Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake. Tumaini Swila amaliza ushahidi. Mawikili wa Serikali wafunga Ushahidi. Jaji kutoa uamuzi 18/02/2022

Nilitegemea na DCI Boaz naye atatinga ndani ya nyumba pamoja na Mzee Sirro ili kupambana na mawakili wasomi wa upande wa utetezi! Sasa ndiyo basi tena! ☹️

All in all, Jaji angeifutilia mbali tu hii kesi. Maana haina kichwa wala miguu. Watuhumiwa nao wakifungua kesi ya kudai fidia, kwa unyanyasaji walio fanyiwa na polisi! itakuwa poa sana.
 

Yaani ukiajiriwa na mwenyekiti wa CHADEMA taifa, polisi inaona ni kosa kubwa utatungiwa lolote la kufikirika
 
upande wa serikali wameona wasiwasumbue wasitaafu wale kiinuamigongo yao vyema wasije kudhalilika mahakamani sa hii kwa kuombaomba kila mara kwenda toilet
 
Kibatala: Nikisema huenda baada ya Mwaka Mmoja pia Mtaona hana Hatia nitakuwa nawaonea. Je Luteni Denis Urio alishawahi Kuwaambia Kuhusu Gabriel Muhina na Khalid

Shahidi: Hapana

Mambo moto sana, shahidi wa upande wa Jamhuri ana wakati mgumu kutetea kesi waliyoiunda kwa mikono yao wenyewe.
 
 
Si tulikubaliana tuna mashahidi 23 jamani, mfanye kuwaleta wengine hata wawili basi, au ndo mmegundua nn kwani mbona wote wanao ushahidi mzuri jamani ninyi Jamhuri mbona hvyo lkn?

Jamhuri imeghairi ? ina maana upande wa Jamhuri hauoni tena umuhimu wa mashahidi wengine kumi upande wa Jamhuri kuletwa mahakamani ili watoe ushahidi usio na shaka ili haki itendeke ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…