Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Kila siku tunawaambia siasa haziafnyiki mitandaoni, zinafanyika huko site coz hapa Tz sio U S A
 
katika Kata 22 zilizofanya uchaguzi mdogo Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata 21 huku chama cha demokrasia na maendeleo kikiambulia kata moja pekee mkoani Manyara katika kata ya Duru.
Pia Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi mnono katika Jimbo LA Dimani Zanzibar dhidi ya mgombea wa muungano wa ukawa.
 
Huwa yanajulikana mapema. Lakini chama cha siasa kushiriki Uchaguzi ni sehemu ya uenezi pia.
Uchaguzi unajulikana kuwa ni Chadema VS Dola (Polisi,DED, usalama nk) maana mshindani CCM ni kama vile hayupo au ana nguvu kama TLP tuu
Tehetehetehetehe. Sasa nafasi yenu wapinzani ipo wapi? Na je kule mnakoshinda ina maana hakuna hao uliowataja?
 
Umeongea point kubwa sana Mkuu.

Mkuu tatizo ni kuwa bado kuna watu wanajiita wapinzani kumbe ni mahawara wa Ccm kama Lipumba,Dovutwa nk. Vyama makini mfano utokee Uchaguzi mdogo tena hata vikisusia hao watasimama na kwa vile wapo kisheria basi mbele ya jumuia ya kimataifa utaitwa Uchaguzi wa vyama vingi.
Tujiulize, tuwafanye nini wasaliti hao?
 
katika Kata 22 zilizofanya uchaguzi mdogo Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata 21 huku chama cha demokrasia na maendeleo kikiambulia kata moja pekee mkoani Manyara katika kata ya Duru.
Pia Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi mnono katika Jimbo LA Dimani Zanzibar dhidi ya mgombea wa muungano wa ukawa.
acha uhuni, dimani hamjashinda, msema ukweli mpenzi wa Mungu, mneingiza kura fake
 
Huwa yanajulikana mapema. Lakini chama cha siasa kushiriki Uchaguzi ni sehemu ya uenezi pia.
Uchaguzi unajulikana kuwa ni Chadema VS Dola (Polisi,DED, usalama nk) maana mshindani CCM ni kama vile hayupo au ana nguvu kama TLP tuu

Basi muwe mnaacha Mbwembwe za kutangaza kushinda kabla ya kupiga kura au hayo ya DED na Usalama wa Taifa huwa mnayajua baada ya kura kuhesabiwa!
 
Chakaza Daudi Mchambuzi


Mpaka sasa kati ya kata 22 CCM wana kata 19
Chadema wao wanakata line za vodacom tu
Vyama vingi havikuja tuwe na ushabiki wa kama Yanga na Simba. Ila ni kuleta fikra kinzani chanya zitakazotufikisha mbali kijamii na kiuchumi. Jambo unalotakiwa kufurahia ni kuwa sera au fikra zako zitatekelezwa sio chama chako kimeshinda. Kwa kuwa hatuna Dira kama nchi hata uwepo wa vyama umekuwa ni deal za kujipatia maisha tu lakini si kufikisha maendeleo kwa wananchi. Pole Tanzania pole Africa tuna miaka mingi sana ya kuwa binadamu tutakaolewa nini maana ya
 
acha uhuni, dimani hamjashinda, msema ukweli mpenzi wa Mungu, mneingiza kura fake
Pole ndg mwanaMatombo kwa kupigwa kipigo kitakatifu.Hakika huko kwenu leo Matombo ni majonzi na giza lililo kuu!Tuliwaakumbusha lkn kwamba siasa si matamko na mbwembwe
 
DODOMA
*Halmashauri ya Mpwapwa*
Kata ya Ng'hambi
CCM 2,061
CDM. 707

*Manispaa ya Dodoma*
Kata ya Ihumwa
CCM. 2,447
CDM. 1,590
ACT. 38

MOROGORO
*Manispaa ya Morogoro*
Kata ya Kiwanja cha Ndege
CCM. 3,643
CDM. 1,932
CUF. 817
ACT. 72

IRINGA
*Halmashauri ya Mufindi*
Kata ya Igombavanu
CCM. 2,034
CDM. 361
ACT. 71
Kata ya Ikweha
CCM. 2,242
CDM. 631

ARUSHA
*Halmashauri ya Meru*
Kata Ngarenanyuki
CCM. 1,746
CDM. 1,556

_Halmashauri hii ina kata 26, CHADEMA ilishinda kata 25 na CCM ilishinda kata moja tu ambayo ndio hiyo inarudiwa uchaguzi_.

ARUSHA
*Halmashauri ya Arusha (Arumeru Magharibi)*
Kata ya Mateves
CCM. 2,045
CDM. 1,966
NCCR. 897

_Halmashauri hii ina kata 27, CHADEMA ilishinda kata 21 na CCM ilipata kata 6 mojawapo ndio hiyo inayorudia uchaguzi_.

DAR ES SALAAM
*Halmashauri ya Temeke*
Kata ya Kijichi
CCM. 7,647
CUF. 4,574
CDM. 3,433
ACT. 336
UDP. 193
D/MAKINI 107

SINGIDA
*Halmashauri ya Mkalama*
Kata Kinampundu
CCM. 1,944
CDM. 1,133

SHINYANGA
*Kahama Mji*
Kata ya Isagehe
CCM. 2,582
CDM. 367
ACT. 385

KATAVI
*Halmashauri ya Mpimwe*
Kata Kasansa
CCM. 1,494
CDM. 1,088

MWANZA
*Halmashauri ya Kwimba*
Kata ya Malta
CCM. 1,997
CUF. 1,725
CDM. 422
ACT. 305

*Halmashauri ya Sengerema*
Kata Kahumulo
CCM. 2,251
CDM. 245

RUVUMA
*Halmashauri ya Mbinga*
Kata ya Maguu
CCM. 3,783
CDM. 358

*Manispaa ya Songea*
Kata ya Tanga
CDM. 1,904
CCM. 1,739

KAGERA
*Halmashauri ya Muleba*
Kata ya Kimwani
CUF. 2,898
CCM. 2,882

_Diwani aliyeshinda kata hii aliuwawa kwa mapanga, watuhumiwa ni aliyekuwa mgombea udiwani wa CCM na Afisa Mtendaji kata_.

GEITA
*Geita Mji*
Kata ya Nkome
CCM. 5,443
CUF. 3,035
CDM. 333

KILIMANJARO
*Halmashauri ya Mwanga*
Kata ya Lembeni
CCM. 2,403
CDM. 1,080
NCCR. 87

MANYARA
*Halmashauri ya Babati*
Kata ya Duru
CDM. 1,953
CCM. 1,916

PWANI
*Kibaha Mji*
Kata Misugusugu
CCM. 1,545
CDM. 1,525
CUF. 55
ACT. 66
_Kata hii CHADEMA ilishinda, wakachakachua, tukaenda mahakamani, ikaamuriwa uchaguzi urudiwe_. *Matokeo Halisi yalikuwa:*
CDM 1525
CCM 1515
CUF 55
ACT. 66

_Katika uchaguzi huu mdogo, CHADEMA inatetea kata moja tu ya DURU Halmashauri ya BABATI. Kata zingine 19 zinazobaki zilikuwa chini ya CCM_
 
Ni dhahiri katika uchaguzi mdogo uliorudiwa leo, CHADEMA wamepigwa vibaya mno ndo maana hatujasikia kelele. Tunasubiri kusikia wakilalamika kuwa wameibiwa kura, sasa sijui wale walinzi wao wa kulinda kura wamegoma au?
kwa utawala huu wa awamu ya tano na tume hizi zilizo chini ya wakurugenzi makada wa ccm upinzani wasahau.
 
Matokeo Rasmi kata ya Isagehe-Kahama ni km ifuatavyo;
-NCCR-MAGEUZI-KURA=11
-CHAUMA-KURA=11
-C.U.F-KURA=30
-CHADEMA-KURA=439
-ACT-WAZALENDO-KURA=578
-C.C.M-KURA=1562.
Kura zilizoharibika ni -49.
 
Vyama vingi havikuja tuwe na ushabiki wa kama Yanga na Simba. Ila ni kuleta fikra kinzani chanya zitakazotufisha mbali kijamii na kiuchumi. Jambo unalotakiwa kufurahia ni kuwa sera au fikra zako zitatekelezwa sio chama chako kimeshinda. Kwa kuwa hatuna Dira kama nchi hata uwepo wa vyama umekuwa ni deal za kujipatia maisha tu lakini si kufikisha maendeleo kwa wananchi. Pole Tanzania pole Africa tuna miaka mingi sana ya kuwa binadamu tutakaolewa nini maana ya

Pole wewe pekeyako
Mimi ni binadamu
Baki na unyama wako
 
Bado kuna binadamu mwenye akili timamu anapanga foleni kuipigia kura ccm,!!! maajabu haya
 
Back
Top Bottom