Yajue ya Tanga Mjini na maajabu yake

Yajue ya Tanga Mjini na maajabu yake

Unakuta kutwa mzee katulia tu na msuli
Kumbe ana bonge la shamba la minazi
Mhhh! Kwa standard ya Tanga, ni shamba la ukubwa gani ambalo mtu anaweza kujigamba kwamba ana bonge la shamba i.e. ni lenye eneo na idadi gani ya minazi?:AYOOO:
 
Linaweza lisiwe kubwa sana yaani hekari nyingi lakini linamtosha

Kwani Nazi kwa kiazi kikubwa zinatoka mkoa gani
 
Mhhh! Kwa standard ya Tanga, ni shamba la ukubwa gani ambalo mtu anaweza kujigamba kwamba ana bonge la shamba i.e. ni lenye eneo na idadi gani ya minazi?:AYOOO:
Mnazi ambao ni wa asili hii yetu ambayo hata haizai sana inatoa Nazi 70-120 kwa mwaka, heka moja kama minazi 140, hizo ni Nazi 10,000 mpaka 15,000, hata kama unauza bei ya Chini kama 500 inaweza fika 5M ama zaidi.

Tanga mjini imezungukwa na Muheza, mkinga na pangani fukwe ya Bahari ya hindi hadi unakuja kutokea bagamoyo kuna mashamba ya kutosha.

Ubaya wa minazi return yake inachukua muda mrefu, kupanda mti miaka 7 unakaa tu kunahitaji moyo, ila ukianza kuvuna unakula tu good time.
 
1 - Saa 3 usiku hakuna daladala barabarani.
2- Saa 4 usiku huoni watu nje na usiulize kwanini. Jiongeze bro!
3- Ugali wa 1500 unapata mboga 7, usisahau uono (dagaa mchele) buree.
4- Ndio jiji lenye baiskeli za kukodi kama bodaboda na kiti chenye sponji.
5- Disco wanapiga taarabu.
6- Hakuna kelele wala vurugu ni kimyaaa hadi raha.
7 - Kijana akishakuwa na uhakika wa kula na kulala anaoa hata wake watatu kwa mpigo.
8- Binti wa Kitanga mwambie apande pikipiki utalipa. Akifika mnunulie chips yai na soda. Kwisha!
9 - Ndio jiji lenye soda zake. 'Healtho' au 'Anjari'. Huko Bakhresa na Mo hawasikiki.
10 - Ukiishi na watu vizuri kuoa na kuolewa hupati shida wao ndo wanamaliza kazi.
11- Raskazone, Donge,Tanga Beach ndio ushuani kwa mafogo.
12- Maji ya kunywa siyo ya kununua dukani, ya bomba tu yanakata kiu, safi hadi raha.
13- Kwa mabinti uwe na pumzi, ukijiroga bro utatolewa jasho ujute.
14 - Kuna traffic light mbili tu pale Toyota na Mombo Hospitali.
15- Machimbo yetu yaleee ni nenda Sabasaba na Kwa Chichi. Hii ni code kwa wakware.
16 - Daladala ipo radhi kumsubiri mtu hata ikibidi kupiga rivasi kumfuata alipo.
17- Ni jiji lililopangika vizuri uswahilini, mjini mpaka ushuani.
18 - Kule madem wanaenda bar au club na madera na ushungi kichwani.
19 - Tanga kila binti anajua mapenzi na wanaheshimu wanaume.
20 - Mabinti wa Tanga wanapenda ndoa na wanajua kulea waume.

Ongeza nyingine ✍️
Ulichokiandika ni ukweli mtupu 100%.
Kwa kuongezea.
21. Tanga mjini baiskeli ndio kila kitu, unaweza kuhisi kila mtu anajua kuendesha baiskeli, kila nyumba kuna baiskeli, baiskeli zinapiga miche za kubeba watu kama boda boda.

22. Tanga hakuna haraka, hakuna stress, watu waishi kwa kuridhika mnoo, maisha yaenda tu tena kwa rahaaa.

Mwisho wa yote, msambaa mnaweza kumdharau kwingine kote lakini kwa Tanga mjini, kabila la wasambaa ndio kabila la kuringa, kuheshimiwa na kupapatikiwa.
 
Mnazi ambao ni wa asili hii yetu ambayo hata haizai sana inatoa Nazi 70-120 kwa mwaka, heka moja kama minazi 140, hizo ni Nazi 10,000 mpaka 15,000, hata kama unauza bei ya Chini kama 500 inaweza fika 5M ama zaidi.

Tanga mjini imezungukwa na Muheza, mkinga na pangani fukwe ya Bahari ya hindi hadi unakuja kutokea bagamoyo kuna mashamba ya kutosha.

Ubaya wa minazi return yake inachukua muda mrefu, kupanda mti miaka 7 unakaa tu kunahitaji moyo, ila ukianza kuvuna unakula tu good time.
Nanukuu: "Mnazi ambao ni wa asili hii yetu ambayo hata haizai sana inatoa Nazi 70-120 kwa mwaka, heka moja kama minazi 140, hizo ni Nazi 10,000 mpaka 15,000, hata kama unauza bei ya Chini kama 500 inaweza fika 5M ama zaidi." Yan mtoto anazaliwa anakua hadi aweze kuingia std 1 ndipo unaanza kupata mazao ya shamba lako.
Vp gharama nyingine inakuwaje e.g. Mkwezi, Mfuaji, Usafirishaji na Post-harvest losses?
 
Terrible life ndio ipi hiyo,usipoangalia ndio mkoa unaaongoza kwa wazee kuishi muda mrefu...
Low senescence rate and insignificant rate of tear and wear kwa sababu hawafanyi kazi za suluba. Nakubali Nikosolewe.
 
Nanukuu: "Mnazi ambao ni wa asili hii yetu ambayo hata haizai sana inatoa Nazi 70-120 kwa mwaka, heka moja kama minazi 140, hizo ni Nazi 10,000 mpaka 15,000, hata kama unauza bei ya Chini kama 500 inaweza fika 5M ama zaidi." Yan mtoto anazaliwa anakua hadi aweze kuingia std 1 ndipo unaanza kupata mazao ya shamba lako.
Vp gharama nyingine inakuwaje e.g. Mkwezi, Mfuaji, Usafirishaji na Post-harvest losses?

Kwa wewe unaeanza yes, ila mashamba ya Nazi mostly watu wananunua ama wanarithi. Na unapanda minazi mipya wakati minazi ya zamani ipo, so ukishafika level ya kuvuna haina shida tena.

Mkwezi, ufuaji, usafirishaji ni gharama ndogo, 5M ni at minimum kabisa nimepigia, even ukitoa gharama zote hizo kuna probability kubwa bado ikawa ni 5M+, heka moja wakwezi wawili tu wanatosha.

Ukiwa uliza wenyewe wenye Nazi ni hadi 2M wanapata kwa mvuno Na kwa mwaka ni mara 3 ama zaidi wanavuna, so tuna rudi pale pale.

makaveli10 anazijua zaidi atakuja kukupa darasa
 
Nashukuru ila kwa bahati mbaya huku kwetu umasaini kilimo cha minazi tunakisikiaga tu - Hakipo.
 
Kwa wewe unaeanza yes, ila mashamba ya Nazi mostly watu wananunua ama wanarithi. Na unapanda minazi mipya wakati minazi ya zamani ipo, so ukishafika level ya kuvuna haina shida tena.

Mkwezi, ufuaji, usafirishaji ni gharama ndogo, 5M ni at minimum kabisa nimepigia, even ukitoa gharama zote hizo kuna probability kubwa bado ikawa ni 5M+, heka moja wakwezi wawili tu wanatosha.

Ukiwa uliza wenyewe wenye Nazi ni hadi 2M wanapata kwa mvuno Na kwa mwaka ni mara 3 ama zaidi wanavuna, so tuna rudi pale pale.

makaveli10 anazijua zaidi atakuja kukupa darasa
Mnazi uliokomaq vizuri, unaweza kuvuna kila baada ya miezi mi3 we unavuna zile kavu kabisa, zilizokomaa vizuri saaana(kavu, hii mara nyingi ukiifua huwa na rangi kama ya kahawia isiyokoza au tuite brown ) unaacha zile ambazo hazijakomaa vizuri(mkwezi mzuri kule juu anajua hii imekomaa(kavu) na hii bado)
Hivyo kwa mwak mnazi unaweza kuuvuna mara 3 hadi 4.

Kwangu mnazi ambao niliwahi kushusha nazi nyingi zaidi kwa mpigo zilikuwa 94(yalikuwa ni makole ma3), mnazi huu nilikuja kuukata kinyooonge sababu hakukuwa na namna. Minazi mingine unaweza kuvuna nazi 30+ 40+ na kuendelea mpaka 70 kama mnazi hausumbuliwi(kuvunwa hovyo bila mpangilio) ama kuchumwa sana madafu, ama wezi kuipitia pitia, wezi ni chamgamoto, unaweza jikuta unaambulia nazi 2 kwa mnazi au 0 kabisa..

Kuhusu mkwezi, wakwezi wengi huwa wanachukua nazi 2 kwa kila mnazi au gharama ya nazi 2 kwa bei ya nazi sehemu husika, kama nazi ni 500 moja, basi utamlipa buku kwa kigongo(mnazi).
 
Back
Top Bottom