Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Tumezidi kuwa wajinga na walalamikaji ndio maana wanafanya watakavyo ila kuna mwisho hata mbwa koko unapo mchokoza kila siku ipo siku atakuonyesha adabu
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri anatembelea vituo akiwa ameambatana na viongozi wa ccm.

Sheria za uchaguzi haziruhusu viongozi wa vyama vya siasa kupiga kambi kwenye vituo vya uchaguzi.

Hii imeweza kutokea Ngarenanyuki tu mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzu kutembea na viongozi wa ccm.

mkurugenzi akiwa ameambatana na makada wa ccm wamewanyang'anya mawakala wa vyama daftari lenye majina ya wapiga kura.

Safari ya demokrasia kwa nchi yetu bado sana.
Hii haikubaliki popote.

Tume ya taifa ya uchaguzi kwa mtindo huu huu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.
 
Ivi cuf si walisusa uchaguzi hawa kulikoni tena?
 
Huko zenj kuna chama kipya kinaitwa cut?
 
Awamu hii tutaona mengi sana....

Ova
 
Kuendelea kulalamika hakutusaidii bali tunapaswa kutafuta mbinu za kukabiliana na huu uharamia maana tumeshalalamika sana na kwa miaka mingi na hakuna kinachobadilika.
 
Sasa wamechukua daftari mnakimbilia jf kushitaki,wapuuzi kabsa mnataka mumbembelezwa na Nani...walikua wangapi ....piga ngumi hao
 
Heko CCM Na M a DED Kazi nzuri hiyo ndio Demokrasia wapinzania wakileta fujo Polisi iwakamate Na Mahakama iwafunge bila faini
 
Acha majungu, weka picha si uko huko?
 
Heko CCM Na M a DED Kazi nzuri hiyo ndio Demokrasia wapinzania wakileta fujo Polisi iwakamate Na Mahakama iwafunge bila faini
Naunga mkono hoja, endesha nchi kidicto..pitisha kwa nguvu Wa upande wetu hata kama hapendwi na wananchi tutamlinda, atakayeleta fyoko kama tia ndani. Walizoea kubembelezwa awamu hii ubabe mbele hakuna kulemba.
 
Huyu DED namfahamu ni mmojawapo wa waliopewa zawadi na mkuu yaani zawadi ya U-DED na hivyo amekuwa mtu asiyejiamini kabisa . Amedhamiria lazima CCM ishinde ili kukwepa kutumbuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…