Kama huko ndiko kuona mbali basi neno "kuona mbali halina maana":blabla:
You are very right and this is unacceptable! Tatizo ni kuwa wahusika hawalioni kabisa hili na wanaridhika kirahisi sana hapana tuseme imetodsha sasa! Imetosha ajira zooote za mashirika ya fedha mazurimazuri wanapewa dini moja hii haikubaliki kabisa. Magufuri amewekwa hapo kutuidanganya wananchi na wengine wanadanganyika let us wake up!!!!!
Wakipitisha madudu bungeni Poa, Wakipitisha madudu huku kwenu povu hadi puani
Nimekusamehe kwa maana mie sio mjinga. Kulingana na maelezo ya Nape mara tu baada ya kikao kuisha, amesema hatatangaza majina matatu, wasubiri kesho! Sasa mjinga nani hapo?
Hawana jipya hawa UKAWAkwa style hii ukawa mtasubiri sana,kama mindset ndo ziko hivi
Wakuu habari,
Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.
Karibuni sana.
=================
Updates;
1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.
2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu
3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state
4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.
5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.
6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano na kamati ya maadili ya Wagombea urais.
7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.
8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.
9. Update 22:55
CC bado inaendelea, sasa hivi watu wa catering wanawapelekea vyakula na vinywaji (Pengine ni daku ya leo kwa waliofunga?)
Julai 11, 2015:
1. Update 01:00
CC imemaliza kikao chake; Nape kakutana na waandishi na kuna tetesi kuwa kuna kundi lilikuwa linajipanga kufanya mapinduzi ya Mwenyekiti wa CCM. Aidha, Nchimbi na wenzake wawili wameondoka wakiwa wamejaa jazba na wameonekana kutokubaliana na maamuzi ya CC. Updates zaidi zinafuata...
2. UPDATE 01:20
Hatimaye 5 Bora imejulikana, ni:
1) Bernard Membe
2) John Magufuli
3) Asha Rose Migiro
4) January Makamba
5) Amina S. Ali
View attachment 267181
3: Update 12:00
Nchimbi, Mkono na Kibajaji wamezuiwa getini wasiingie mkutanoni kisa hawana vitambulisho. Baada ya tafrani ya takribani robo saa wajumbe hao wameruhusiwa kuingia.
4: Update 12:15
Mwenyekiti wa CCM Taifa, mh. Kikwete amefungua kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (NEC) cha kuchuja majina matano nafasi ya kugombea Urais.
5: Update 12:51
NEC imemaliza kikao cha kupiga kura, Tatu bora inatangazwa hivi punde (Kama itatokea)
6: Update 13:05
Kikao cha Halmashauri Kuu kimepitisha jina la Dr. Shein kuwa mgombea wa Urais Zanzibar.
7.Update 13:25
Wanec wametoka nje, hawana imani na CC, wanahoji kwanini Membe apite 5 bora, Lowassa aachwe?. Wametishia kuifuta CC. Ngoma imeachwa wazee kina Mwinyi na Mkapa wamebaki wakishauriana na viongozi nini cha kufanya.
8. Update 13:33
Hali ni tete Dodoma, Wapambe wa Lowassa, Wametishia Amani, Wamejikusanya kwenye bustani ya Nyerere Squre Wanaimba. Tunamtaka Lowassa tunamtaka Lowassa...!!
9:Update 14:00
Mkutano umefunguliwa na Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete na kuahirishwa baada ya Dakika saba kwa kile wanachodai ni kuruhusu watu wakapate Chakula cha mchana. Wakati Mwenyekiti wa Chama anaingia, Wajumbe wa NEC walimpokea kwa wimbo wa "Tuna imani na Lowassa" hadi rais anakaa wameendelea kuimba.
10: update 17:30
Mkutano wa NEC, wajumbe wanapiga kura hivi sasa kupata wagombea tatu (3) BORA. Mkutano mkuu wa Taifa Utaanza saa TATU usiku.
Kuna watu sijui wamekula malimao?we nadhan ulikua unaangalia marudio AZAM TV & CHANEL 10.
ngoma ni leo kuanzia saa 3 uck
Magufuli
Migiro
Makamba
wanatanzania kama kweli tuna nia njema na mama Tanzania{kama mbatia anavyopenda kuita} hiki chama kinapashwa kupumzishwa kushika hatamu, kupitia huu mchakato nimejifunza mambo kadhaa
1.huwezi kuwa kiongozi ndani ya ccm hata kama unakubalika na wanachama wote wa ccm
2.unaweza kuwa kiongozi wa ccm pale tu kiongozi/viongozi wa juu wa chama,pamoja na familia zao,tunalionna hili kwa mwenyekiti
3.matajiri wanawachagulia ccm/Tanzania viongozi
Top three
1. Magufuli
2. Membe
3. Migiro
Kusudio la ccm ni kumpitisha Membe lakini Kwa kuwa mamvi amekatwa timu yake itahamia kwa Magufuli ili kumkomoa #Membe
Hapo wanao baki ni
1. B. Membe
2. J. Makamba,
3. A. Ally
mwisho wa kuwasilisha
Yaani nimefurahi sana kwenye hiyo orodha. Hapo Magufuli akipita roho kwatuuuuuu!Mkuu nimewambia watu hapa wanataka kunitoa roho heb wape nawewe
Mrembo una majibu mazuri hadi nimekupenda ghafla. Ntakupataje aisee??
Fact! Naona wameonja uchungu ambao huwa tunaupata pale ambapo wanaptisha madudu bungen tena kwa mbwembwe