Kwa taarifa rasmi na ya uhakika toka CCM waliojiandikisha hadi mwaka Jana hadi march mwaka huu pamoja na wakulipia card zao ni 15,000,000 waliojiandikisha April hadi July ni zaidi ya 2,000,000. Bado wale walioamua kuunga mkono juhudi za rais👍
Usisahau jumla ya wapiga kura ni 29,000,000
We data za CHADEMA unazijua au unasikia? Wanachama vijana zaidi mil. 14, akina mama mil. 3 wazee mil2 hapo hujagusa wasio na kadi .
Ni hivi habari ya data za wanachama wa vyama tuachane nayo kabisaa!
Hii habari ya kila chama kujifanya inatoa takwimu haina afya kwa mstakabali wa matokeo ya uchaguzi.
Hata CHAUMA, CUF, TLP wataibuka na takwimu zao, tena za mamilioni ya wanachama. Ukiiwajumlisha utakuta Tanzania ina wanachama wa vyama vya upinzani zaidi ya milion 100 wakati idadi ya watanzania ni milioni karibia 60.
Tusijichanganye, na tusipotoshe wananchi kwa takwimu uchwara. Mwenye kadi ya CCM hazuiliwi kumpigia kura Tundu Lisu na mwanachama wa TLP anaweza kumpigia kura Magufuli.
Kama hivyo ni kweli basi, takwimu zetu za wanachama tuendelee kuzihifadhi kwenye makabati yetu maana hazina mahusiano yeyote na kura. Lowasa, Sumaye, Kingunge ni CCM kindakindaki lakini mwaka jana walikipigia kura CHADEMA.
Kuna watu wanaendelea kuunga juhudi na wengine sera ya UHURU, HAKI NA MAENDELEO inawaamsha wanabadili maamuzi, wanaona waende kwa upande wa ukombozi japo wana kadi za CCM. Wengine wanalipiza kisasi cha kukatwa wakati wajumbe waliisha amua ya kwao.
Hii habari ya Polepole ya takwimu za wanachama ni propaganda, tusiipe uzito, tuipotezee. CCM kuwa na wanachama milioni 15 ni jambo la kusadikika tu, halina ukweli wowote.