Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 17, 2021: Kesi yaahirishwa mpaka tarehe 18/11/2021 saa tatu asubuhi

Hii kesi ina vichekesho sana, Yaani nyaraka ilikataliwa kupokelewa mahakamani kutoka kwa shahidi A halafu shahidi B analeta tena nyarak ile ile na kuomba ipokelewe.

Hapa kuna kesi kweli au ndio kusogeza muda mbele? Tunaanza kupoteza muda kuongelea kitu mjadala wake ulishafungwa.

Yaani shaghala baghala tu
 
Upande wa utetezi

 
Mm nilidhan Shahid kanyofolewa mbona Bado anaendelea kutoa ushahid kama kweli Sheria inafata mkondo wake?
 
Kwa kesi inayoendelea, inaonekana wazi Jaji anapwaya kwa kiasi kikubwa. Mawakili inaonekana uwezo wao kishetia upo juu maradufu ya uwezo wa Jaji.

Matokeo yake, ni kila mara Jaji kuahirisha kesi ili aende akasome. Hakuna hoja, hata ndogo kiasi gani, anayoweza kuisikiliza na kuitolea uamuzi hapó hapo.

Hatari iliyopo, kwa mwenendo huu wa kesi, na weledi walio nao mawakili Vs weledi wa jaji, jaji kila mara atafanya kazi ya kuahirisha kesi, na kuifanya kesi ishindwe kumalizika.

Kwa namna inavyoenda, kama Jaji atabakia huyu huyu, inaweza kuchukua hata zaidi ya miaka mitatu kesi hii kumalizika, tena kukiwa na makosa mengi ya kiweledi yatakayokuwa yamefanywa na Jaji.
 
Alipataje ujaji kilakitu hakijui anyway tusibirie nataman mbowe atamke neno wabadilishiwe jaji
 
wamegwaya baada ya kuona kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa mboe alikuwa anaratibu mipango ya kigaidi.
Ushahidi wa taratibu za kipolisi ni sawa upo

Ushahidi wa mbowe kulipua vituo vya mafuta uko wapi !??

Ushahidi wa mbowe kukata magogo ya miti uko wapi!?

Je mahakama inaweza toa hukumu kwa Mambo ambayo hayajatokea!?

Je wewe una akili sawa sawa!? Uthibitishie umma huu![emoji15]
 
Hii inaweza kukupa uhalisia jinsi ambavyo kuna upinzani mkubwa sana kwenye kesi hii pengine haijawahi kutokea. Mawakili wa Utetezi wako makini sana katika kila neno atamkalo Shahidi lakini mawakili wa serikali wao wanachofanya ni kutafuta upenyo kwa kutumia sheria kushindisha kesi kitu ambacho kimekuwa kigumu sana kwao.

Mawakili wa Utetezi wako makini Sani sana kuhakikisha kua wanashinda kesi hii au kuonyesha madhaifu yake, hawa wa Jamhuri wanalipwa mishahara na posho za umma ndiyo maana kuna wakati ni kama hawajali hivi. Wanadai wanafanya uzalendo kwa nchi lakini uzalendo wenye kutoka nje ya misingi ya kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…