Mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuingia kwa kishindo kikubwa mjini Bukoba.
Mji wa Bukoba ambao ni ngome Kuu ya Chadema unatarajiwa kuzizima Leo wakati shujaa huyo atakapokanyaga viunga vya mji huo.
Mgombea Ubunge wa Bukoba Mjini mwenye ushawishi mkubwa Chief Kalumuna amewaalika wananchi wote wa Bukoba kumlaki na kumsindikiza kwa maandamano makubwa mgombea huyo wa Urais atakapowasili Hadi katika viwanja vya Gymkhana.
Wachunguzi wa siasa za Bukoba wanasema huenda Leo mji wa Bukoba ukavunja Rekodi ya Mapokezi iliyowekwa na miji ya Tunduma, Mbeya na Mwanza.
Mpaka Sasa kila dalili zinaonyesha mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ana Uhakika wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 60%
Kabla ya kuingia Bukoba Mjini Lissu atahutubia mikutano katika miji ya Karagwe na Misenyi
Yaliyojiri
Kama ilivyotarajiwa Lissu amewasili Bukoba Mjini majors ya saa 10 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa watu waliojipanga majiani huku msafara ikiongozwa na bodaboda zaidi ya Mia tano.
Akihutubia halaiki hiyo ya watu Lissu kwa maneno yake mwenyewe amesema kwa Sasa Bukoba ndiyo inayoshikilia Rekodi ya Mapokezi.
Pamoja na mambo mengine kwa Mara nyingine Lissu amelaani vikali sheria Kandamizi ya Mafao ya wastaafu inayozuia Fao la Kujitoa na kupunguza Mafao ya Wafanyakazi maskini wanapostaafu.
Lissu amesema ole wao Wafanyakazi wakiichagua CCM kwani Sheria hii iliyojaa hila na uovu ilaanza kutumiia mwakani.
Lissu ameahidi Wafanyakazi kufutilia mbali sheria hii isiyojali Haki za watu endapo wananchi wakimchagua kuwa Rais wao.
View attachment 1576775
View attachment 1577480
View attachment 1577481
View attachment 1577482
View attachment 1577499
View attachment 1577500
View attachment 1577501
View attachment 1577502