Lililo dhahiri na ambalo naona wengi wetu hatulijui au hatutaki kulijua, ni kwamba Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM anajulikana kwa wenye chama tangu mapema. Kinachofanyika ni kukamilisha taratibu tuu.
Wajumbe watabakia kupiga kura na hata wote wakiamua kumkataa mmoja wao, aliekataliwa anaweza kutangazwa mshindi. Kwani nani anaesaidia kuhesabu kura? Kama kuna watia nia ambao walikuwa wanataka kuona demokrasia ya kweli kwenye mchakato mzima, Wangeomba chama chao kibadili kanuni, ili chama cha upinzani kisaidie kuhesabu kura na kutoa matokeo!
"Kwa sasa kazi iliyobakia ni kukamilisha taratibu tu"
Kidumu chama chetu