Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Novemba 4, 2019 kuanzia majira ya saa tatu na nusu (3:30) asubuhi atawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni



Wanaoapishwa ni pamoja na;
1. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG)

2. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.

3. Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait.

4. Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu

Aidha, Mhe. Rais Magufuli anawaapisha Majaji 12 wa Mahakama Kuu
*****

View attachment 1253571
Charles Edward Kichere akiapishwa kama Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)​

Woyoooooooooo.....
 
Hapo kwenye kutengua,mbona Assad alishindwa kumtengua?

Mkuu ni kwamba alimuacha tu, lakini angeweza kumuengua bila hata kujali hiyo katiba. Kwa ujumla hana woga wowote kwenye kuvunja katiba. Anatii hisia zake zaidi kuliko hiyo katiba. Na hata akiivunja hiyo katiba ni mamlaka ipi inaweza kumchukulia hatua?
 
Maoni ya Profesa

1572856377826.png
 
Kwa nini ni wakumulikwa na tochi? Ni katika stage gani huwa wanajifunza upigaji?
Kuna familia zingine kule nasikia ni hatari mtoto hata akiwa shule za msingi labda darasa la sita hivi Kama mzazi hajawahi sikia kuwa mwanae kaiba chochote Hadi anafikia darasa la sita anamkamata mtoto anampeleka kwa mganga wa kienyeji amwangalizie mwanae Ana tatizo gani? Karogwa au Nini? Kwa Nini Hadi anafikia darasa la sita hajawahi yeye mzazi sikia kuwa mwanae kaiba Cha mtu hata Cha mwanafunzi mwenzie ? .Mzazi anaona sio kitu Cha kawaida hasa kwa mtoto wa kiume
 
Wakisemwa Wasukuma waliojazana Hazina kwa sasa mnasema tunahubiri ukabila, kwa vile mume wenu kataja kabila msilolipenda mmetoka kama mwewe. CHENGE ni Mchaga wa Uru au Kiboroloni?
Ukisikia paaaaa
 
Mentality ya kijinga kabisa ufisadi hauna kabila, Makonda Anayejenga hotel ya kisasa ya mabilion wakati analipwa chini ya mshahara wa ml 10 kwa mwezi vipi na yeye ni mchaga? wakina Lugumi, Chenge, Ngereja wote hao ni wachaga?

Yaani sizani kama kuna kabila bongo ambalo halijiusishi na ufisada kama lipo basi halijapata fulsa.
 
Ile power aliyoondolewa Assad Kachere atarudishiwa?
 
Maagizo kwa CAG ni vitisho!Ipo haja ya kupata katiba bora. Ni dhambi dunia ya leo kuumpa mwadamu nafasi ya pili baada ya Muumba.
Huo ndio ukweli ,ameambiwa ukweli huu na mamsifu mh.rais kwa kusema ukweli

State agent
 
Anamuapisha CAG mteule, anasema maneno ya msingi sana.

1. Usiende kujifanya na wewe ni Muhimili, Mihilimi ni mitatu tu. (ASSAD alijiona muhimili eeh)

2. Una nidhamu sana, unatenguliwa hapa, na pale, lakini haulalamiki

3. Una elimu nzuri na uzoefu wa kazi.
Nimesikia neno mwenye Serikali yupo, daah tumefikia hapa.
 
Anamuapisha CAG mteule, anasema maneno ya msingi sana.

1. Usiende kujifanya na wewe ni Muhimili, Mihilimi ni mitatu tu. (ASSAD alijiona muhimili eeh)

2. Una nidhamu sana, unatenguliwa hapa, na pale, lakini haulalamiki

3. Una elimu nzuri na uzoefu wa kazi.
Huyu jamaa anakumbuka aliyosena siku anamtumbua TRA?
 
Magufuli kamuapisha jaji mmoja, ambaye ni mchagga na alikuwa fair competition,

Anasema jamaa alivyo muadilifu hadi alipokuwa Fair competition watu walikuwa wanajiuliza "Huyu ni Mchagga gani asiependa Rushwa"

Alisema Makonda, kuwa Mengi alikuwa ni mchagga wa pekee, Mchaga gani anaesaidia Yatima, na leo Baba nae amewakilisha mawazo ya wengi, walio kuwa kumbe watu wengi hushangaa wakiona mchagga, haibi, hapokei rushwa, na anasaidia watu!

Swali Wachagga mlifikaje hapa, kwenye jamii kuwaona namna hii?
Baba nae kasema! haya watuambie walifikiaje jamii kuwapa alama ya wizi!!
 
Back
Top Bottom