Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

abu sahafu mkuu wa propaganda .we have surrounded them ,we are bombing them ,wakati airport imeshatekwa.
Huyu Nape ana maneno na mbwembwe sana yaani anavyobwabwaja na kuarusha roho watia nia. Huyu anafaa sana kuwa kama yule msemaji wa Iraq kipindi cha vita na USA na partners wake.
 
Wajumbe wa CC wanatoka mule wakijua kabisa kuwa fulani ma fulani ndo wamepita. Hadi sasa Lowasa lazima ajue kama kapita au lah, na lazima CC imueleze kuwa tumekuacha kwa sababu hii, hii na hiii...
Tungekuwa tushajua tayari maana angewaambia watu wake wa karibu

lowasa ni nani mpaka yeye ndo ambiwe na sio wengine 28. Au kwa kuwa ana nguvu za pesa za kifisasi kupitia Richmond?
 
Wakuu habari,

Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.

Karibuni sana.

===================

Updates;

1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano
na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.


-------

JINA la Edward Lowassa, mmoja wa wasaka urais kwa udi na uvumba, limeenguliwa katika hatua za awali za kinyang’anyiro hicho. Anaandika Saed Kubenea …(endelea).
Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na mmoja wa viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinasema, jina la mwanasiasa huyo limeondolewa kutokana na shinikizo la baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho.
“Ni kweli jina la Lowassa limeondolewa katika kinyang’anyiro hiki. Baadhi ya wakubwa wamekuja na msimamo na wameapa kutosikia mtu anayeitwa Lowassa likikatiza na kuingia NEC,” ameeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.
Vikao vya uteuzi vya CCM – Kamati ya Maadili, Kamati Kuu (CC) na Halamashauri Kuu – tayari vimeanza mjini Dodoma mchana huu. Kikao cha NEC kinatarajiwa kuanza saa mbili usiku.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, ikiwa Lowassa ataondolewa katika kainyang’anyiro hicho katika hatua za awali, basi ndoto za mwanasiasa huyo kushika madaraka ya juu katika nchi, zitakuwa zimezimwa.
Lowassa amekuwa akihaha kutaka kuwa Rais wa Jamhuri tangu mwaka 1995, ambako alijitosa kugombea nafasi hiyo.
Hata hivyo, jina lake liliondolewa katika hatua ya awali baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere “kumng’ang’ania” na kushinikiza kuobdolewa kwa jina lake.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Lowassa hakujitosa katika kinyang’anyiro hicho; badala yake alimuunga mkono Kikwete kwa makubaliano ya kufanywa kuwa waziri mkuu na baadaye kuwa rais.
Habari zinasema, kuzimwa kwa ndoto za Lowassa, kunafuatia taarifa kuwa mchakato wa uchujaji majina ya wasaka urais kupitia CCM, kuendeshwa na baadhi ya vigogo kutoka idara ya usalama ambayo imesheheni “wabaya” wake.
Lowassa, mwanasiasa machachari katika siasa za CCM, ni miongoni mwa makada 38 wa chama hicho waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama chao kugombea wa urais wa Jamhuri.
Inaelezwa kuwa vita ya kisiasa anayopigana Lowassa kwa sasa, siyo tena kati yake na chama chake, bali ni kati yake na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
Mgogoro wa Lowassa na TISS unatokana na ukaribu wa mwanasiasa huyo na aliyewahi kupata kuwa Mkurugenzi mkuu wa idara hiyo, Apson Mwang’onda.
“Lowassa akiteuliwa kugombea nafasi hiyo, atakuwa amewashinda watu wa usalama waliopo sasa; jambo ambalo haliwezi kukubarika,” kimeeleza chanzo kimoja cha taarifa mjini Dodoma.
Anaongeza, “…ikiwa hivyo, maana yake ni kuwa TISS iliyoko kwenye uongozi wa sasa itakuwa imeonyesha udhaifu mkubwa mbele ya Apson anayeratibu mbinu na mikakati ya Lowassa.”
Mkurugenzi wa usalama wa sasa, Othuman Rashid anadaiwa kumuunga mkono Bernard Membe, mmoja wa wasaka urais anayetajwa kuwa chaguo la Kikwete.
Katika hatua nyingine, taarifa zinamnukuu mmoja wa viongozi wa kamati kuu akisema, chombo hicho muhimu katika uteuzi wa wagombea urais, imegawanyika.
“Mgawanyiko unatokana na baadhi ya watu kutaka Lowassa asikatwe, huku wengine wakisema, sharti aondolewe,” anasema mmoja wa watoa taarifa wa gazeti hili.
 
Ungeweza kabisa kunijibu kuwa umejuaje kuliko kuninukuu na kunambia nipitie post za nyuma!

Nyuma wapi? Mada ina kurasa 37 and counting halafu unanambia nirudi nyuma?

Good grief!

Tumetumiwa taarifa na chanzo cha kuaminika, ni part ya vikao vinavyoendelea
 
Hivi UKAWA mnataka mgombea gani ambaye mnaona mtamuweza.

CCM hata wampitishe yule mkulima bado atamuacha mbali sana Dr.Slaa.

UKAWA wanamuogopa sana Lowassa sijui kwa nini.
 
Duuuuhhhh..........naona wamenganisha ftar,, daku na kuswali taraweh kabisa...
 
Back
Top Bottom