Wasalaam, nimefatilia hotuba baada ya zoezi la kula kiapo nikastuka sana na kustaajabu kusikia ile kauli kwamba CAG anaweza kutumbuliwa hata ndani ya mwaka mmoja. Nikajiuliza haya ni maelekezo au vitisho? Baada ya kutafakari nikagundua kuwa katiba yetu ya mwaka 1977 imempa rais mamlaka makubwa ya kimaamuzi pia nikakumbuka maneno ya mwl nyerere kwamba kwa katiba hii angeamua kuwa dictetor asingeshindwa hii inaashiria katiba yetu ina mapungufu makubwa sana na ni katiba iliyotungwa wakati wa utawala wa chama kimoja na sasa tuna vyama vingi vya siasa.
Kwa muktadha huu nina hofu kama CAG mpya atatekekeza majukumu yake kwa uwazi na waledi maana muda wote atakua na hofu ya kutumbuliwa na muhimili mnene kuliko yote, kwa maana nyingine atalazimika kufanya kazi za ukaguzi kwa kufata maelekezo kutoka juu kwamba hapa kagua na pale usipaguze usikague km unataka kibarua kiendelee kuwepo maana atakua na nidhamu ya uoga.
Mungu ibariki Tanzania siku moja tupate katiba mpya kwa ustawi wa taifa hili.