Mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu yupo Mkoani Geita akiendeleza kampeni zake za kuingia Ikulu.
Lissu aliyewasili mkoani Geita hapo Jana na kupata mapokezi yaliyovunja Rekodi ya Tanzania katika mji wa Katoro Jimbo la Busanda.
Mkoa wa Geita ni nyumbani kwa mgombea wa CCM John Magufuli Lakini shauku ya wananchi kumuunga mkono mgombea wa Chadema inakitia hofu kubwa chama tawala Cha CCM.
Lissu aliwasili usiku mjini Geita na kulakiwa na halaiki kubwa ya watu wanaokadiriwa kufikia elfu 10
Umati wa huo wa watu ulimsindikiza mpaka Hotelini alikofikia na ulikesha nje ya Hoteli hiyo kwa kile walichodhani wanamlinda Rais wao.
Mapokezi ya Lissu Geita ni salaam tosha kwa chama tawala na mgombea wake kwamba Zama zao zinaelekea ukingoni
Molemo Media itawaletea yatakayojiri katika mkutano wa Hadhara mjini Geita
Video ya kwanza chini inaonyesha mapokezi yake ya Jana alipotua kwa Mara ya kwanza mkoani Geita Jimbo la Busanda.
Yaliyojiri Jioni Hii
Kama ilivyotarajiwa Lissu amewasili kwa kishindo kikubwa mjini Geita.Umati wa watu uliomlaki umesababisha achelewe kuingia viwanjani.
Akimwaga sera kwa wananchi mkombozi huyo wa Tanzania ameendelea kuhubiri sera yake ya Uhuru Haki Na Maendeleo ya Watu.
Lissu ameendelea kulaani ukandamizaji dhidi ya Wafanyakazi wa Tanzania ikiwemo kutokuongezewa mishahara kwa miaka mitano na kupitishwa kwa sheria Haramu dhidi ya Mafao ya Wafanyakazi kwa kuondoa Fao la Kujitoa na kupunguza Mafao ya wastaafu.Lissu amesema akiingia madarakani uonevu huo utakuwa umefikia mwisho.