Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
1. Samia hakutoa amri kuamuru mauaji ya raia na wananchi- Hii itasemwa ili kujaribu kumsafisha Samia kwenye jumuiya ya Kimataifa na kujaribu kumuepusha na kikombe cha ICC.
2. Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hawakutoa amri za kuamuru kuuwawa kwa Wananchi- Hili litasemwa ili kuwaepusha wakuu hawa na mkono wa ICC. Inaweza pendekezwa waachie nafasi zao kwa kudaiwa tu kushindwa kuzuia mauaji bila kushtakiwa ila hili pia ni kiinimacho tu maana wengi wameshafika umri wa kustaafu na wamelipwa mabilioni ya fedha kama shukrani na pongezi kwa kuuwa wananchi na kuhakikisha Samia anabaki madarakani.
3. Polisi waliopiga risasi za moto na kuua wananchi walijichukulia Sheria mkononi. Vyombo vya Ulinzi na Usalama vifanye uchunguzi kuwabaini askari husika na kuwachukulia hatua- Hii ni kuleta danganya toto kwenye Jumuiya ya Kimataifa ili kuonesha kuna hatua zinachukuliwa kumbe ni kuchezesha akili za watu tu.
4. Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Dar, Geita, Arusha, Mbeya, Songwe, Mwanza waondolewe kwenye nafasi zao- Hii ni kujaribu kuonesha kuna uwajibikaji ila ni kiini macho tu. Hawa wataendelea kuwa askari hadi watakapostaafu. Hakutakuwa na kushtakiwa wala nini.
5. Idadi ya vifo ni chini ya 100 pia hakukuwa na makabuli ya halaiki wala watu kuzikwa kinyume na taratibu. Hili litasemwa ili kujaribu kuonesha mauaji yaliyofanyika ni ya idadi ndogo ya watu na kujaribu kukataa kuwa hakuna makabuli ya halaiki ili kujaribu kukwepesha ushahidi uliopo kwenye Taasisi mbalimbali za Kimataifa na Vyombo vya habari vya kimataifa.
6. Uchaguzi ulifanyika vizuri, ulikuwa huru na wa haki, kura zilipigwa vizuri na matokeo yaliyotangazwa yalikuwa halali. Hili litasema ili kumtengenezea legitimacy Samia kuonekana ni Rais halali aliyepatikana kwa njia halali.
7. Waliojeruhiwa na kupoteza maisha walipwe. Hili litasemwa kujaribu kuidanganya Jumuiya ya Kimataifa kuwa wanajali na wanaponya nyoyo za watu. Litasemwa pia ili kujaribu kuwadanganya Watanzania kuwa watapewa hela ili kuwatuliza maumivu.
8. Mchakato wa Maridhiano uanze haraka kutibu majeraha. Ili litasemwa ili kuendelea kuiribuni Jumuiya ya Kimataifa kuwa wameanzisha rasmi mchakato wa Maridhiano ili kuifanya isichukue hatua ikiwemo kulazimisha wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya haki na kuhukumiwa. Ikumbukwe hili lilishapangwa na ccm na samia wao hata kabla ya Uchaguzi maana walipanga kuuwa watu ili wabaki madarakani
9. Mchakato wa Katiba Mpya kuanza. Hii litasemwa pia kwa ajili ya kuirubuni Jumuiya ya Kimataifa ili isichukue hatua kali dhidi ya Samia na Wahusika wote.
10. Hakuna vikosi wala silaha kutoka Zanzibar au Nje ya Tanzania vilivyoingizwa na Serikali kuwaua Watanzania. Hili litasemwa kujaribu kuwasafisha Samia, mtoto wake Abdul, mkwe wake Mchengerwa, DGIS Mombo, Chief of Staff JWTZ na Mkuu wa Kamandi ya Maji JWTZ wanaotuhumiwa kuingiza vikosi kutoka Zanzibar na Mercenaries kutoka Uganda, Msumbiji na Burundi kuwaua Watanganyika waliokuwa wanadai haki zao. Vikosi hivi vimeshiriki sana kuua watu zaidi ya elfu 10 na ikumbukwe pia inasemekana hili jambo limewaudhi sana askari wachache wenye akili waliopo JWTZ ambao wameapa kulipa kisasi.
Mwisho.
Kwa kuwa haya ndo yatakuwa sehemu ndogo tu ya matokeo ya inayoitwa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 2025, tunapenda kumwambia Samia na ccm yake kuwa watakapolalia ndipo tutakapoamkia. Hakuna Jiwe litasalia juu ya Jiwe safari hii. Yeye na Watu wake waliopanga na kufanya mauaji ya ndugu zetu lazima watachukuliwa hatua kali za kisheria kimataifa ikiwemo kukamatwa na kushtakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) pamoja na Mahakama nyinginezo za Nje ya Tanzania.
Huu uongo mnaopanga kuilisha dunia na Watanzania hakuna atakayeupokea na kuukubali. Hata Jumuiya ya Kimataifa itaukataa na kuendelea na taratibu nyingine za kuwashughulikia nyie wauaji.
Damu za ndugu zetu lazima zipate haki inayostahili kwa wahusika wote kuishia gerezani.