Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes, msingi wa kesi hii ya UGAID upo hapa - wacha tuone kama kaja na jipya. Wale wa Rau madukani hamna kitu... huyu ndye mastermind wa mchongo mzima! Ngoja tumsikilize kama atakuwa na jipya.
Tagia hapo hi kesi imesha kua ngumu kwa jamhuri........inaendelea ili mradi kufunika aibuHuyo wa Leo ni shahidi muhimu kuliko wote, kama hataeleza vitu vikivyonyooka kesi itakuwa ngumu sana kwa jamhuri
[emoji38][emoji38][emoji38]Yes, msingi wa kesi hii ya UGAID upo hapa - wacha tuone kama kaja na jipya. Wale wa Rau madukani hamna kitu
Huyu ameletwa mahakamani kwa vitisho , hana ushahidi wa maanaHuyo wa Leo ni shahidi muhimu kuliko wote, kama hataeleza vitu vikivyonyooka kesi itakuwa ngumu sana kwa jamhuri
Kesi ilisha isha juzi kwa goodluck sasa ni kukamilisha ratibaHuyo wa Leo ni shahidi muhimu kuliko wote, kama hataeleza vitu vikivyonyooka kesi itakuwa ngumu sana kwa jamhuri
OH SERIKALI HAINA MASHAIDI WALA USHAHIDISalaam Wakuu,
Leo tarehe 24/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.
Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
Kujua kesi ilipoishia soma: Yaliyojiri kesi ya Mbowe 24/01/2022: Shahidi wa 11, H4347 Goodluck amaliza ushahidi wake. Shahidi wa 12 kuendelea tarehe 26/01/2022
UPDATES
- Jaji ameingia Mahakamani
- Kesi inatajwa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili Wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na wakili
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
- Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Tulimanywa Majige
- Ignasi Mwinuka
- Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
- Nashon Nkungu
- John Mallya
- Dickson Matata
- Maria Mushi
- Khadija Aron
- Seleman Matauka
- Idd Msawanga
- Michael Lugina
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja Wakili Peter
Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea.
Jaji: Anakuwa Shahidi namba Ngapi?
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Anakuwa Shahidi namba 12 Shahidi anakwenda kuitwa Shahidi anaingia Mahakamani, Mrefu Mwembamba, Mweupe Kidogo
Jaji: Majina yako
Shahidi: Naitwa Luteni Denis Urio
Jaji: Umri
Shahidi: Miaka 42
Jaji: Kabila
Shahidi: Mchaga
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkristo
Jaji: Kazi yako
Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi Tanzania.
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama, kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, kweli tupu, Mungu Nisaidie Wakili wa Serikali.
Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ataongozwa na Wakili Abdallah Chavula
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula anqsimama na Kwenda Kwa ShahidiWakili wa Serikali: Shahidi nitakuwa nakuuliza Maswali, Ukijibu utakuwa unamjibu Mheshimiwa Jaji, Naomba Uongee kwa Sauti Ya Juu
Shahidi: Sawa
Wakili wa Serikali: Tukumbushe Majina yako
Shahidi: Naitwa Luteni Denis Leo Urio
Wakili wa Serikali: Mkazi wa Wapi?
Shahidi: Mkazi wa Ngerengere Morogoro
Wakili wa Serikali: Unafanya Shughuli gani
Shahidi: Ni Mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania
Wakili wa Serikali: Kituo Chako Cha Kazi ni wapi
Shahidi: Ni Ngerengere Morogoro
Wakili wa Serikali: Kituo Chako Kinafahamika kwa Jina gani?
Shahidi: 92 KJ Ngerengere
Wakili wa Serikali: Cheo Chako ni Kipi
Shahidi: Luteni wa Jeshi
Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni Yapi
Shahidi: Ni Platoon Commander Kuongoza Askari Walio Chini yangu
Wakili wa Serikali: Unaongoza Askari Wangapi
Shahidi: Afisa Mmoja na Askari 30
Wakili wa Serikali: Ni Askari gani wanayofanya kazi Katika Kikosi cha KJ 92
Shahidi: Ni Wanajeshi Waliopata Mafunzo Maalum, Komando
Wakili wa Serikali: tuambie Wewe Umetumikia Jeshi Kwa Miaka Mingapi
Shahidi: Miaka 18
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ulijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania Mwaka gani
Shahidi: Tarehe 16,June 2003
Wakili wa Serikali: Jeshi la Wananchi Tanzania lina Majukumu yepi
Shahidi: Lina Majukumu ya Ulinzi wa Mipaka dhidi ya Uvamizi Wa Ndani na Nje
Wakili wa Serikali: Jukumu lingine ni lipi
Shahidi: Kwenye Operation ya Ulinzi Wa Amani Kwenye Mataifa yenye Mgogoro
Wakili wa Serikali: Umesema Wewe ni Luteni wa Jeshi, Je Umekuwa Kwenye Nafasi hiyo kwa Miaka Mingapi
Shahidi: Kwa Miaka 6
Wakili wa Serikali: Umeeleza Mahakama Kwamba Miongoni Mwa Majukumu ya Jeshi ni Kuleta Amani Kwenye Mataifa Mengine, Ushiriki wako ni Vipi
Shahidi: Nimeshirriki Kulinda Amani 2011 Nchini Sudani, Na 2019 ni Sudan hiyo hiyo Jimbo la Darfur
Wakili wa Serikali: Tueleze Mahakama Kule Darfur ulipo enda Majukumu yako yalikuwa yepi
Shahidi: Kuhakikisha Wale Staff Officer (Wapatanishi) Ku Ensure Usalama wao Kwa Sababu Wao ni Unarmed Personnel
Wakili wa Serikali: Kuna Mtu anafahamika Kwa Jina la Khalfani Bwire Unamfahamu Vipi
Shahidi: Nina Mfahamu Kwa Muda Mrefu, Nili Mtrain, Nikifanya naye Kazi Kituo Kimoja cha 92 KJ
Wakili wa Serikali: Umemfahamu Kuanzia Mwaka gani
Shahidi: Kuanzia 2006 Mpaka 2009
Wakili wa Serikali: Wakati Unamfahamu, yeye alikuwa ana Jukumu gani
Shahidi: alikuwa Kiongozi Mdogo, anaongoza,Ni Section Commander, alikuwa anaongoza Watu 9
Wakili wa Serikali: Cheo Chake Kilikuwa ni Kipi
Shahidi: Rank ya koplo
Wakili wa Serikali: Unaposema Ulifahamiana naye kuanzia 2006 Mpaka 2009 umamaam gani
Shahidi: Ukomo wake Ulikuwa Mwaka 2019
Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mpaka I kafika Ukomo wake
Shahidi: alifukuzwa Kazi Jeshini
Wakili wa Serikali: Kwa sababu Zipi afukuzwe Kazi
Shahidi: Kwa Utovu wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Wakati Mwaka 2019 anafukuzwa + kazi Wewe Ulikuwa wapi
Shahidi: Kwenye Operation Ya Peace Keeping, Sudan Jimbo la Darfur
Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Khalfani Bwire alifukuzwa Kazi kwa Utovu wa Nidhamu
Shahidi: Ni 2020 Mwezi March Baada ya Kutoka Darfur
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ni Mazingira Yapi Ulifahamu Kwa Yeye Kufukuzwa Kazi Jeshini
Shahidi: Nilipata Taarifa hizo kutoka Kwa Administration Officer of the Unit
Wakili wa Serikali: Administration Officer ndiyo nani?
Shahidi: Mtu anaye fuatilia Maisha ya Askari Wote Kikosini na Maafisa ya Jeshi, Pia ni Kiongozi
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu na Khalfani Bwire tangu 2006 Mpaka 2019 yalikuwaje
Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri tu, Ya Kiongozi na afisa wake.
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu baada ya Ajira Kukoma yalikuwaje
Shahidi: Bado nilikuwa naendelea Kuwasiliana naye, Mawasiliano ya Kawaida tu
Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu anaitwa Adam Hassan Kasekwa ama Jina Lingine anaitwa Adamoo.
Shahidi: Nafahamiana naye toka Mwaka 2012 ndipo alipofika Kwenye Unit ya 92KJ alifika Kwenye Mafunzo, Nikam' train, aka' pass Maana nilimpokea Mimi.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama, Huyu Adam Kasekwa ama Adamoo alifanya kazi Jeshini Kwenye 92 KJ alifanya kazi Mpaka Lini
Shahidi: Mpaka Mwaka 2018
Wakili wa Serikali: Nini Kilimsibu Mwaka huo 2018
Shahidi: Alifukuzwa Kazi Jeshini.
Wakili wa Serikali: Alifukuzwa Kazi Jeshini Kwa Sababu zipi
Shahidi: Kwa Utovu Wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Mpaka anafukuzwa Kazi Jeshini Kwa Utovu, Je alikuwa na Cheo gani
Shahidi: alikuwa Private Soldier.
Wakili wa Serikali: Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini
Shahidi: Ni Askari ambaye hana Rank inayo kuwa Displayed, Ni Askari anayekuwa Chini ya Kiongozi Wake
Wakili wa Serikali: Wakati Adam Kasekwa anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa upo wapi
Shahidi: Nilikuwa Nipo Arusha.
Wakili wa Serikali: Ni wakati Gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Adam Kasekwa kafukuzwa Kazi Jeshini
Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi Kutoka Arusha Kwenye Kozi
Wakili wa Serikali: Taarifa za Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu Wewe Ulizipata Wapi?
Shahidi: Administration Officer
Wakili wa Serikali: alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira gani
Shahidi: Ofisini Kwake
Wakili wa Serikali: Mazingira ya Mahusiano Baina ya Wewe na Adam Kasekwa yalikuwa Je Kipindi Kile Kabla ajafukuzwa Jeshi.
Shahidi: Yalikuwa Mazuri tu
Wakili wa Serikali: VIpi Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi na Kuondoka Jeshini yalikuwaje
Shahidi: Yalikuwa Mazuri
Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu Naitwa Mohammed Abdilah Ling'wenya Unamfahamu Vipi
Shahidi: Namfahamu Nilifanya naye Kazi Kituo Kimoja
Wakili wa Serikali: Kituo Gani hicho
Shahidi: 92 KJ
Wakili wa Serikali: umeanza Kufanya naye Kazi huyo Mohammed Ling'wenya kuanzia Mwaka gani Mpka Mwaka gani
Shahidi: Kuanzia Mwaka 2010 Mpaka Mwaka 2017
Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mwaka 2017
Shahidi: alifukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mpaka anafukuzwa Kazi, alikuwa ana Cheo gani Katika Jeshi
Shahidi: Alikuwa ni Private Soldier
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini
Shahidi: Ni Askari Mwenye Cheo Cha Mwisho chini
Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Mahusiano yenu
Shahidi: Tulikuwa na Mahusiano Mazuri
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu, Mahusiano yenu yalikuwaje
Shahidi: Yaliendelea Kuwa Kama alipokuwa Kazini
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama wakati Mohammed Ling'wenya anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa Wapi
Shahidi: Nilikuwa Kwenye Kazi Maalum
Wakili wa Serikali: Ni Wakati Gani Ulikuja Kupata Ufahamu, kuwa Mohammed Ling'wenya amefukuzwa kazi
Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi, kutoka kwa Administration Officer
Wakili wa Serikali: Huyo Administration Officer alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira Yepi
Shahidi: Tukiwa Ofisini
Wakili wa Serikali: Unasema Unamfahamu Khalfani Bwire Je akiwa Miongoni Mwetu unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Sababu ipi itakufanya Umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 10, lakini pia Body Morphology
Wakili wa Serikali: Mtu huyo Yupo wapi
Shahidi: aliyepo Mbele yangu, Tunatizamana, Yupo Jirani na Magereza
Wakili wa Serikali: Pia Umemtaja Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo, Je Unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Ni sababu Zipi hasa zitafanya Umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5 lakini pia na Body Morphology Yake
Wakili wa Serikali: Hebu tuonyeshe Mtu huyo Yupo wapi
Shahidi: Ni Wapili Kutoka Kulia Mwa Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: tuambie Mwingine unaye Msema ni Mohammed Abdilah Ling'wenya, na Yeye Vipi Unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Sababu Ipi Itakufanya umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5, pia Body Morphology yake, Tatu ana Makovu Usoni na Mkononi.
Wakili wa Serikali: Hapa Yupo wapi
Shahidi: Ni watatu Kutoka Upande Wa Kulia wa Bwire
Wakili wa Serikali: Shahidi isaidie Mahakama, Unasema Adam Kasekwa Na Mohamed Ling'wenya Walikuwa ni Private Soldier, Je pale Jeshini Walikuwa na Majukumu Yapi
Shahidi: Wao Ni watendaji wa Shughuli za Kijeshi
Wakili wa Serikali: Huyu Khalfani Hassan Bwire, Adam Hassan Kasekwa, Mohammed Abdilah Ling'wenya wakati wa Utumishi wao Wa Jeshi Pale 92 KJ Makazi yao yalikuwa wapi?
Shahidi: Walikuwa Wa naishi huko, Khalfani Bwire Ngerengere, Adam Kasekwa alikuwa Anaishi Chalinze katika Utaratibu Wa Misbehave
Wakili wa Serikali: Hapana Usiende Huko
Shahidi: Na Mohamed Ling'wenya na Yeye Chalinze
Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Mwaka 2011 ulikuwa Darfur, Je katika Wenye Cheo Cha Private Soldier nani Uliyekuwa naye
Shahidi: Sikumbuki
Wakili wa Serikali: Unaposema Ukumbuki unamaanisha nini
Shahidi: Sina Kumbukumbu Ka Nilikuwa na Mmoja wapo.
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama pale Darfur Ulipokuwa Unaishi Kwenye ile Nyumba yako Ulikuwa Unaishi na Nani
Shahidi: Tulikuwa tunaishi Viongozi Watupu
Wakili wa Serikali: Na Mwaka 2012 pale Darfur Pia Mwenye Cheo Cha Private, nani ulikuwa naye
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili wa Serikali: Mtu anaitwa Freeman Mbowe Wewe Unahusiana naye Vipi
Shahidi: Tulifahamiana naye Mwaka 2008 Mpaka 2020
Wakili wa Serikali: Unaweza Kusema ni Mazingira Gani yaliyopelekea Nyinyi Kufahamiana.
Shahidi: Mwaka 2008 Freeman Mbowe anilipigia Simu akaniita Kwa Majina yangu
Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi
Shahidi: Siwezi Kukumbuka hiyo Tarehe
Wakili wa Serikali: Shahidi Irejee Mahakama tena, Unasema alikupigia Simu lini
Shahidi: Mwaka 2008
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi na Mwezi gani
Shahidi: Sikumbuki Tarehe Wala Mwezi
Wakili wa Serikali: alikupigia Simu, wewe si yako ilikuwa ya Namba gani
Shahidi: ilikuwa 0754612518
Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka na Yeye namba yake iliyokupogoa ilikuwa namba gani
Shahidi: Ilikuwa Mtandao Wa Airtel, ila namba Sikumbuki
Wakili wa Serikali: alikueleza nini
Shahidi: alipiga Simu akauliza Wewe ni Denis Urio, Nikamwambia Yes ndiyo Mimi, akasema ni Askari wa Jeshi la Wananchi, Nikamwambia Ndiyo, akajitambulisha, Kwa Sababu Namfahamu Nikamuamkia.
Wakili wa Serikali: Kwa Sababu Unamfahamu Ukamuamkia, Ulikuwa Unamfahamu Vipi
Shahidi: Alikuwa anaonekana Kwenye Vyombo Vya Habari, Haikuwa Jina geni, I Amana anafahamika
Wakili wa Serikali: Baada ya wewe Kumpa Salamu nini Ulifanya
Shahidi: alikuwa ana confirm Profile Yangu.
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini
Shahidi: alikuwa nauliza wewe si Denis Urio Nikasema Ndiyo, ni Mtu wa Kilimanjaro basi Mimi Ndugu yako, Ndipo Uhusiano Ulianza
Wakili wa Serikali: Hebu Iambie Mahakama Namba yako ya Simu alitoa Wapi
Shahidi: Sifahamu alipoitoa.
Wakili wa Serikali: Yeye alikueleza, Ni wapi ametoa Namba yako
Shahidi: aliniambia Kuwa Mbona Unafahamu, Kwa Mtu Kupata Namba ya Simu Siyo Tatizo, Usiwe na Wasiwasi
Wakili wa Serikali: Ni Kitu gani kilipelekea Mpaka Yeye Kusema Kuwa Mbona Unafahamika Sana.
Shahidi: Ni pale Nilipo taka Kujua amepata wapi Namba Yangu
Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Sasa Hayo Maneno ni Wakati gani alikutamkia
Shahidi: Mara ile ya Kwanza Kuwasiliana, Nikiwa natumia Mtandao Wa Voda yeye akitumia Mtandao Wa Airtel.
Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie Baada ya Siku hiyo kuwasiliana Mawasiliano yenu yalikuwaje
Shahidi: Tulikuwa tunaendelea Kuwasiliana, Iwe Kwa Kunisalimia alikuwa ananitumia Ujumbe wa Kuni wish hata Kama Kuna Sikukuu au Event Yoyote
Wakili wa Serikali: Mlimkuta ana kwa ana Lini
Shahidi: Tukikutana Ana Kwa Ana Mwaka 2012
Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Mwaka huo 2012 Ilikuwa ni Tarehe Ngapi na Mwezi Gani
Shahidi: Siwezi Kukumbuka Tarehe Wala Mwezi
Wakili wa Serikali: Shahidi nikirudishe Nyuma, Umeeleza Awali Kwamba 2011 ulikuwa Darfur Nchi Sudan, Je Ulirejea Nchi Mwaka Gani
Shahidi: Nili rejea Mwaka 2011 Mwezi wa 10
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Tarehe Ngapi
Shahidi: Siwezi Kukumbuka Siku wala Tarehe.
Wakili wa Serikali: Ni Mazingira Yepi Yalipelekea Ninyi Mwaka 2012 Kukutana
Shahidi: Mwaka 2012 nikiwa Maeneo Ya Mgulani (Saba Saba) Nilipokea Simu ya Mheshimiwa Mbowe Kama Ilivyo Kawaida yake akaniambia Upo wapi, Nikamwambia Nipo Maeneo Ya Mgulani (sabasaba).
Wakili wa Serikali: alikueleza nini
Shahidi: Alini uliza nipo Wapi, Nikamuelekeza Location nilipo
Wakili wa Serikali: Location Maana yake ni nini
Shahidi: Eneo nilipo
Wakili wa Serikali: Endelea
Shahidi: aliniambia Kuwa Kuna Kitu anataka Tuongee, Je tunaweza Kuonana? Nikamuuliza Wewe Upo wapi akasema Yupo Mikocheni Cassa Motel
Jaji: Unaweza Kutaja Spelling zake
Shahidi: CASA Sikumbuki Vizuri
Wakili wa Serikali: Wewe Ukamwambia Nini
Shahidi: Sijui Mikocheni Vizuri, Wala Mahala Ilipo
Wakili wa Serikali: Ulifanya Nini sasa
Shahidi: Baada ya kumwambia Siyo Mwenyeji aliambiwa niende Kituo Cha Tax Ni Mwambie Dereva Yoyote yule anipeleke CASA Motel
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupewa hayo Maelekezo, Maamuzi yako yalikuwa ni nini
Shahidi: Nilienda Kwa Dereva Tax, Nikamwambia Anipeleke CASA Motel, nikaweza Kufika CASA Motel
Wakili wa Serikali: Hicho Kituo Cha Tax Ulicho enda Kutafuta Tax ni Kituo Cha Wapi
Shahidi: Ni Saba Saba Mbele Kidogo Kama Unaenda Kwa Aziz Ally Wilaya Ya Temeke.
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Hiyo Safari yako ya CASA hotel Ilikuwaje
Shahidi: Nili weza Kufika, Nikampigia Simu akapokea, akauliza nimefika Wapi, Nikamwambia Nimeshafika
Wakili wa Serikali: Taratibu Jaji anaandika..
Wakili wa Serikali: endeleaaaa
Shahidi: akanielkeza Pale CASA Motel Kuna Vitu Kama Vimepangwa Kuna watu walikuwa wamekaa Mbali Mbali Ka Wanne hivi, Baada ya Kufika akaniuliza huyu anadai TSh ngapi Nikamwambia TSh 20
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumwambia Ikawaje
Shahidi: Alilipa hiyo Tsh 20.
Wakili wa Serikali: Wakati yoye Haya Unayosema Kuanzia Kupigana Simu Mpaka Unafika CASA Hotel Ilikuwa ni Majira yapi
Shahidi: Ilikuwa Kuanzia Saa Saba Mchana Mpaka Alasiri
Wakili wa Serikali: Pale Mlipoliwa Mmekaa na Kukutana naye, Mwingine nani Mliye kuwa Mmekaa naye
Shahidi: Hapakuwa na Mtu Mwingine zaidi yangu Mimi na Yeye
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa, Nini Mlichozungumza Wakati Mmekutana
Shahidi: Mambo Makubwa matatu, Kutaka Kujua Mimi ni Nani, nafanya kazi gani, Nina Cheo gani?
Wakili wa Serikali: Kwenye Hayo Madodoso wewe Ulimjibu nini
Shahidi: Mimi ni +Rank gami Majibu niliyompa, Nilimwambia Mimi Sina Rank
Wakili wa Serikali: Ulipomueleza Wewe huna Rank Ulikuwa Unamanisha Nini
Shahidi: Nilimwambia Mimi Sina Cheo Chochote.
Wakili wa Serikali: Kwanini Ulimueleza hayo
Shahidi: Kwa sababu aliniuliza Swali
Wakili wa Serikali: Lingine lipi ulilomjibu
Shahidi: Nilimjibu nafanya kazi Mkoani Morogoro, na Nyumbani ni wapi nilimwambia Mimi Nyumbani ni Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Vijijini.
Wakili wa Serikali: Kingine Kipi
Shahidi: Akitaka Kujua Msimamo Wangu dhidi ya Vyama Vya Upinzani
Wakili wa Serikali: Kwenye hilo la Msimamo Wako Majibu yako Yalikuwa ni Yepi
Shahidi: Nilimwambia Kwa Mujibu wa Kazi yangu Siruhusiwi Kufungamana na Chama Chochote
Nyie pigeni porojo tu ila Mbowe anafungwa tena kwa ushahidi usio na mashakaKwenye hii kesi shahidi anaandaliwa kama anaenda kufanya NECTA wakati hujui Kibatala atatoa maswali kwenye topic ya Geometry? Algebra? hujui akiomba kielelezo namba fulani swali linalofuata shahidi anachanganyikiwa kwamba atumie calculator au four figure table, shahidi akienda kwenye desa/kibuti anatoa majibu ya swali la kwanza kumbe aliulizwa swali la tatu........
Labda Kaongeze wewe ushahidi lakini sio wa hawa kina urioNyie pigeni porojo tu ila Mbowe anafungwa tena kwa ushahidi usio na mashaka
Watu wenye akili za aina yako mi uwa nasema pumbu si mzigo kwasababu ni lakoOH SERIKALI HAINA MASHAIDI WALA USHAHIDI
OH SERIKALI HAINA MASHAIDI WALA USHAHIDI
Kama kafika kizimbani na katoa ushahidi- waya ndo umekatikia hivyo- Mbowe anachungulia jela kutokea mahabusuUrio ndo anajua kila kitu anaweza kuchomoa waya ndo itakuwa mwisho wa kesi
fix tupu, loohWakili wa Serikali: Lingine lipi mililozungumza
Shahidi: Alini uliza Juu ya Makampuni ambayo yangeweza Kufunga Mfumo Wa Mawasiliano Kwenye Ofisi zao, na Kama Jeshini Kuna Makampuni yaliyofunga Mawasiliano Jeshini. Nilipo Muuliza Kwanini anataka Kufanya kazi na Makampuni Yaliyofunga Mawasiliano Jeshini, Akajibu Kuwa anataka Kufuatilia Mawasiliano ya Viongozi Wenzie Wanaotoa Siri Nje ya Chama.
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Baada ya Kuku uliza Juu ya Swala hilo, Majibu yako Yalikuwa ni nini
Shahidi: Nilimshauri aende Kwenye Taasisi za Elimu ya Juu ndiyo atapata Suluhu ya Tatizo lake Wakili wa Serikali Nini Kiliendelea Sasa Baada ya Hapo.