REF/AB/T/001/2017 22/01/2017
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Dar Es Salaam
YAH: UCHAGUZI WA VURUGU
Tafadhali husika na mada ya barua hii kama inavyojieleza hapo juu.
Mhe. Mkurugenzi wa Uchaguzi, kama Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya THE CIVIC UNITED FRONT CUF- Chama Cha Wananchi) napenda kueleza kwako ukiukwaji wa Sheria na taratibu za uchaguzi unaofanywa katika vituo mbali mbali vya uchaguzi kama ifuatavyo:-
1. Kutolewa kwa Mawakala wa Upigaji Kura wa Chama Cha CUF kinyume na sheria ya Tume yaTaifa ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 (Sura ya 343), na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Na. 4 ya mwaka 1979 (Sura ya 292): Katika hali isiyotarajiwa, Mawakala wa Chama changu wametolewa na kudhalilishwa katika vituo vya kupigia kura, Kwa Mfano: Abeid Majid Abeid (Bweleo, Chumba Na. 1), Yunus Masoud Gharib (Bweleo, Chumba Na. 2), Abdi Mustafa Habib (Uwandani, Chumba Na. 6) wametolewa katika vituo vya uchaguzi. Pia tumeshuhudia mawakala wa vyama vyengine wasiokuwa wa CCM wametolewa katika vituo vyao vya kupigia kura, Kwa Mfano: Shani Khatib Khamis (NRA, Fumba, Chumba Na. 2), Mbarouk Ali Haji (NRA, Uwandani, Chumba Na. 3), Ibrahim Muharam Mwinyi (NRA, Uwandani, Chumba Na. 4), Suleiman Othman Omar (CHAUMMA, Kisakasaka, Chumba Na. 2), Masoud Khamis Ramadhan (CHAUMMA, Uwandani, Chumba Na. 3) wote wametolewa kwenye vituo bila ya sababu za msingi kwa lengo maalumu la kukinufaisha Chama Cha CCM.
2. Kubadilishwa kwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK): Itakumbukwa kwamba tarehe 25/10/2015 kulifanyika uchaguzi wa Mbunge wa Dimani na Chama Changu kilipatiwa Nakala ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ni jambo la makusudi ambalo limeratibiwa na Tume yako kuandaa Daftari jipya ambalo leo wamepatiwa wasimamizi wa Vyumba vya Uchaguzi likiwa tofauti na lile lililotumikguzi Mkuu wa Oktoba,2015.Vile vile Mawakala, wangu wamegunduwa katika baadhi ya maeneo, wapiga kura halali wametolewa katika vyumba vya kupigia kura wakikoseshwa haki zao za msingi za kuchagua Mbunge wa Jimbo lao la Dimani huku wakishuhudia makundi ya wapiga kura kutoka nje ya shehia zao wanaruhusiwa kupiga kura.
3. Kuruhusiwa kwa Wapiga Kura Haramu kupiga kura: Katika hali ya kusikitisha, wapiga kura kadhaa wameripotiwa kupewa shahada za kupigia za watu wengine na kuruhusiwa kupiga kura na wasimamizi wa vituo vya uchaguzi!
4. Uchaguzi kukabidhiwa na kuendeshwa na Jeshi la Polisi na kuingiliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania: Kwa mujibu wa Sheia ya Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio yenye mamlaka ya kusimamia na kuendesha uchaguzi hapa Nchini; hali inayoonekana katika vituo vyote vya uchaguzi ni kuachiwa Polisi na JWTZ kuendesha uchaguzi na kufanya wanavyotaka wakati wote kwa mfano:Tumeliona gari la JWTZ Na: 3579 JW 14 likichukuwa makundi ya watu wasiokuwa wapigakura wa Dimani na kuwapeleka katika vituo vya kupigia kura vya Fuoni Kibondeni na Kituo cha Skuli ya Sekondari ya Fuoni. Jeshi la Polisi nalo ndilo lenye kazi ya kuwatoa Mawakala pamoja na wapiga kura halali katika viyuo vya kupigia kura kinyume na taratibu za uchagzuzi.
Uchaguzi unaoendeshwa kwa mtindo huu hauwezi kuitwa uchaguzi wa haki na huru na hauwezi kuakisi maamuzi ya wapiga kura.
5. Upigaji wa kura wa Wafu: Tumegunduwa katika vituo mbali mbali wanaletwa watu wasiojulikana na kuwapigia kura watu waliofariki.Mfano mzuri ni ule unaonihusu mimi mwenyewe.
Dada yangu khalisi: Samia Khatib Ramadhan ambaye alifariki tarehe 5 Januari,2017,ambaye alikuwa mpiga kura wa Kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Dimani,naye amepigiwa kura katika uchaguzi huu mdogo wa jimbo hili ambalo mimi ni Mgombea.Nnachotaka kufahamishwa Mheshimiwa Mkurugenzi ni sheria ipi ya Tume yako inayoruhusu Mfu kupigiwa kura?
Abdulrazak Khatib Ramadhan
Mgombea wa Uchaguzi, Jimbo la Dimani
Nakala:
Msimamizi wa Uchaguzi,
Katibu Mkuu CUF
Katibu CUF- Wilaya ya Magharibi ?B?