Jaji ameingia Mahakamani Muda huu
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali
Jenitreza Kitali
Abdallah Chavula
Pius Hilla
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi
Jeremiah Mtobesya
John Malya
Seleman Matauka
Wakili wa Serikali Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji nasisi tupo tayari Kupokea Malekezo
Jaji Jana nilihairisha Shauri Jana Jioni, Nikasema Nitasoma Uamuzi leo.
Lakini Kutokana kwa Wingi wa Hoja naomba Muda zaidi Mpaka Kesho
Nikakamilishe Kuandika Uamuzi
Naomba Radhi kwa Hairisho hili ambalo hatukulitarajia
Mawakili wa pande zote mbili Wanasimama Kukubaliana
Jaji kama nilivyosema kwamba nahairisha Shauri Mpaka Kesho, Upande wa Mashitaka Mtamleta Shahidi atakaa Kizimbani Na ataendelea Kutoa Ushahidi
Nahairisha Mpaka Kesho Saa 3 Asubuhi
Jamani[emoji23][emoji23][emoji23]
Huyu siyo jaji, Sasa anawaambia wamlete shahidi kesho aje kuendelea kutoa ushahidi wa Nini Sasa ,huku hujatoa rulling (hukumu/maamuzi/maelekezo) halafu unaahirisha mpaka kesho ili iweje Sasa???? Aiseeeeee Hakuna kitu hapo ,,,,ni upumbavu tu, hatuna haki taifa hili, unaahirisha mpaka kesho ,ko ni pingamizi gumu lakini utalitupilia ,Jaji Tiganga ni Kama ndugai tu Hakuna kitu hapo.