Yajue Mapinduzi ya Niger kwa upana zaidi

Shida ni viongozi wetu sasa na sio hao westerns, ni tamaa za viongozi wetu.
 
Maelfu ya wananchi wa Niger na Gabon walimiminika mitaani kushangilia na kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi!!! Sijui Rais anajisikiaje kuona wananchi wamemkataa na kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi!! Inaonesha hawa viongozi walikuwa vibaraka tu wa mabeberu na walitumikia maslahi ya mabeberu badala ya kuwatumikia wananchi wao. Matumaini pekee kwa wananchi hao ilikuwa kwa majeshi yao tu. Majeshi ya Niger na Gabon yamedhihirisha kuwa ni majeshi ya wananchi haswa!!

Bila aibu mataifa ya magharibi bado yanawataka vibaraka wao warudi madarakani!! Haya mataifa ya mabeberu hujinasibu kuwa yanasimamia demokrasi!! Demokrasi ni kukubaliana na matakwa ya wengi!! Bila aibu Ufaransa imegoma kumrudisha nyumbani balozi wao aliyevuliwa hadhi ya ubalozi nchini Niger. Pia Ufaransa imegoma kuyaondoa majeshi yake yaliyopo Niger baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Niger.

Watanzania tujifunze kitu hapo!! Mabeberu ukiwaruhusu kuingiza majeshi yao nchini kwako, huwa wanag'ang'ania milele!! Tumeiona kwa Iraq, Ujerumani, Japan, Korea ya kusini na sasa Poland!! Nchi zote hizo kuna majeshi ya marekani na marekani hawezi kukubali kutoka. wananchi wa Japan kwa mfano mara kadhaa wamekuwa wakiandamana kupinga kuwepo majeshi ya marekani kwenye maeneo yao!. Marekani iliingiza majeshi yake Syria kwa nguvu na hawataki kutoka!!

Hapa chini maelfu ya raia wa Niger wakiandamana kupinga uwepo wa majeshi ya Ufaransa nchini mwao!!

View: https://twitter.com/i/status/1698181141206049264
 
Done ✔️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…