Mkuu;
Mimi nimetoa fikra yangu na sikulazimishi kuikubali au kuikataa.
Ni kweli wanaChadema na wana ''Cuf original'' hawawezi kuchonganishwa na mada isiyochonganisha!
Kama ningekuwa na akili ndogo, basi wewe mwenye akili kubwa wala usingepoteza muda wako kuweka komenti kwenye mada ya mtu mwenye akili ndogo labda kama hujitambui.
Mimi nadhani wanaotia huruma ni wale wanazungusha mikono huku wakiimba Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko bila kufahamu kilicho nyuma ya Lowassa.
Kuhusu strong speech. Ndio maana tunasema Lowassa anaisarambatisha CHADEMA! Yaani hakuweza kutoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu ili ashinde Urais halafu baada ya kushindwa uchaguzi ndiyo anaanza kutoa strong speech ili muendelee kumuamini zaidi.