Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Katika Mapokezi ya Tundu Lissu na Mkutano Mkubwa wa Hadhara Geita Mjini

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Katika Mapokezi ya Tundu Lissu na Mkutano Mkubwa wa Hadhara Geita Mjini

Media
20200924_073048.jpg
 
Molemo bana!

Hujachoka tu kuandika thread kama hizi kuanzia mwaka 2010.

Nakumbuka wakati wa kampeni mwaka 2010 ulivyokuwa unaleta thread kuhusu Dk. Slaa.

Mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu pia ukaleta tena thread kama hizi!

Mwaka huu hujachoka pia lakini tatizo lako kila ukileta thread kama hizi mgombea wako hupigwa chini!

Jiandae na mwaka huu kama ilivyotokea miaka ya nyuma!
 
Hongera sana lissu, fafanua vizuri kauli mbiu ya haki, Uhuru na maendeleo ya watu.tumia lugha ya kawaida ya kueleweka kwa umma kama haki ya dhamana polis, haki ya kufanya kazi na kuongezewa mshahara
 
Mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu yupo Mkoani Geita akiendeleza kampeni zake za kuingia Ikulu.

Lissu aliyewasili mkoani Geita hapo Jana na kupata mapokezi yaliyovunja Rekodi ya Tanzania katika mji wa Katoro Jimbo la Busanda.

Mkoa wa Geita ni nyumbani kwa mgombea wa CCM John Magufuli Lakini shauku ya wananchi kumuunga mkono mgombea wa Chadema inakitia hofu kubwa chama tawala Cha CCM.

Lissu aliwasili usiku mjini Geita na kulakiwa na halaiki kubwa ya watu wanaokadiriwa kufikia elfu 10

Umati wa huo wa watu ulimsindikiza mpaka Hotelini alikofikia na ulikesha nje ya Hoteli hiyo kwa kile walichodhani wanamlinda Rais wao.

Mapokezi ya Lissu Geita ni salaam tosha kwa chama tawala na mgombea wake kwamba Zama zao zinaelekea ukingoni

Molemo Media itawaletea yatakayojiri katika mkutano wa Hadhara mjini Geita

Video ya kwanza chini inaonyesha mapokezi yake ya Jana alipotua kwa Mara ya kwanza mkoani Geita Jimbo la Busanda.
Tunamuomba Rais mtarajiwa kutembelea vijiji vya Nyamikoma,kamwanga na lwenge viko kms 5 tu kutoka geita mjini, hakuna huduma ya maji Safi na salama,hakuna umeme,hakuna barabara,hakuna shule,hakuna zahanati. Magufuli tumemuomba muda mrefu hataki na Hajawahi kufika huku tangu azaliwe. Katoro hakuna maji kabisaaaaaaa
 
Back
Top Bottom