Elections 2015 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa

Elections 2015 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa

Mgufuli atamshinda mshikaji kiulaini sana na tutabaki tunaulizana nini kimetokea. Kura za mashibiki pekee hazitoshi mnahitaji kupata pia kura za watu makini wanaojielewa.

Hivi kuna tofauti kati ya kura za mashabiki na kura za watu makini? Hili ndio nilikuwa sijui, admittedly.
 
Watu wa chato hawana ubaguzi kama wale wa kiskazini. Watampokea na kumskiliza. Watu hawa si wale wanabaguana hata huko kwao jijini arusha kwa kuitana Arusha Asili na Arushamoshi. Hii tabia ya watu wa chato inanipa Tumaini kuwa Magufuli atawatumikia watanzania wote bila kuwabagua.

We endelea kutunga misamiati ya kibaguzi haitakusaidia. Arusha hii unayosema haipo popote mwongo mkubwa Mungu atakuhukumu kwa kutaka kutugawa . Huna tofauti na Lucifer. Nina ujasiri wa kukupinga kwa sababu nipo Arusha miaka 20 sasa hamna kitu cha namna hiyo
 
Yaani nchi tumkabidhi fisadi!!hapana haiwezekani
Mchawi mpe mtoto akulelee, hawezi kumroga kwa sababu unamfahamu. Ni afadhali mchawi unayemfahamu kuliko usiye mjua, atakumaliza bila kugahamu huku akiwasingizia wachawi wengine.
 
chadema muwe makini na mdundo mnaoucheza wa ngoma ya lowasa ya umati/mafuriko. siku hizi hotuba nzuri/mawe kwa utawala siyo tena ajenda yenu.
sikuwepo jana chato ila nimeishi chato kwa vipindi tofauti magufuli akiwa mbunge.
haijalishi ule umati wa chato ni wanachato au wanageita ila ukweli mchungu ni kwamba mkoani geita ukawa itapata pesa kura kiduchu sana za urais.
wekezeni kwenye siasa za ushawishi, mkiendelea kuwekeza nguvu kwenye kujaza watu pekee mtapotea kama wafuasi wa kibwetele
 
Unaweza kutupatia matokeo ya uchaguzi Serikali za mitaa hapo Chato? Ukipata au kutoa jibu ya swali hilo ndio hasa matokeo ya umati ule.
 
Makamba kandaganya jana..... Magufuli bila uraisi chato wasingempa ubunge... ubabe wake umemponza mpaka kwenye uraisi....EL the presida of Tz....
 
Unaweza kutupatia matokeo ya uchaguzi Serikali za mitaa hapo Chato? Ukipata au kutoa jibu ya swali hilo ndio hasa matokeo ya umati ule.

hapa namuongelea magufuli wala siiongelei ccm.
kwani magufuli aligombea uwakilishi serikali za mtaa?
 
Kinachofanya nikukubali siku zote ni uwazi wako, haijalishi wewe ni UKAWA. mnahitajika vijana wenye maono kama wewe.
 
Unaweza kutupatia matokeo ya uchaguzi Serikali za mitaa hapo Chato? Ukipata au kutoa jibu ya swali hilo ndio hasa matokeo ya umati ule.

kitu kingine ambacho chadema inajisahaulisha ni kwamba serikali za mitaa zilifanyika escrow ikiwa hot. walifaidika sana na kura za hasira.
kwa sasa richmond ndo hot. tabiri matokeo
 
hapa namuongelea magufuli wala siiongelei ccm.
kwani magufuli aligombea uwakilishi serikali za mtaa?
Huyo anayeleta hoja za matokeo ya serikali za mitaa kaishiwa. Na kama ndivyo basi CCM na itangazwe mshindi sababu aliwagaragaza vibaya wapinzani.
 
Back
Top Bottom