Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Hivi msimamizi bado ni Jecha aliyehaidiwa zawadi ama?
 
Hahaha. CCM oyeee!!!!. Watani wanalia lia tu.
 
CCM naipenda sana. Hapa tunachinja. Watani wetu wanakodoa kodo wanakodoa.
 
Leo ndo leo uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na uchaguzi wa madiwani kata 20 Tanzania bara.

Ni chaguzi zitazotoa mwelekeo na mabadiliko na ukubalikaji wa vyama tangu uchaguzi mkuu wa 2015.

Karibuni tupeane updates na matukio yanayojiri huko.

.......Updates...........

* Uchaguzi wa Ubunge unafanyika kwenye jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini Magharibi – Zanzibar

Uchaguzi wa madiwani unafanyika kwenye kata Ishirini (20) katika Halmashauri Kumi na Tisa (19) za Tanzania Bara, kata hizo ni...

1. Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha),
2. Igombavanu (Mufindi DC, Iringa),
3. Ikweha (Mufindi DC, Iringa),
4. Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro),
5. Ihumwa(Dodoma MC, Dodoma),
6. Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam),
7. Kahumulwa (Sengerema DC, Mwanza)
8. Maguu (Mbinga DC, Ruvuma),
9. Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma),
10. Kimwani (Muleba DC, Kagera),
11. Kinampundu (Mkalama DC, Singida),
12. Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
13. Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi),
14. Duru (Babati DC, Manyara),
15. Malya (Kwimba D.C, Mwanza),
16. Misugusugu (Kibaha TC, Pwani),
17. Mateves (Arusha D.C, Arusha),
18. Nkome (Geita DC, Geita),
19. Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na
20. Tanga (Songea MC, Ruvuma)
--
siyoi koroi, Uchaguzi udiwani Kata ya Ngarenanyuki DED na ccm wapora daftari la wapiga kura.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri anatembelea vituo akiwa ameambatana na viongozi wa ccm.

Sheria za uchaguzi haziruhusu viongozi wa vyama vya siasa kupiga kambi kwenye vituo vya uchaguzi.

Hii imeweza kutokea Ngarenanyuki tu mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzu kutembea na viongozi wa ccm.

mkurugenzi akiwa ameambatana na makada wa ccm wamewanyang'anya mawakala wa vyama daftari lenye majina ya wapiga kura.

Safari ya demokrasia kwa nchi yetu bado sana.
Hii haikubaliki popote.

Tume ya taifa ya uchaguzi kwa mtindo huu huu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.

--
Francis12, UPDATES MCHAGUZI MDOGO JIMBO LA DIMANI Z'BAR.

Kumetokea mgogoro kati ya mawakala wa CUF na Askari Polisi. Hali hii imepelekea mawakala wa CUF kuondolewa kwa nguvu kwenye vyumba vya kupigia kura na hivyo mawakala wa CCM kubaki peke yao.

Sababu za mgogoro huu ni kama ifuatavyo:

-Mawakala wa CUF amegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tiki kwa mgombea wa CCM.

-Mawakala wa CUF wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na wameruhusiwa kupiga licha ya majina yao kukosekana kwenye daftari.

-Chumba number 6 kituo cha Kibondeni, imegundilikana kwamba masunduku yote yaliyopo yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tayari.

-Wapiga kura wengi jimbo la Dimani ni hewa.

-Police wameanza kupiga watu maeneo ya Fuoni kituo cha Kibondeni baada ya watu hao kudai kuna kura feki kwenye kituo hicho.

-Katika kituo hicho cha Fuoni mabasi yamekua yakisomba watu na kuwaleta kupiga kura. Watu hao si wakazi wa jimbo la Dimani. Picha hapo chini inaonesha moja ya mabasi yanayotumika kusomba watu na kuwapeleka vituoni kupiga kura.
Umeanza uzushi sasa yaani kipindi hiki masanduku yakamatwe?
 
Dimani uko kwakua anafanya fisiemu wala hawarejei uchaguzi
Reporter wetu tutumie n picha za matukio
 
Kazi ya mawakala sio kushika daftari la majina na kuanza kuhakiki majina hiyo ni kazi ya tume
 
Back
Top Bottom