Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

ushaihidi wa mchongo...eti makampuni yaliyofunga mawasiliano jeshini Mbowe anayatafuta - useless.
Mbona hutaki kulijibu swali rahisi? Kati yako na Luteni, tumwamini nani? And why?
 
Kila wakati komando anafukuzwa kambini kwa utovu wa nidhamu, kiongozi wao Denis Urio hayupo kituoni….. akirudi anapewa taarifa tu.

Strange..!!
Makomandoo hawafukuzwi kazi. Tambua hilo. Akifukuzwa au hilo likitokea, ni straight kifungoni. Hao wengine unaodhani walifukuzwa, walitumwa huko mtaani, tactically, ili kutimiza malengo.

Read between the alphabetical letters!
 
1643189813428.png
 
Ipo. Hapa siti ya mbele
Kwani nawe mchaga

Shahidi: Kitu cha Kwanza tulisalimiana Salamu za Muda Mrefu, Lakini Baada ya Salamu hizo akaniambia komredi mwaka huu wa 2020 Kuna Uchaguzi Mkuu, Hivyo Chama Changu Kimepanga Kuchukua Dola Kwa namna na Kwa Gharama Yoyote ile. Akaniambia Wewe si Unaona Watu wa wanyonge wa hali ya Chini wanavyoishi Maisha ya Shida Akanielekeza, komredi Tumefahamiana Muda Mrefu, Tunatoka Mkoa Mmoja, pia wewe ni Mchaga Mwenzangu, Tukichukua Dola Unafikiri Wewe Utakosa Cheo Cha Juu Jeshini?

Akaniambia hivyo Jeshini Kuna Watu Waliostaafu au Kufukuzwa Kazi ya Jeshi.. Wale ambao wamefanya Mafunzo Maalum ya Komandoo. Homeboy naomba unitafutie Vijana hao wenye Mafunzo Maalum ya Komando, ambao nitaambatana nao kwenye Harakati za Kuchukua Dola. Najua Watakuwa na Uwezo wa Kunisaidia Kufanya Nchi isitawalike, Kuleta Taharuki na Kusiwe na Amani.. Tutafanya hayo Kwa Kuzua Taharuki Mheshimiwa Freeman Mbowe Alisema yalikuwa ni Kulipua Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Moto Masoko na Mikusanyiko Mkubwa Ya watu.

Kukata Miti Mikubwa iliyoota pembezoni Mwa Barabara zote, Hasa Kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro hasa Mjinwa Moshi na Barabara Kuu ya Morogoro - Iringa, Kwa Kufanya Vitendo hivyo Vitatu Kutapelekea watu Kuwa na Taharuki na Kuandamana Nchi Nzima.

Mikoa Mingine Iliyobakia Itasapoti Mikoa hii niliyo highlight.. Point Nyingine ya Mwisho ni Kuwadhuru Viongozi Wengine Wa Serikali, Ni Viongozi ambao ni Vikwazo Kwa Vyama Vya Upinzani.. Hivyo Homeboy nisaidie Kuwapata hao watu Nina Haraka nao sana, MWISHO WA MAELEZO YAKE FREEMAN.
 
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Tuambie, Ieleze Mahakama Alikueleza au Kukwambia Kitu gani alichokuitia

Shahidi: Kitu cha Kwanza tulisalimiana Salamu za Muda Mrefu, Lakini Baada ya Salamu hizo akaniambia komredi mwaka huu wa 2020 Kuna Uchaguzi Mkuu, Hivyo Chama Changu Kimepanga Kuchukua Dola Kwa namna na Kwa Gharama Yoyote ile...

Seriously, Mbowe?
 
Mbona hutaki kulijibu swali rahisi? Kati yako na Luteni, tumwamini nani? And why?
Kwa hiyo mahakama inaweza kuamini hizo porojo za huyo Luteni Urio!

Yaani kirahisi tu, tulikutana CASA Motel pale Mikocheni, akaniuliza kuhusu mifumo ya mawasiliano, na bla bla nyingine!! Halafu tuamini!

Aweke mezani ushahidi usiotia shaka, badala ya huo ushahidi wa nadharia! na muendelezo ule ule wa porojo za Rau Madukani! Sijui kukata magogo, kuzua taharuki!!
 
Kwa hiyo mahakama inaweza kuamini hizo porojo za huyo Luteni Urio!

Yaani kirahisi tu, tulikutana CASA Motel pale Mikocheni, akaniuliza kuhusu mifumo ya mawasiliano, na bla bla nyingine!! Halafu tuamini!

Aweke mezani ushahidi usiotia shaka, badala ya huo ushahidi wa nadharia. Na siyo muendelezo ule ule wa porojo za Rau Madukani!
It's over! Jambo hilo ni zito sana!
 
Kwa hiyo mahakama inaweza kuamini hizo porojo za huyo Luteni Urio!

Yaani kirahisi tu, tulikutana CASA Motel pale Mikocheni, akaniuliza kuhusu mifumo ya mawasiliano, na bla bla nyingine!! Halafu tuamini!

Aweke mezani ushahidi usiotia shaka, badala ya huo ushahidi wa nadharia. Na siyo muendelezo ule ule wa porojo za Rau Madukani!
Ndiyo mwendo wenyewe mkuu- ushahidi usio na mashaka ndio huo
 
Back
Top Bottom