Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Tumezidi kuwa wajinga na walalamikaji ndio maana wanafanya watakavyo ila kuna mwisho hata mbwa koko unapo mchokoza kila siku ipo siku atakuonyesha adabu
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri anatembelea vituo akiwa ameambatana na viongozi wa ccm.

Sheria za uchaguzi haziruhusu viongozi wa vyama vya siasa kupiga kambi kwenye vituo vya uchaguzi.

Hii imeweza kutokea Ngarenanyuki tu mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzu kutembea na viongozi wa ccm.

mkurugenzi akiwa ameambatana na makada wa ccm wamewanyang'anya mawakala wa vyama daftari lenye majina ya wapiga kura.

Safari ya demokrasia kwa nchi yetu bado sana.
Hii haikubaliki popote.

Tume ya taifa ya uchaguzi kwa mtindo huu huu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.
 
Ivi cuf si walisusa uchaguzi hawa kulikoni tena?
 
Wakuu mtusaidie tujue mini kinaendelea kuhusu chaguzi ndogo zinazofanyika nchi nzima. Mi nadhani tungepeana updates hapa jukwaan, maana nasikia huko Zenji kuna sintofahamu Kati ya polisi na wananchi baada ya mawakala wa cut kutolewa na kuwekwa kizuizini. Wenye taarifa sahihi mtujuze!! Wahadha Salaam aleykum!!
Huko zenj kuna chama kipya kinaitwa cut?
 
Kuendelea kulalamika hakutusaidii bali tunapaswa kutafuta mbinu za kukabiliana na huu uharamia maana tumeshalalamika sana na kwa miaka mingi na hakuna kinachobadilika.
 
Sasa wamechukua daftari mnakimbilia jf kushitaki,wapuuzi kabsa mnataka mumbembelezwa na Nani...walikua wangapi ....piga ngumi hao
 
Heko CCM Na M a DED Kazi nzuri hiyo ndio Demokrasia wapinzania wakileta fujo Polisi iwakamate Na Mahakama iwafunge bila faini
 
Wakala wa chadema aliyepo Kituo cha uchaguzi kijichi B Mh. CCaro Kazinza kakamatwa na polisi, na kituoni kwake hakuna wakala kwa sasa. Wakala wa akiba dada Salma Sharif alitaka kwenda kusimamia lkn naye amefukuzwa. Watu katika eneo hilo wanakimbizwa na kukamatwa ovyo. Katika pitapita yangu nimekutana na watu ambao wanasadikiwa kuwa ni wana CCM walikuwa wakisema hawatakubali kushindwa kwani watatumia hata goli la mkono.

Haya waangalizi na washabiki wa demokrasia tunaomba mliangalie hili kwa jicho la pekee. Kwani huu ni uchaguzi mdogo tu wa udiwani, je wa ubunge na urais itakuwaje?
Acha majungu, weka picha si uko huko?
 
Heko CCM Na M a DED Kazi nzuri hiyo ndio Demokrasia wapinzania wakileta fujo Polisi iwakamate Na Mahakama iwafunge bila faini
Naunga mkono hoja, endesha nchi kidicto..pitisha kwa nguvu Wa upande wetu hata kama hapendwi na wananchi tutamlinda, atakayeleta fyoko kama tia ndani. Walizoea kubembelezwa awamu hii ubabe mbele hakuna kulemba.
 
Huyu DED namfahamu ni mmojawapo wa waliopewa zawadi na mkuu yaani zawadi ya U-DED na hivyo amekuwa mtu asiyejiamini kabisa . Amedhamiria lazima CCM ishinde ili kukwepa kutumbuliwa
 
Back
Top Bottom