Salaam Wakuu,
Leo tarehe 24/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.
Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
Kujua kesi ilipoishia soma: Yaliyojiri kesi ya Mbowe 24/01/2022: Shahidi wa 11, H4347 Goodluck amaliza ushahidi wake. Shahidi wa 12 kuendelea tarehe 26/01/2022
UPDATES
- Jaji ameingia Mahakamani
- Kesi inatajwa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili Wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na wakili
- Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Tulimanywa Majige
- Ignasi Mwinuka
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
- Nashon Nkungu
- John Mallya
- Dickson Matata
- Maria Mushi
- Khadija Aron
- Seleman Matauka
- Idd Msawanga
- Michael Lugina
- Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja Wakili Peter
Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea.
Jaji: Anakuwa Shahidi namba Ngapi?
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Anakuwa Shahidi namba 12 Shahidi anakwenda kuitwa Shahidi anaingia Mahakamani, Mrefu Mwembamba, Mweupe Kidogo
Jaji: Majina yako
Shahidi: Naitwa Luteni Denis Urio
Jaji: Umri
Shahidi: Miaka 42
Jaji: Kabila
Shahidi: Mchaga
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkristo
Jaji: Kazi yako
Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi Tanzania.
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama, kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, kweli tupu, Mungu Nisaidie Wakili wa Serikali.
Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ataongozwa na Wakili Abdallah Chavula
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula anqsimama na Kwenda Kwa Shahidi
Wakili wa Serikali: Shahidi nitakuwa nakuuliza Maswali, Ukijibu utakuwa unamjibu Mheshimiwa Jaji, Naomba Uongee kwa Sauti Ya Juu
Shahidi: Sawa
Wakili wa Serikali: Tukumbushe Majina yako
Shahidi: Naitwa Luteni Denis Leo Urio
Wakili wa Serikali: Mkazi wa Wapi?
Shahidi: Mkazi wa Ngerengere Morogoro
Wakili wa Serikali: Unafanya Shughuli gani
Shahidi: Ni Mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania
Wakili wa Serikali: Kituo Chako Cha Kazi ni wapi
Shahidi: Ni Ngerengere Morogoro
Wakili wa Serikali: Kituo Chako Kinafahamika kwa Jina gani?
Shahidi: 92 KJ Ngerengere
Wakili wa Serikali: Cheo Chako ni Kipi
Shahidi: Luteni wa Jeshi
Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni Yapi
Shahidi: Ni Platoon Commander Kuongoza Askari Walio Chini yangu
Wakili wa Serikali: Unaongoza Askari Wangapi
Shahidi: Afisa Mmoja na Askari 30
Wakili wa Serikali: Ni Askari gani wanayofanya kazi Katika Kikosi cha KJ 92
Shahidi: Ni Wanajeshi Waliopata Mafunzo Maalum, Komando
Wakili wa Serikali: tuambie Wewe Umetumikia Jeshi Kwa Miaka Mingapi
Shahidi: Miaka 18
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ulijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania Mwaka gani
Shahidi: Tarehe 16,June 2003
Wakili wa Serikali: Jeshi la Wananchi Tanzania lina Majukumu yepi
Shahidi: Lina Majukumu ya Ulinzi wa Mipaka dhidi ya Uvamizi Wa Ndani na Nje
Wakili wa Serikali: Jukumu lingine ni lipi
Shahidi: Kwenye Operation ya Ulinzi Wa Amani Kwenye Mataifa yenye Mgogoro
Wakili wa Serikali: Umesema Wewe ni Luteni wa Jeshi, Je Umekuwa Kwenye Nafasi hiyo kwa Miaka Mingapi
Shahidi: Kwa Miaka 6
Wakili wa Serikali: Umeeleza Mahakama Kwamba Miongoni Mwa Majukumu ya Jeshi ni Kuleta Amani Kwenye Mataifa Mengine, Ushiriki wako ni Vipi
Shahidi: Nimeshirriki Kulinda Amani 2011 Nchini Sudani, Na 2019 ni Sudan hiyo hiyo Jimbo la Darfur
Wakili wa Serikali: Tueleze Mahakama Kule Darfur ulipo enda Majukumu yako yalikuwa yepi
Shahidi: Kuhakikisha Wale Staff Officer (Wapatanishi) Ku Ensure Usalama wao Kwa Sababu Wao ni Unarmed Personnel
Wakili wa Serikali: Kuna Mtu anafahamika Kwa Jina la Khalfani Bwire Unamfahamu Vipi
Shahidi: Nina Mfahamu Kwa Muda Mrefu, Nili Mtrain, Nikifanya naye Kazi Kituo Kimoja cha 92 KJ
Wakili wa Serikali: Umemfahamu Kuanzia Mwaka gani
Shahidi: Kuanzia 2006 Mpaka 2009
Wakili wa Serikali: Wakati Unamfahamu, yeye alikuwa ana Jukumu gani
Shahidi: alikuwa Kiongozi Mdogo, anaongoza,Ni Section Commander, alikuwa anaongoza Watu 9
Wakili wa Serikali: Cheo Chake Kilikuwa ni Kipi
Shahidi: Rank ya koplo
Wakili wa Serikali: Unaposema Ulifahamiana naye kuanzia 2006 Mpaka 2009 umamaam gani
Shahidi: Ukomo wake Ulikuwa Mwaka 2019
Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mpaka I kafika Ukomo wake
Shahidi: alifukuzwa Kazi Jeshini
Wakili wa Serikali: Kwa sababu Zipi afukuzwe Kazi
Shahidi: Kwa Utovu wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Wakati Mwaka 2019 anafukuzwa + kazi Wewe Ulikuwa wapi
Shahidi: Kwenye Operation Ya Peace Keeping, Sudan Jimbo la Darfur
Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Khalfani Bwire alifukuzwa Kazi kwa Utovu wa Nidhamu
Shahidi: Ni 2020 Mwezi March Baada ya Kutoka Darfur
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ni Mazingira Yapi Ulifahamu Kwa Yeye Kufukuzwa Kazi Jeshini
Shahidi: Nilipata Taarifa hizo kutoka Kwa Administration Officer of the Unit
Wakili wa Serikali: Administration Officer ndiyo nani?
Shahidi: Mtu anaye fuatilia Maisha ya Askari Wote Kikosini na Maafisa ya Jeshi, Pia ni Kiongozi
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu na Khalfani Bwire tangu 2006 Mpaka 2019 yalikuwaje
Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri tu, Ya Kiongozi na afisa wake.
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu baada ya Ajira Kukoma yalikuwaje
Shahidi: Bado nilikuwa naendelea Kuwasiliana naye, Mawasiliano ya Kawaida tu
Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu anaitwa Adam Hassan Kasekwa ama Jina Lingine anaitwa Adamoo.
Shahidi: Nafahamiana naye toka Mwaka 2012 ndipo alipofika Kwenye Unit ya 92KJ alifika Kwenye Mafunzo, Nikam' train, aka' pass Maana nilimpokea Mimi.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama, Huyu Adam Kasekwa ama Adamoo alifanya kazi Jeshini Kwenye 92 KJ alifanya kazi Mpaka Lini
Shahidi: Mpaka Mwaka 2018
Wakili wa Serikali: Nini Kilimsibu Mwaka huo 2018
Shahidi: Alifukuzwa Kazi Jeshini.
Wakili wa Serikali: Alifukuzwa Kazi Jeshini Kwa Sababu zipi
Shahidi: Kwa Utovu Wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Mpaka anafukuzwa Kazi Jeshini Kwa Utovu, Je alikuwa na Cheo gani
Shahidi: alikuwa Private Soldier.
Wakili wa Serikali: Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini
Shahidi: Ni Askari ambaye hana Rank inayo kuwa Displayed, Ni Askari anayekuwa Chini ya Kiongozi Wake
Wakili wa Serikali: Wakati Adam Kasekwa anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa upo wapi
Shahidi: Nilikuwa Nipo Arusha.
Wakili wa Serikali: Ni wakati Gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Adam Kasekwa kafukuzwa Kazi Jeshini
Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi Kutoka Arusha Kwenye Kozi
Wakili wa Serikali: Taarifa za Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu Wewe Ulizipata Wapi?
Shahidi: Administration Officer
Wakili wa Serikali: alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira gani
Shahidi: Ofisini Kwake
Wakili wa Serikali: Mazingira ya Mahusiano Baina ya Wewe na Adam Kasekwa yalikuwa Je Kipindi Kile Kabla ajafukuzwa Jeshi.
Shahidi: Yalikuwa Mazuri tu
Wakili wa Serikali: VIpi Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi na Kuondoka Jeshini yalikuwaje
S
hahidi: Yalikuwa Mazuri
Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu Naitwa Mohammed Abdilah Ling'wenya Unamfahamu Vipi
Shahidi: Namfahamu Nilifanya naye Kazi Kituo Kimoja
Wakili wa Serikali: Kituo Gani hicho
Shahidi: 92 KJ
Wakili wa Serikali: umeanza Kufanya naye Kazi huyo Mohammed Ling'wenya kuanzia Mwaka gani Mpka Mwaka gani
Shahidi: Kuanzia Mwaka 2010 Mpaka Mwaka 2017
Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mwaka 2017
Shahidi: alifukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mpaka anafukuzwa Kazi, alikuwa ana Cheo gani Katika Jeshi
Shahidi: Alikuwa ni Private Soldier
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini
Shahidi: Ni Askari Mwenye Cheo Cha Mwisho chini
Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Mahusiano yenu
Shahidi: Tulikuwa na Mahusiano Mazuri
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu, Mahusiano yenu yalikuwaje
Shahidi: Yaliendelea Kuwa Kama alipokuwa Kazini
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama wakati Mohammed Ling'wenya anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa Wapi
Shahidi: Nilikuwa Kwenye Kazi Maalum
Wakili wa Serikali: Ni Wakati Gani Ulikuja Kupata Ufahamu, kuwa Mohammed Ling'wenya amefukuzwa kazi
Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi, kutoka kwa Administration Officer
Wakili wa Serikali: Huyo Administration Officer alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira Yepi
Shahidi: Tukiwa Ofisini
Wakili wa Serikali: Unasema Unamfahamu Khalfani Bwire Je akiwa Miongoni Mwetu unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Sababu ipi itakufanya Umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 10, lakini pia Body Morphology
Wakili wa Serikali: Mtu huyo Yupo wapi
Shahidi: aliyepo Mbele yangu, Tunatizamana, Yupo Jirani na Magereza
Wakili wa Serikali: Pia Umemtaja Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo, Je Unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Ni sababu Zipi hasa zitafanya Umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5 lakini pia na Body Morphology Yake
Wakili wa Serikali: Hebu tuonyeshe Mtu huyo Yupo wapi
Shahidi: Ni Wapili Kutoka Kulia Mwa Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: tuambie Mwingine unaye Msema ni Mohammed Abdilah Ling'wenya, na Yeye Vipi Unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Sababu Ipi Itakufanya umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5, pia Body Morphology yake, Tatu ana Makovu Usoni na Mkononi.
Wakili wa Serikali: Hapa Yupo wapi
Shahidi: Ni watatu Kutoka Upande Wa Kulia wa Bwire
Wakili wa Serikali: Shahidi isaidie Mahakama, Unasema Adam Kasekwa Na Mohamed Ling'wenya Walikuwa ni Private Soldier, Je pale Jeshini Walikuwa na Majukumu Yapi
Shahidi: Wao Ni watendaji wa Shughuli za Kijeshi
Wakili wa Serikali: Huyu Khalfani Hassan Bwire, Adam Hassan Kasekwa, Mohammed Abdilah Ling'wenya wakati wa Utumishi wao Wa Jeshi Pale 92 KJ Makazi yao yalikuwa wapi?
Shahidi: Walikuwa Wa naishi huko, Khalfani Bwire Ngerengere, Adam Kasekwa alikuwa Anaishi Chalinze katika Utaratibu Wa Misbehave
Wakili wa Serikali: Hapana Usiende Huko
Shahidi: Na Mohamed Ling'wenya na Yeye Chalinze