Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Unategemea unaenda kulinda nini?.
angalia malengo ha mbowe ambayo yameainishwa.
mtu wa kwanza kumchoma mbowe ni Nani ?
Kama sio LUTENI urio aliyepanga naye mipango?
Kuna ukweli ambao hamtaki kuukubali je mbowe alimtuma kamanda urio kumtafuta vijana?
Kwa ajili ya kazi gani?

Narudia tena, matamanio yako ndio unayageuza ukweli, kwasababu kwenye haya maelezo ya leo huenda ndio roho yenu ya ushahidi ilipo. Hapa inaonekana imeshaandika na pointi kabisa kibindoni maana ule ujinga wote wa serikali unategemea maelezo haya ya huyu muhuni wa leo.
 
Hilo la ulinzi amelisema Luteni Urio. Halafu hakuishia hapo. Amesema pia kwamba harakati ilikuwa UGAIDI. Umemsikia? Sasa kama unakubali hilo la kuwa walinzi binafsi (bodyguards), kubali pia na hili la pili la terrorism.

Otherwise, reject the whole thing. Hapo nitakuona shujaa & muungwana sana!
Wakati Urio anasema kuhusu Ugaid haja connect na wale vijana ni maelezo yake kua wale vijana aliwatafutia kazi ya Ulinzi na wao baada ya kufika walimwambia tumeajirwa na tutalipwa kwa mwez

Hawa watu walipelekwa kama mapandikiz manake walipewa kazi ya kutoa report kama wataona ana suspicious activity

Kwakua akili zako n sifuri ww huon kwamba vijana wametoka kwenye hii case rasmi
 
Unategemea unaenda kulinda nini?.
angalia malengo ha mbowe ambayo yameainishwa.
mtu wa kwanza kumchoma mbowe ni Nani ?
Kama sio LUTENI urio aliyepanga naye mipango?
Kuna ukweli ambao hamtaki kuukubali je mbowe alimtuma kamanda urio kumtafuta vijana?
Kwa ajili ya kazi gani?
Mjingamimi! Naishia hapa
 
1.) Mwanajeshi amepata taarifa nzito asipeleke kwa mkuu wake jeshini apeleka polisi? Analichafua jeshi kwakuwaingiza wenzie kwenyekesi za ugaidi nabado yukokazini?
DCI unajua kazi na mipaka yake?

2.) Nini kilichomfanya Free amuamini na kumfungukia ishu kubwa kiasi hicho? Kwanini asimwambie tuu amtafutie walinzi alafu akishawapata angewapa hizo kazi nyingine! Free anaakili na amesalitiwa maranyinhi asingemwamini MTU kijinga hivyo.
Lazima alimwamini kwa mambo mengi aliyotaja Luteni Urio. Ndiyo maana amepewa nickname ya ^HOMEBOY^ Unajua maana yake?

3.) Unamtafutia MTU magaidi kisha husemi wewe ulidai/ulilipwa kiasi gani? Mara yapili tena unatumwa bila posho? Nonsense!!
Natamani kusikia akiulizwa hili kesho. Katika huo udalali yeye amelipwa kiasi gani? But, tayari tumeshajua kwamba aliahidiwa ^cheo cha juu.^ That's good enough to begin with!

4.) Kesi nzito ya Free wanaemchukia, polisi wasichomeke mtuwao akaajiriwe naFree wapate info? Wakwambie homeboy endelea tuu kutafuta watuwako?
Because nadhani waliona si salama sana kuwaweka officials wao wa usalama karibu na mtu mwenye nia husika za ugaidi alizozianisha Luteni Urio.

Pili, pengine kwa FM kudai kwamba nitafutie watu wastaafu na waliofukuzwa jeshi, labda tayari alikuwa na majina. Alichotaka tu jinsi ya kuwafikia--kukonekti nao.

5.) Polisi washindwe kumrekodi mbowe akipanga hayo mavitu na haowajeda kweli?
6.) Polisi lazima wangekutana na kina Adamoo wawaseti ili ushahidi uwe wawazi wasiteseke mahakamani kamahivi.
Who knows? Labda ndicho kimesaidia hadi leo hii aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai yuko hai hadi leo. Labda bila hivyo (ushirikiano na mawasiliano ya karibu), angeshaliwa kichwa na wahuni.

7.) Urio aangaliwe alikosa kazini wakati katiwa ndani aeleze kwanini alikosa kazi na aliswekwa ndani?

Shahidi: Sijui 🙂
8.) Polisi walijua mapeeema sabaya anapangiwa shambulizi walieleza walinzi wake? Walimwambia OCD wa hai?
Shahidi: Sijui 🙂
9.) Kwanini polisi walitoka AR kwenda operation KLM wasiyoijua vyema? KLM hakuna wapelelezi?

Shahidi: Sijui :"
10.) Kwahiyo Free ndiye alifahamika mapeeeema Siku yakwanza kwa kupanga uhalifu,nikwavipi alichelewa kukamatwa wakakamatwa kina Adamue et all?
Non sense hiikitu, inasikitisha taasisi kuuubwa kutumia kodizetu kuendesha kesimichongo kamahii... Na CAG tunamlipa remunerations nyiiingi anakaa anatizama hii aibu akiamini atashinda kesi!! Kweliiii!!!
Matukio huwa yanatend kufunguka kadiri muda unavyokwenda! Time always tells the whole truth!
 
Sasa uhuni wa urio ni upi?
Kumtafutia mbowe vijana?
Au kumchoma mbowe?
Mbona tangu mwanzo wa hii kesi nilisema mbowe alibugi kufanya mipango na watu wa jeshi.
Shida mnaendeshwa na ushabiki wa vyama.
hao watu Wana viapo.
Narudia tena, matamanio yako ndio unayageuza ukweli, kwasababu kwenye haya maelezo ya leo huenda ndio roho yenu ya ushahidi ilipo. Hapa inaonekana imeshaandika na pointi kabisa kibindoni maana ule ujinga wote wa serikali unategemea maelezo haya ya huyu muhuni wa leo.
 
Unategemea unaenda kulinda nini?.
angalia malengo ha mbowe ambayo yameainishwa.
mtu wa kwanza kumchoma mbowe ni Nani ?
Kama sio LUTENI urio aliyepanga naye mipango?
Kuna ukweli ambao hamtaki kuukubali je mbowe alimtuma kamanda urio kumtafuta vijana?
Kwa ajili ya kazi gani?
Nadhani sasa huna budi kulibadili jina lako ili lisiendelee tena kuwa mjingamimi . At least uitwe mjinga mwerevu .

Au, pengine, wewe ni saa mbovu inayosema ukweli kwa nasibu japo mara mbili kwa siku?
 
Na kabla hawajaleta tahaluki tena mwanzo wao wa kazi wanakamatwa kwanini?
Yaani huyu Urio ndio amekuja kuunguza mkanda wote wa movie ya Kina Kingai

Kama yeye aliambiwa atafute vijana wa Kuleta taharuki na yeye hakukubaliana kwanini wasingepeleka 'watu wao' ambao wangekuwa wanajua nini kinaendelea ili iwe rahisi kuwasiliana nao na kupata taarifa ya kila hatua badala yake anawapeleka kina Lijenje tena kwa kuwadanganya wanaenda kumlinda halafu hapohapo unataka uwapigie simu kila dakika kwamba mnafanya nini au mmepewa kazi gani? Huu si upunguani?

Halafu kabla hawajafanya chochote mnawakamata.

Kama hizi ndio akili za walinzi wa nchi yetu tuna hasara tupu.
 
ishia hapo hapo.
Ila huo ndo ukweli.
Unatafuta nini na wanajeshi Kama sio kukuchoma?
najua hauwezi kuyajua haya Mambo uenda bado mtoto mdogo.
Nikuulize swali dogo kwanini mtu wa kwanza kumchoma mbowe ni kamanda urio?
Mjingamimi! Naishia hapa
 
Hapana. Kesi yoyote ya jinai ni lazima kuwe na ushahidi mzito "to prove beyond reasonable doubt"

Kwa maana mtuhumiwa hawezi kuhukumiwa kwa hisia ama porojo pekee.

Katika uwanja wa sheria inatamkwa kwamba ni bora kuwaachia huru watu 100 kuliko kumhukumu kifungo mtu mmoja asiye na hatia.
Sheria inaambatana na haki, isipokuwa haki huwa ipo ndani ya sheria, ili kuipata haki unahitaji sheria kuithibitisha haki, kwa hyo kinachotokea Sasa Ni kuiambia sheria itoe haki kwa kuangalia vielelezo vilivyopo, na hapo ndpo wakili anapoingia, kumtetea mteja wake, mwisho tutajua tu Ni wakili yupi ameweza kuitafsr sheria ili haki ionekane??
Stay tuned..
 
Hapana Mimi uwa nasimamia ninachokiamini.
PIA HATUJUANI.
Tupo humu tunacheka,tunarumbana lakini HATUJUANI fani zetu.
Kikubwa tuheshimiane.
Nadhani sasa huna budi kulibadili jina lako ili lisiendelee tena kuwa mjingamimi . At least uitwe mjinga mwerevu .

Au, pengine, wewe ni saa mbovu inayosema ukweli kwa nasibu japo mara mbili kwa siku?
 
Mbowe alimtafuta Lt. Urio kwa sababu zipi??

Hayo anayafahamu mwenyewe kwa kina ndani ya Moyo wake.
 
Kwa kawaida unapowatafuta magaidi, huwezi kuwaambia tunaenda kuua wala kufanya vurugu. Unawaambia tunaenda kuikomboa nchi. Kwenye neno ^kuikomboa^ hapo ndimo yamejificha yote hayo.

Likewise, usikute yeye alipewa kazi (na FM) ya kwenda kuwatafuta na kuwaunganisha kwake. How? ^Just waambie tu kwamba wanakuja kwangu kunipatia ulinzi binafsi. Mambo mengine yote hayo mimi nitayamaliza mwenyewe!^
Hapana mkuu! Huu ushahidi ni ngumu kumesa!😄

Halafu anasema baada tu ya kumtafutia Mbowe watu wa kwenda kufanya uhalifu, Mbowe akawa hapokei tena simu zake.

Yani mtu ambaye umemwambia siri zako, na akakutafutia watu wa kwenda kufanya uhalifu, umkaushie halafu uendelee na mipango hiyo ya kihalifu, as if hatofahamu na kwenda kutoa taarifa?

Maana huo u “homeboy” Mbowe aliachana nao baada ya kumwambia siri zake za kufanya uhalifu na baada ya kumtafutia wanajeshi wa kufanya uhalifu? Gimme a break dog 😄

Hii kesi imepangwa kizembe mnoo! “Loopholes everywhere”, subiri mawakili wa utetezi watakavyomkaanga na mafuta yake yeye mwenyewe!

Kwanza ni upuuzi wa hali ya juu kuwatoa kina Khalfan Bwire na wenzake kwenye shughuli zao halali za kujipatia kipato na kuwadanganya kuwa wanaenda kuwa walinzi wa Mbowe.

Halafu huo ujira wa kumdhuru Sabaya ni upi? Huyu shahidi ni “the most supid son of a bitch I’ve ever heard from to be honest”
 
Urio amezua maswali mengi zaidi ya majibu.

Je Moses Linjenje ataonekana au kufaamika mahali alipo?

Je Urio alitoa pesa yake kufadhili ugaidi?

Je Urio ataweza kuonesha vithibitisho vya makutano na Mbowe?

Je .....
Kesi ndo inaanza Sasa.
 
Wakati Urio anasema kuhusu Ugaid haja connect na wale vijana ni maelezo yake kua wale vijana aliwatafutia kazi ya Ulinzi na wao baada ya kufika walimwambia tumeajirwa na tutalipwa kwa mwe...
Imagine kwenda kuwa mlinzi wa mtu anayesemekana ana viashiria vya ugaidi! Better yet, Luteni Urio aliambiwa na ^walinzi^ hao kwamba kazi yao imebadilika kutoka kuwa ya ulinzi, na sasa ni ya kwenda kumla mtu kichwa huko Moshi.

Umeona?

Sasa tuchukulie kwamba walidanganywa. Kwa nini wasingemwambia Boss wao kwamba kazi waliyofanyiwa interview na kuitiwa siyo hiyo? Au, kwa sababu ya usalama wao wenyewe, wazuge tu kana kwamba wameridhia kwenda kuitekeleza mishe husika (tactical appreciation), kisha wakasepa zao? Na hapa tunawazungumzia MAKOMANDOO, si watoto fulani wa darasa la nne!

Ina maana involvement yao huioni? Huoni wakienda kutenda uhalifu kwa hiari yao wenyewe?

Leo hii, nikimwomba rafiki yangu twende matembezini (but at the back of my mind niko na malevolence or should I say ^femalevolence,^ halafu along the way nikamshirikisha tumkabe roba hasimu wangu (Mola aepushie mbali!), then rafiki yangu huyo hana haki kabisa mbele ya vyombo vya sheria kujitetea kwamba sikuwa nimemwambia tunaenda kumtoa mtu roho. Do you understand?
 
Bora wewe kidogo umekuwa muelewa.ila makamanda wao hawataki kuelewa.
Mimi tangu mwanzo nilisema mbowe kujenga mipango na hao watu wa jeshi lilikuwa ni kosa Ila wafuasi wake walinipinga humu .
Watu wa majeshi sio.
Sasa Yule aliyepanga nae mipango ndo kaenda kumchoma.
Tuna mlaumu kingai na wenzake kumbe mchawi alikuwa nae
Wewe Mjingawewe Acha kulazimisha dhamira yako Ndiyo iwe sheria.

Sheria gani inawazuia wanajeshi waliostaafu/kufukuzwa wasitafute kazi nyingine yoyote iliyo halali?

Hiyo kazi unayotaka kutulazimisha iliyokukwa ifanyike kwa Mbowe ni ipi tofauti na kazi ambayo watuhumiwa wenyewe wameisema lakini hata huyo Urio mwenyewe kaithibitisha kuwa walienda kumlinda Mbowe.

Hayo ya kupanga ugaidi hadi sasa anabaki nayo Urio kama "story tu" hadi hapo atakapoyathibitisha au kuthibitishwa na viambata vya ushahidi vilivyo halali kisheria.
 
Kingai alichemka... Urio alisema kuwa 500K alipokea ili jamaa wakafanye uhalifu... Je, kuna sehemu mashahidi waashtaka kuanzia Kingai wameonesha ualifu uliofanywa na watuhumiwa...
500K ili wakafanye uhalifu? Na wakati aliwaambia ni kwenda kumlinda Freeman?

Unawakabidhi watu pesa unawaambia ni za kwenda kwenye kazi ya ulinzi. Halafu mahakamani unasema uliwakabidhi wakafanye uhalifu. Aliwaambia hao washitakiwa pesa hizo ni za kwenda kufanya uhalifu?! Kesi gani hii?!

Suala la uhalifu ni mchongo wao na kina Kingai. If anything, hawakutaka Freeman apate ulinzi maana ndiyo hao waliotaka kumuuwa Lissu, waliomteka Ben Saanane na kumpoteza, na pia waliomshambulia Mbowe wakamvunja mguu.
 
Yaani huyu Urio ndio amekuja kuunguza mkanda wote wa movie ya Kina Kingai

Kama yeye aliambiwa atafute vijana wa Kuleta taharuki na yeye hakukubaliana kwanini wasingepeleka 'watu wao' ambao wangekuwa wanajua nini kinaendelea ili iwe rahisi kuwasiliana nao na kupata taarifa...
Yaani acha tu
 
Back
Top Bottom