ambavyo pengine
Kiarabu kimeazima kutoka Lugha ya
Kingozi) ni ndimi za kaskazini na zile
za kusini.
Ndimi za Kaskazini ambazo bado zipo
na wenyewe wanatambuliwa ni kama
vile Kibarawa, Kiamu, Kipokomo, na
kadhalika. Ama Ndimi za Kusini
ambazo hazikuathiriwa mno ni
Kingazija, Kimakunduchi, Kipemba na
Kivanga. Ndimi za Kati na Kati ambazo
bado zikalipo ni kama vile, Kigiriama,
Kiduruma, Kijibana; hizi ni miongoni
mwa kabila ambazo leo zajiita au
zatambuliwa kama Mijikenda (yaani
miji tisia).
Utakuta ya kuwa katika makabila ya
kati na kati, yale ambayo
hayakuathiriwa sana ni yale ambamo
watu wake hawakuwa Waislamu. Na
ndiyo maana mpaka hii leo utaona ya
kuwa makabila ya Mijikenda
(isipokuwa Digo), ni makabila ambayo
wengi katika watu wake si Waislamu.
Hii ni kwa sababu makabila kama ya
Mvita, Tangana na Changamwe
hayakujitahidi au kujishughulisha
kufanya usambazaji wa Risala ya U-
Islam kwa makabila haya; Waarabu
piya walipokuja hawakuwa na lengo
hilo la kuingia vijijini kufanya Da’wah.
Lengo lao kubwa ilikuwa ni biashara.
Kama tujuavyo U-Islam ulifika
Kaskazini Mashariki mwa Bara la
Afrika kabla haujafika katika sehemu
nyengine za bara Arabu kama vile,
Yemen, Omani na hata katika mji wa
Madina na sehemu nyingi za nchi
tunayoijua leo kama Saudi Arabia.
Yaani U-Islam ulifika Abisinia (Ethiopia
ya leo) katika mwaka wa 615, miaka
mitano tu baada ya Mtume Muhammad
(s.a.w.) kupewa risala (610). Mtume
alizaliwa mwaka wa 570. Ingawa wale
Waislamu waliokuja kuomba hifadhi
Abisinia walikwenda zao Madina baada
ya kutawazwa kwa serikali ya kwanza
ya Islam mwaka wa 623 (huu ni
mwaka wa kwanza wa Hijria),
walikuwa washawasilimisha watu
kadha wa kadha (akiwemo Mfalme
wao, Najash); hii ndiyo ilikuwa ni
sababu ya kuanza kusambaa kwa U-
Islam katika bara la Afrika. Kwa hivyo
ni muhimu kutambua na kuamini ya
kuwa makabila fulani ya Afrika ya
Mashariki yalisilimu kabla ya kuja kwa
Waarabu hawa tuwajuwao leo,
waliokuja kwa biashara katika pwani
ya Afrika ya Mashariki kutoka Yemen,
Omani, na kadhalika.
Na khususa ni Waarabu hao wa Yemen
na Omani ndiyo waloowana na baadhi
ya hao Wangozi, au wanaojulikana leo
kama Waswahili. Kwa hivyo, baadhi ya
Waswahili wana damu za Kiarabu na
baadhi yao hawana damu ya Kiarabu.
Katika dasturi za Kizungu za kufuata
ukoo, mtu anapotanganya tu damu na
asekuwa Mzungu, basi azaliwae katika
mtanganyiko huo katu hakubaliwi
kuwa ni Mzungu. Na ndiyo twaona ya
kuwa ingawa kuna asili mia thalathini
(30%) ya Wamarekani Weuse (African-
Americans) ndani ya Marekani, lakini
wanasibishwa na U-Afrika na U-weuse
(Blacks) pekee, na katu hawanasibishwi
na uzungu. Kwa Waarabu nao ni rahisi
zaidi kunasibishwa na taifa hilo ikiwa
mtu lugha yake ya kwanza ni Kiarabu.
Ama kwa Waswahili tukati na kati,
yaani aghlabu mtu hunasibishwa na
Uswahili kwa lugha na asili. Kwa hivyo
leo wako baadhi ya Waswahili wenye
damu za Kiarabu ambao wametagua,
kwa sababu mbalimbali, kujinasibisha
zaidi na U-Arabu kuliko U-Afrika;
kadhalika, kuna baadhi yao, kwa
sababu moja au nyengine, wameamua
kujinasibisha zaidi na U-Afrika kuliko
U-Arabu.
 
Unaposema kabila katika uwanda wa
mwambao wa pwani lugha halisi ni
kiswahili lakini tofauti ni lahaja kwa
unguja kuna
kiunguja,kihadimu,kipemba bara huku
kuna kimtangata, kimrima, kiamu nk.
Kuna wengi suala la mabila hasa ya
wenyeji wa mwambao hawaelewi
pengine maelezo yafuatayo yatatoa
mwanga:-
Swahili ni Taifa la makabila yaliopo
katika Pwani ya Afrika ya Mashariki na
visiwa vyake tokea Barawa hadi Sofala.
Baadhi ya makabila hayo ni
Wabarawa, Wapate, Waamu,
Wagiriama, Wadigo, Waduruma,
Wakauma, Wakambe, Wachoni,
Warabai, Waribe, Wajibana,
Wakilindini, Wajomvu, Wamtwapa,
Wachangamwe, Watangana, Wamvita,
Wapokomo, Wavanga, Wamakunduchi,
Wapemba na Wangazija. Kabila hizi
zote zilikuwa zikizungumza lugha
ilokuwa ikijulikana kama Kingozi. Hata
hivyo, makabila yote haya yalikuwa na
ndimi (dialect) zao na miji yao; baadhi
yao bado wangali na ndimi zao na miji
yao. Ndimi zote hizi zina ukhusiano au
ukuruba mkubwa wa maneno na
maana zake. Kwa mfano, utakuta
kwamba kuna ukuruba fulani baina ya
Kipemba na Kiamu.
Kila kabila ina ndimi yake, dasturi
zake, mila zake, tungo zake, na
kadhalika. Haya yote ni kabla ya
Waarabu na Washirazi hawajaanza
kuhamia kimaisha katika Pwani ya
Afrika ya Mashariki - takriba karne
nane hadi kumi zilizopita (yaani baina
ya miaka 800 hadi 1000).
Washirazi hawakuathiri mno mila,
dasturi, mapisi, na lugha hiyo ya Watu
wa Pwani. Waarabu ndiyo walioathiri
sana, khususa Makabila ya Kati na
Kati (kwa mfano, Wamvita, Watangana
na Wakilindini). Makabila haya
yaliathirika mno hadi ya kuwa majina
haya yalipotea na ndimi zao za kiasili
zilipotea vilevile. Ndimi ambazo bado
zipo ingawa zimeazima maneno fulani
ya Kiarabu (kama ambavyo pengine
Kiarabu kimeazima kutoka Lugha ya
Kingozi) ni ndimi za kaskazini na zile
za kusini.
Ndimi za Kaskazini ambazo bado zipo
na wenyewe wanatambuliwa ni kama
vile Kibarawa, Kiamu, Kipokomo, na
kadhalika. Ama Ndimi za Kusini
ambazo hazikuathiriwa mno ni
Kingazija, Kimakunduchi, Kipemba na
Kivanga. Ndimi za Kati na Kati ambazo
bado zikalipo ni kama vile, Kigiriama,
Kiduruma, Kijibana; hizi ni miongoni
mwa kabila ambazo leo zajiita au
zatambuliwa kama Mijikenda (yaani
miji tisia).
Utakuta ya kuwa katika makabila ya
kati na kati, yale ambayo
hayakuathiriwa sana ni yale ambamo
watu wake hawakuwa Waislamu. Na
ndiyo maana mpaka hii leo utaona ya
kuwa makabila ya Mijikenda
(isipokuwa Digo), ni makabila ambayo
wengi katika watu wake si Waislamu.
Hii ni kwa sababu makabila kama ya
Mvita, Tangana na Changamwe
hayakujitahidi au kujishughulisha
kufanya usambazaji wa Risala ya U-
Islam kwa makabila haya; Waarabu
piya walipokuja hawakuwa na lengo
hilo la kuingia vijijini kufanya Da’wah.
Lengo lao kubwa ilikuwa ni biashara.
Kama tujuavyo U-Islam ulifika
Kaskazini Mashariki mwa Bara la
Afrika kabla haujafika katika sehemu
nyengine za bara Arabu kama vile,
Yemen, Omani na hata katika mji wa
Madina na sehemu nyingi za nchi
tunayoijua leo kama Saudi Arabia.
Yaani U-Islam ulifika Abisinia (Ethiopia
ya leo) katika mwaka wa 615, miaka
mitano tu baada ya Mtume Muhammad
(s.a.w.) kupewa risala (610). Mtume
alizaliwa mwaka wa 570. Ingawa wale
Waislamu waliokuja kuomba hifadhi
Abisinia walikwenda zao Madina baada
ya kutawazwa kwa serikali ya kwanza
ya Islam mwaka wa 623 (huu ni
mwaka wa kwanza wa Hijria),
walikuwa washawasilimisha watu
kadha wa kadha (akiwemo Mfalme
wao, Najash); hii ndiyo ilikuwa ni
sababu ya kuanza kusambaa kwa U-
Islam katika bara la Afrika. Kwa hivyo
ni muhimu kutambua na kuamini ya
kuwa makabila fulani ya Afrika ya
Mashariki yalisilimu kabla ya kuja kwa
Waarabu hawa tuwajuwao leo,
waliokuja kwa biashara katika pwani
ya Afrika ya Mashariki kutoka Yemen,
Omani, na kadhalika.
Na khususa ni Waarabu hao wa Yemen
na Omani ndiyo waloowana na baadhi
ya hao Wangozi, au wanaojulikana leo
kama Waswahili. Kwa hivyo, baadhi ya
Waswahili wana damu za Kiarabu na
baadhi yao hawana damu ya Kiarabu.
Katika dasturi za Kizungu za kufuata
ukoo, mtu anapotanganya tu damu na
asekuwa Mzungu, basi azaliwae katika
mtanganyiko huo katu hakubaliwi
kuwa ni Mzungu. Na ndiyo twaona ya
kuwa ingawa kuna asili mia thalathini
(30%) ya Wamarekani Weuse (African-
Americans) ndani ya Marekani, lakini
wanasibishwa na U-Afrika na U-weuse
(Blacks) pekee, na katu hawanasibishwi
na uzungu. Kwa Waarabu nao ni rahisi
zaidi kunasibishwa na taifa hilo ikiwa
mtu lugha yake ya kwanza ni Kiarabu.
Ama kwa Waswahili tukati na kati,
yaani aghlabu mtu hunasibishwa na
Uswahili kwa lugha na asili. Kwa hivyo
leo wako baadhi ya Waswahili wenye
damu za Kiarabu ambao wametagua,
kwa sababu mbalimbali, kujinasibisha
zaidi na U-Arabu kuliko U-Afrika;
kadhalika, kuna baadhi yao, kwa
sababu moja au nyengine, wameamua
kujinasibisha zaidi na U-Afrika kuliko
U-Arabu.

mkuu umetisha
 
Wapemba : pemba
Watumbatu : tumbatu
Washilazi :shilazi.
Naona tunatajiwa sehemu watokazo Wakati mada inataka kabila.
Je nasi tuseme hivi.
Watabora _ tabora
Wadodoma _ dodoma
Waarusha _ arusha.
?????

Ulitaka waitweje wakati hivyo ndivyo wanavyoitwa?? ongeza na haya
Wadiba, wahadimu, na wapesia!!......haya na hawa wape maeneo!!
 
kama yapo yataje hapa

Usiwe mwepesi wa kupost tuu uwe mwepesi wa kusoma post unazojibiwa!!.. hayo makabila unataka yatajwe mara ngapi??.. zi umetajiwa wadiba, wapemba, wahadimu, wapesia, wabantu n.k!!... unataka niongeze na lukelo??
 
Safi sana watononokaji..hii inaashiria ukomavu wa kihistoria big up wakuu
 
OK! kwa sasa Zanzibar hakuna makabila, na huo ni makakati uliochukuliwa kupotezea upuuzi wa mambo ya ukabila.
Is it possible kufuta makabila brother ??
well it doesn't make any sense kusema hakuna.....yameenda wapi? na yalikua ni yapi?
 
Is it possible kufuta makabila brother ??
well it doesn't make any sense kusema hakuna.....yameenda wapi? na yalikua ni yapi?
Yea! Nikupotezea tu! kuanzia leo wazanzibari tutajitambulisha kwa utaifa wetu sio makabila yetu. Ukiulizwa we kabira gani jibu mimi ni mtanganyika au mzanzibari. Document zote Zanzibar hakuna kipengele kinachoulizia kabila, ni Dini na utaifa tu, so kizazi cha sasa hakielewi chochote kuhusu ukabila, wanachojuwa ni Uislamu wao na Uzanzibari wao.
 
Yea! Nikupotezea tu! kuanzia leo wazanzibari tutajitambulisha kwa utaifa wetu sio makabila yetu. Ukiulizwa we kabira gani jibu mimi ni mtanganyika au mzanzibari. Document zote Zanzibar hakuna kipengele kinachoulizia kabila, ni Dini na utaifa tu, so kizazi cha sasa hakielewi chochote kuhusu ukabila, wanachojuwa ni Uislamu wao na Uzanzibari wao.
.yameenda wapi? na yalikua ni yapi?
 

Zanzibar itabaki kisiwa cha Waarabu na Waswahili tu. Na lugha lugha itazungumzwa kiarabu na kiswahili na kiingerza. Wabara mtabaki na UBANTU wenu na lugha zenu za jadi. Si ndiyo mnapendelea UBAGUZI huo ?
kama hamutaki Uswahili acheni * mtii na jongoo wake ** siye tutaukumbatia ustaarabu wetu na kulala na uswahili wetu.
Hivi ndugu zangu mnafahamu kuwa kiarabu na kiswahili ndiyo lugha zinazotumia na wengi bara la afrika?
 
Back
Top Bottom