Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Kama Charles Kicheere ana akili nzuri, angeikataa kazi hii ya CAG. Naona atapata shida sana kwenye awamu zitakazokuja baada ya Magufuri. Amepewa nafasi kwenda kukiuka misingi ya u-CAG

Hivi zitakuwepo kweli awamu zingine?
Na ikiwepo tuombe lisijetoka jiwe kikaja kiazi.
 
jaji mfawidhi,

Kuna utofauti kati ya kipindi na Miaka. Katiba imesema miaka ila imetoa nafasi kwa sheria kuangalia kuweka umri wowote unaofaa... Sheria imeweka vipindi wa utawala wa CAG na haijaweka ulazima wa kuteuliwa tena. phrase 'shall be eligible' humaanisha kuwa na vigezo stahiki (having necessary quality/satisfy requirements)

Therefore katika kipindi cha pili CAG anaweza kuwa na vigezo stahiki lakini sio lazima ateuliwe tena. huenda unachoweza kukimbia mahakamani kukichallenge ni legality ya kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Hesabu za Umma juu ya vipindi hivyo viwili. Katiba imetaja miaka na sio vipindi.
 
Hivi zitakuwepo kweli awamu zingine?
Na ikiwepo tuombe lisijetoka jiwe kikaja kiazi.
Hata asipotoka kwa sanduku la kura atatoka kwa njia ambayo Mungu mwenyewe anajua. Hawezi kuiacha Tanzania kwenye mkono ya shetani.
 
Tutaona sasa sheria na Katiba ipi yenye nguvu. Maana tunaambiwa "when the law(s) contradict(s) with the constitution the constitution the constitution shall prevail"
 
Ni vyema kama umetambua kuwa Mfumo wa Uongozi wa JPM ni Data za upishi upishi na ujanja ujanja. Nakuhakikishia ripoti inayofuata itaonyesha faida kubwa sana kwenye mashirika ya UMMA. Tutasahau kabisa kuwa ATCL itamaliza kupata hasara mwaka 2023
kocha yoyote akiona mchezaji performance yake huwa anatoa anaweka mwingine ndicho kilichotokea hamna kingine ili apate matokeo mazuri ashinde mechi
 
Nasikia Assad kapata bonge la mkataba serikali ya Sweden
 
Influenza,

Rais anasema hawezi kupewa mamlaka ya kuteua akakosa mamlaka ya kutengua. Tumwulize anaweza kutengua uteuzi wa jaji mkuu ama jaji yoyote wa mahakama kuu?
 
Hivi Dodoma kashindwa kabisa kwenda uko? Nashindwa kuelewa kabisa ilikuwa ni siasa au mkakati nilitegemea mambo kama aya yafanyike Dodoma maana juzi tu kasema kashaamia uko.

Kwa hiyo wewe Technically unataka kumpangia rais shughuli zake? Kwa nini usingeuliza sababu? Mtakalia kuropokaropoka tu humu JF.
 
" Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema, usije ukaenda huko ukajifanya na wewe ni mhimili, mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa, na katika kiapo chako nilikuwa nakisikiliza nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwahiyo mwenye Serikali yupo "- @MagufuliJP #MwananchiUpdates

Hebu tujadili zaidi.
 
Sasa kajiteulia wa kulinda wizi wao wa kuchukua pesa BOT muda wowote kama ilivyokuwa kwa marehemu Mobutu Sese Seko wa Congo.

Grow up and be respectful to your president, huwezi kumlinganisha na huyo kichaa. Kuweni na shukrani na democracy ambayo ameileta JPM na kukuza uchumi wa Tanzania. JK mlimwita Vasco Da Gama na mnafahamu Hazina hakukuwa na fedha alipoondoka hata vifaranga vyake vilikuwa na biashara huyu anafanya juhudi za kufufua uchumi mnaanza tena hadithi za Abunuwasi na Bulicheka.
 
Huo Ndio ukweli

CAG sio muhimili wa serkali ila ni mfanyakazi wa serkali

Huyu CAG Mstaafu aliingizwa kichwa na wanasiasa wachumia tumbo akajiona Ndio mwamba

Akapumbumzike alee wajukuu
 
Tutaona sasa sheria na Katiba ipi yenye nguvu. Maana tunaambiwa "when the law(s) contradict(s) with the constitution the constitution the constitution shall prevail"
Inabidi ikatafutwe tafsiri ya kimahakama na baada ya hapo ndipo mabadiliko yafanywe kuputia Bunge.
 
Umejitahidi kufafanua lakini huyo Magufuli keshaamua hivyo, ingewezekana mtu kuombewa mauti ningewashauri mumuombee lakini ndio hivyo tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…