Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

CAG kaagizwa na Amiri jeshi atii maelekezo ya mihimili mingine

Kakumbushwa anaweza kutolewa hata baada ya mwaka mmoja

Vikatiba katiba vyenu wekeni kabatini mpaka 2026

Watanzania wanatakiwa kuwa waangalifu sana; tuliyaona NSSF kule.. watu wanatengeneza mashujaa wao. Alichosema rais hapa miye nitakuwa mwangalifu sana. Anajua nini kule ofisi ya CAG? Labda tusubiri tuone nini kinaendelea sidhani kama hii picha imeisha.
 

Unaweza kutueleza aliacha kiasi gani pale kwenye hazina ya taifa? Awamu hii nafahamu ndio imevunja record kwa kuweka figures za Gov reserves.

BTW Swali hili niliuliza wakati JK ameondoka na halikupata majibu. Unaweza kulipata kwenye makabrasha ya JF.
 
Wasalaam,

Nimefuatilia hotuba baada ya zoezi la kula kiapo nikastuka sana na kustaajabu kusikia ile kauli kwamba CAG anaweza kutumbuliwa hata ndani ya mwaka mmoja. Nikajiuliza haya ni maelekezo au vitisho?

Baada ya kutafakari nikagundua kuwa Katiba yetu ya mwaka 1977 imempa Rais mamlaka makubwa ya kimaamuzi pia nikakumbuka maneno ya Mwl Nyerere kwamba kwa Katiba hii angeamua kuwa dikteta asingeshindwa. Hii inaashiria Katiba yetu ina mapungufu makubwa sana na ni Katiba iliyotungwa wakati wa utawala wa chama kimoja na sasa tuna vyama vingi vya siasa.

Kwa muktadha huu nina hofu kama CAG mpya atatekekeza majukumu yake kwa uwazi na waledi maana muda wote atakua na hofu ya kutumbuliwa na muhimili mnene kuliko yote, kwa maana nyingine atalazimika kufanya kazi za ukaguzi kwa kufata maelekezo kutoka juu kwamba hapa kagua na pale usipaguze usikague km unataka kibarua kiendelee kuwepo maana atakua na nidhamu ya uoga.

Mungu ibariki Tanzania siku moja tupate katiba mpya kwa ustawi wa taifa hili.
 
Hawa wanaopiga makofi na kushangilia magogoni wanamaanisha au wanaogopa kufyekelewa mbaliiiiii!!!!
Mkulu akirudia kuangalia hilo tukio kwenye TV akabaini ulikuwa hupigi makofi au tabasamu fyekelea mbaliiii!!!
 
Rais Magufuli: Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema. Usiende huko ukajifanya Muhimili. Mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa Mahakama, Bunge na Sisi wa Serikali - Katika Kiapo chako ni Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo

Rais Magufuli: Kafanye kazi zako za ukaguzi vizuri bila kuonea mtu. Unapopewa kazi na Mihimili mingine kama Bunge, katekeleze. Usibishane nao - Ukipewa maagizo na Mahakama katekeleze, wewe ni Mtumishi. Lakini pia kasimamie hiyo ofisi, kasimamie watendaji wako MIMI NINAVYO JUA, KATIBA YETU INAMPA MMLAKA CAG . KUWA HATAINGILIWA NA MUHIMILI WALA MTU YEYOTE ATAKAPOKUWA AKITIMIZA MAJUKUMU YAKE YA KAZI. Hii imekaaje ?.
 
Kwamba akiambiwa "hapa usiguse basi apite kimya,"...... Wizi unaendelea
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania Endelea kuchapa kazi

Wale wasaliti wa nchi sijui wataweka wapi sura zao
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania Endelea kuchapa kazi

Wale wasaliti wa nchi sijui wataweka wapi sura zao
 
Unayo hoja. Haya ndio mambo angalau ya kujadili sio neno SHALL..
 
Hakuna aliye huru awamu hii,kila kiongozi analazimishwa kupiga 'kagoti flani'...najiuliza wanavyompamba na kumwogopa hivi ikiibuka ile 666 kunamtu atapinga kweli!??
Ogopa mtu anakwambia kuna 'mwenye' serikali sio kuna 'wenye'... inamana serikali ni yake sio ya wananchi...basi nchi ni yake pia maana anaamua apendavyo!!! Aibu ajabu,bora tungekuwa hatujawahi onja demokrasia.
 

Hata Mwanamke kabla hujaanza Kufanya nae Mapenzi ukimtishia tu hawezi tena kuwa na Furaha na Tendo lenyewe na hata akikupa atakuwa anatimiza tu wajibu ili usije ukamtoa Ngeu bure au Kumtengua Bandama. Namuonea sana Huruma CAG mpya kwani huenda akawa kweli ni Mtu sahihi kwa hiyo nafasi ila kwa aina ya ' Mikwara ' ya Kimamlaka kutoka kwa ' Mwenye Serikali ' hapo atakuwa ni Mtu wa ' Kuburuzwa ' mpaka aliyemteua atakapomaliza muda wake Madarakani achilia mbali ile ya 7 X 2 anayotaka kuitengenezea Mazingira Kikatiba hasa ndani ya Chama ili aanze nayo hapo 2025 kama Mwenyezi Mungu atatuweka Hai wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…