Yaliyojiri JamiiForums Space kuhusu Maambukizi ya COVID-19 na Utoaji Chanjo Tanzania

Yaliyojiri JamiiForums Space kuhusu Maambukizi ya COVID-19 na Utoaji Chanjo Tanzania

Thanks 🙏🏾 to Shangazi Maria Tseshai Sarungi Space ya kule Twitter sasa inapaa kwa umaarufu. Bidada ni mzuri ile mbaya halafu sauti yake sasa na anavyojua kuongea kwa ufasaha na pozi oyooooo!
Jamii Forums inakukaribisha kushiriki kwenye Mjadala kuhusu Maambukizi ya #COVID19 pamoja na Utoaji wa Chanjo nchini Tanzania

Mjadala huu unafanyika Agosti 6, 2021 kupitia Twitter Spaces (JamiiForums) kuanzia Saa 12 jioni na utahusisha Wataalamu wa Afya watakaozungumzia Masuala anuani kuhusu Janga hili

====

UPDATES;1800hrs

======

Kufuatilia mjadala huu, fungua hii link.

#UVIKO3
View attachment 1882254
 
Ikiwa mtu akichanja mwili wake unafanyika sumaku, hii haiondoi uasili wa mwili ulivyoumbwa kweli?

Pili,

Chanjo hizi ni kwa nini zinaruhusu kirusi amwingilie tena aliyenachanjo na hata kusababisha kifo?
Kama ndivyo, nini yofauti kati ya aliyechanjwa na asiye na chanjo
 
We umeona wapi mwili unafanyika sumaku
 
Kuna jamaa anasema ukisogelea zile spika za mchina unasikia "Ze blutus divaisi iz rede to pea" ...wabongo kila mtu ni mtaalamu kwenye hili suala la chanjo ya kovidi [emoji1787]
Huo ni uongo mtupu mkuu,hakuna vitu kama hivyo tatizo watanzania tunapenda sana habari ambazo hazina mashiko.
 
Chanjo hizi ni kwa nini zinaruhusu kirusi amwingilie tena aliyenachanjo na hata kusababisha kifo?
Chanjo haizuii kirusi kuingia mwilini mwa aliyechanjwa. Chanjo inasaidia kuupa uwezo mwili kupambana na hicho kirusi.

Chanjo pia haiwezi kuwa na ufanisi wa 100%. Kama itathibitika kuwa na ufanisi km 90%, wanaokufa baada ya kupata chanjo wanaweza kuwa kwenye hilo kundi la 10%.

Hatari kwa baadhi ya chanjo za covid19 ni kwamba zipo baadhi zisizofikia hata ufanisi wa 60%. Bahati mbaya sana ndizo tunapewa kwenye huo mpango wao wa covax.
 
Kuna jamaa anasema ukisogelea zile spika za mchina unasikia "Ze blutus divaisi iz rede to pea" ...wabongo kila mtu ni mtaalamu kwenye hili suala la chanjo ya kovidi [emoji1787]
Nimecheka sana. Nimeona huu ujumbe wakati ninakawasha haka Karadio nisikilize BBC. [emoji1787][emoji1787]
IMG_20210806_183447_242.jpg

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Dkt. Francis: Watu wengi wanaogopa kwenda kuchanjwa kwasababu ya Uoga. Mitandao ya kijamii ina taarifa nyingi ambazo zimepotosha Watu

Mbele ni kuzuri ila cha msingi tuendelee kuwapa Watu taarifa sahihi. Mtu akiona mwenzie hajapata tatizo naye atakwenda kuchanjwa

#UVIKO3
 
We umeona wapi mwili unafanyika sumaku
😂 Samahani mkuu, nimetoa swali hili kwa wataalamu, wewe ungekaa kimya kwa sababu huna hiyo elimu, wenye taaluma zao hawawi kama wewe, nyamaza!
 
[emoji23] Samahani mkuu, nimetoa swali hili kwa wataalamu, wewe ungekaa kimya kwa sababu huna hiyo elimu, wenye taaluma zao hawawi kama wewe, nyamaza!
We umejuaje kwamba mimi sio mtaalamu?
 
Naomba Dr anijibu kwa nini tuchanjwe ili hali inasemekana(kutoka WHO) baada ya muda flani wa kuchanjwa itatakiwa tena kupata chanjo nyingine ya kubust chanjo za mwanzo, huoni kama itafika wakati tutatakiwa kubust kinga tena ili chanjo iwe effective kitu ambocho itakua ni tegemezi kwa maisha ya baadae na natural immunity itakua sio effective tena, kwa lugha rahisi tutakua wateja wa chanjo mpaka tunakufa,
 
We umejuaje kwamba mimi sio mtaalamu?
Wataalamu hawajibugi kama ulivyojibu wewe, Labda uwe mtaalamu asiye na wito, wataalamu kama nyinyi, ndio wale Baba anakwambia mwanangu nataka uwe doctor na wakati wewe fani yako ni jeshi, ndiyo maana tuna madakitari wakali misiri ya police
 
Kwanza uliuliza swali vibaya,ungeuliza je ni kweli mtu akichanjwa mwili unakuwa na sumaku?,jibu lingekuwa ndio au hapana,na maelezo mengine ungepata...Sasa wewe mkuu umekuja moja kwa moja na majibu yako ndio mana nikakuuliza umeona wapi hicho ulichosema?
 
Dr. Francis& Dr. Mariam: Kuvaa Gloves unatakiwa kila Gloves moja mtu mmoja, kwahiyo kwa siku mtu anayetoa chanjo anatakiwa avae Gloves 400. Hivyo kutokuvaa gloves ni rahisi hata kusafisha mikono kila baada ya kuchanja kuliko kuvua na kuvaa gloves. Pia muongozo wa Kuchanja unaruhusu kuchanja bila gloves
Mimi naona kuvaa gloves ni vizuri zaidi kuliko kunawa mikono, hapa naona tunarahishisha mambo kwa kukwepa gharama za gloves kwa kisingizio eti mtu atavaa gloves 400.

Sheria za afya kwa mtoa huduma anapotoa huduma zinasemaje kwani? Tuanzie hapa
 
Kwanza uliuliza swali vibaya,ungeuliza je ni kweli mtu akichanjwa mwili unakuwa na sumaku?,jibu lingekuwa ndio au hapana,na maelezo mengine ungepata...Sasa wewe mkuu umekuja moja kwa moja na majibu yako ndio mana nikakuuliza umeona wapi hicho ulichosema?
Sawa mkuu, Unajua mkuu, hakuna mtu nayemheshimu kama matabibu aisee, hawa watu ni wa kuheshimu sana, kwanza wako smart sana, hawana nongwa na mtu yeyote, hata angelikuwa ni mchagfu kuliko binadamu awavyo,

Niliingiwa na mashaka juu ya jibu lako, lakini sasa naomba unijibu swali langu mkuu,

tumekuwa tukiona clip mbalimbali kutokea ng'ambo huko, miili ya watu ikishika vitu vya chuma sehemu waliochanja, je hiyo haina shida ktk mwili wa binadamu
 
Thanks [emoji1488] to Shangazi Maria Tseshai Sarungi Space ya kule Twitter sasa inapaa kwa umaarufu. Bidada ni mzuri ile mbaya halafu sauti yake sasa na anavyojua kuongea kwa ufasaha na pozi oyooooo!
Haya sasa, here we go. Tukiwaambia chadema ni zero brain tunaambiwa mataga sukuma gan and the likes. Badala mtu uchambue na kuskiliza ubora wa content anayoongea muhusika ww unaanza kusifia uzuri wa mtu, mara sauti yake mara mapozi..aisee hii nchi wacha CCM tuendelee kuiongoza kamwe hatuwezi kuwapa wapuuz kama hawa nchi.
Pamoja na kwamba CCM kuna wapuuzi pia ila % yao ni ndogo kulinganisha na hawa jamaa..
 
Back
Top Bottom