Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu 22 Septemba 2014, Uwasilishaji wa Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya

Watanzania ni wavumilivu sana..Yani huu uhuni ungekuwa unafanywa kwenye Nchi za Wenye Macho,Masikio na Akili sijui hali ingekuwaje..

Huu upigaji kura kwa njia ya Mitandao daah!!

Warioba alitoa tahadhari Wakamuona hana akili..

Tunaisubiri hiyo yenu CCM ..Malizeni Halafu tukutane Kitaa..Tutaheshimiana tu.
 

uhuni ni ule unaofanywa na CHADEMA mitaani mkuu kuwahamasisha vijana kuandamana wakati Mwenyekiti anakula bata BONDENI
 
Mkuu, kunitaka nimfanyie ushauri mtu mwingine ni jambo la kushangaza. Umeshindwaje kulibeba jukumu hilo kwa kuwa wewe ndiye umezozana naye? Anyway mimi naendelea kusoma updates tu, hayo mengine sina utaalam nayo.
Mkuu, nimekuomba uifanye wewe kazi hiyo kutokana na umahiri ulionao na uvumilivu wako. Hakika wewe ni kifani cha pekee. Tangu tumeanza mchakato huu hakika umekuwa kifani chema.mpole lakini na nimekubali ushauri wako. Nikuhakikishie kuwa mimi na Bramo hatuna ugomvi wowote. Ni tofauti tu ya mtazamo. Wote tupo hapa kuwahabarisha watanzania na wakati huo tunajenga mtandao wetu pendwa wa JF.
 

Wenzao wamesepa dakika za mwisho ili lukwrpa lawama na laana, lakini Wao hawakubali, wameamua kuwa nao kwa kuwafuata hulo huko ili Kama ni maana au lawama, basi na wagawane.
 
Mkuu inadhihirisha ule utafiti unaoonesha kuwa Tz wananchi wake IQ ziko chini. You can imagine hao wabunge kama ndio sample ya watz
umeona mkuu, watu wanalalamika mtaani vibaya sana, maisha magumu, haki haipatikani kwa sababu ya rushwa, lakini wanaowatungia sheria mama wanawatukana! sijui watanzania wakoje!
 
Makonda amemshangaa sana Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, FREEMAN AIKAELI MBOWE kuhamasisha vijana kuingia barabarani huku yeye akila Bata Afrika Kusini
 
Nadhani pia watalipwa POSHO YA KIKAO kwa kuwa watakuwa wamehudhuria kikao kwa remote!!

Sita kiboko yake Yusufu Makamba aliyebadili kanuni za uchaguzi ndani ya CCM kuwa zamu ya mgombea uspika kupitia CCM mwenye jinsia ya KE!!!!
 
Kificho amejibu baadhi ya hoja zilizojitokeza wakati wa mjadala. Kuhusu jinsi ya kupiga kura, anasema kuwa msingi mkuu ni wa kupiga kura ama ya wazi au ya siri. Anasema kuwa kwa walio ndani ya ukumbi ambao watapiga kura ya wazi. Wataitwa majina na watataja inara ambazo wanasema NDIYO na zile ambazo wanasema HAPANA. Kwa wale wa kura ya siri, watapewa karatasi ambazo watajaza ibara watakazounga mkono na zile wanazokataa kuhusu wale watakaokuwa nje ya bunge, watapelekewa karatasi ya aina mbili, yaani moja itaandikwa SIRI na nyingine itaandikwa WAZI. Wabunge watachagua aina ya karatasi. Kwa wale watakaochagua ya WAZI watajaza huko iliko na itqkuja kusomwa bungeni kwa kadri watakavyojaza wabunge wahusika
 
Wenzao wamesepa dakika za mwisho ili lukwrpa lawama na laana, lakini Wao hawakubali, wameamua kuwa nao kwa kuwafuata hulo huko ili Kama ni maana au lawama, basi na wagawane.

kwenda kuhiji siyo kutafuta laana mkuu, labda kama haujui thamani ya kuhiji. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum wao ndiyo wameomba waruhusiwe kupiga kura wakiwa huko, tusiwapotoshe wananchi.
 

Unajilazimisha kutoelewa wakati vitu vinaeleweka,,idadi ya wajumbe ipo katika mahesabu kila mjumbe ana maana kubwa sana,Bunge maalumu la katiba ni bunge maalumu na kura ya mjumbe ni kura maalumu na ana was bu wa kupiga kura,sijui umesema mambo ya kulipa posho kwa wanaokuwa bungeni tuu afu umesema wanaokuwa nje ya bunge kwa nini wapige kura,
Kumbuka mbunge halali ni yule aliejiandikisha na kuhudhulia mijadala mbalimbali,huyo akiwa nje ya bunge ni mjumbe halali na anapaswa kulipwa posho yake na ana haki na wajibu wa kupiga kura popote alipo.
 
Wajumbe wamehojiwa na Mwenyekiti SITTA na wote wamekubali kanuni zibadilishwe
 
johnmashilatu yuko mapumziko baada ya kazi kubwa ya kuandamana mwache kiongozi.
 
Nadhani Makamba alikuwa anamfahamu Sita kuliko Watanzania wengi. Huyu Sita is a curse to our nation. Inawezekana vipi mtu wa hovyo kabisa kama Sita kuna wakati fulani alipata heshima na sifa?
 
Kwahiyo ina maana hata swahiba wake ZZK aliishiwa hoja?
 
uhuni ni ule unaofanywa na CHADEMA mitaani mkuu kuwahamasisha vijana kuandamana wakati Mwenyekiti anakula bata BONDENI

Mkuu Cybercrime umesahau aliyevuruga mchakato yuko USA anakula bata ?? Tena kwa kodi zetu?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…