Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Katika Mapokezi na Mkutano Mkubwa wa hadhara wa Tundu Lissu Mjini Bukoba

CHADEMA walikuwa na Gazeti la Tanzania Daima lingesaidia sana kutufikishia habari za Uchaguzi lakini siku hizi halionekani, kuna Tv binafsi nyingi sana nchini lakini zote zinaonyesha matangazo toka TBC tu. Tatizo ni Awamu ya Tano iliyoingia madarakani kwa makosa ilitumia kila mbinu haramu kuendeleza makosa badala ya kurekabisha yasirudiwe tena matokeo yake hata hayo matangazo ya TBC wengi hatuangalii tena. Uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu sana lakini kwa sababu ya Serikali kuminya uhuru wa vyombo habari na wanahabari, kampeni za mwaka huu zimepoa sana utadhani siyo Uchaguzi Mkuu. Hii inatia wasiwasi huenda watu wengi wasijitokeze kupiga kura na kuruhusu figisufigisu kuingiza viongozi wabovu madarakani.
 
Kina Mayala wanjifanya hawayajui haya
 
Nadhani mambo yakienda sawa itakuwa kesho
Jitahidini sana mfike, huko pia kuna kura nyingi sana tu. Jiwe alishatutenga na anafanya makusudi kulipa kisasi kwa kunyimwa ubunge mara zote alizogombea pale.

Halafu ile si ngome ya chama chochote, anayewekwa akizingua anachezea kichapo. Hivyo kwakuwa jiwe na mbunge wake wamezingua nafasi ipo wazi
 
Tanzania Daima Jiwe alilifungia Mwaka mzima
 
Nashangaa kwa nini hajadekiwa barabara kama ilivyokuwa kwa Lowassa!

Uzuri wa siasa za upinzani Tanzania, wagombea Urais huingia kwenye uchaguzi kwa mbwebwe na baada ya uchaguzi huanza kupotea polepole!

Tanzania kuna vituko!
Najua mnamlaumu sana aliyekosea shabaha. Hii mikikimikiki anayoleta Lisu isingekuwepo....Ulikuwa Devil advocate wa kudai Upinzani umekufa...sasa chupi zinawabana..
 
Kiasili, Magufuli siyo mwanademokrasia. Analazimishwa tu. Ingekuwa ni matakwa yake, angefuta achaguzi, na yeye kujitangaza kuwa ni Rais, na yeyote ambaye angehoji apelekewe askari wenye silaha.

Hivyo tusitegemee maendeleo ya demokrasia wala maendeleo ya watu, kama Magufuli ataendelea kuwa Rais.

Mifano mingi ipo inayothibitisha hulka ya Rais Magufuli. Hata akiamua kukudhalilisha, hataki hata ujitetee, yeye akuseme, akusimange, akutukane, hata kama ni kwa kukuonea, wewe unyamaze tu kimya au uitikie, 'sawa mheshimiwa Rais'. Viongozi wa namna hiyo ni hatari sana kwa Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua mnamlaumu sana aliyekosea shabaha. Hii mikikimikiki anayoleta Lisu isingekuwepo....Ulikuwa Devil advocate wa kudai Upinzani umekufa...sasa chupi zinawabana..
Na kweli namshangaa hata haoni aibu kuja kuchangia hapa wakati ana maandiko yake mengi hapa ya kutabiri kifo Cha Upinzani

Hata huyo Pascal Mayalla alikuwa anajiapiza hapa kwamba Mbowe kaua Chadema
 
Lissu anakamilisha ratiba huko kanda ya ziwa hana chake, mdomo wake umemponza. Anachukia meli,treni,daraja la busisi nk. kwa kifupi ngoja akatembee na uwepo wake unawaponza wagombea ubunge na udiwani kupitia chadema.
Ahahahahaaaaa jamaa yenu akirudi kwao nyie mtaolewa mjini hapa,anzeni kutafuta vibarua mapema
 
This ia terrible.....ni haki Jpm alielie kweli. Eti tunachakata za 2014😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…