Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Ssi tuko kitako tunasubiri kutoka Ddm
 
Wanabodi kulikuwa na kamati ya maridhiano ambayo imefanya vikao inje ya vikao rasmi kwa nia ya kufikia mwafaka kabla ya kikoa cha kamati kuu CC kuanza.

Kikao hiki wamepalulana tu hakuna mwafaka wowote uliofikiwa sasa kikao cha kamati kuu kinaanza hivyo hivyo

Sababu ya kutofikia mwafaka imesemekana ni mwenyikiti is so weak in decision making anayumbishwa na majumbe hata wale wajinga wajinga
 
Kikao cha maadil na usalama chini ya Mwenyekiti wake Ndg Jakaya Mrisho Kikwete kilichokutana katika ukumbi wa whitehouse kimemaliza hivi punde.

Kikao hicho kilichokuwa na ajenda moja tu ya kujadili na kupitisha majina ya wagombea watano watakaopitishwa na NEC ya CCM baadae leo.

Taarifa iliyopo ni kuwa Jaji Augustino Ramadhani, Mhe Pinda, Bernard Membe, prof Mwandosya pamoja na mzee Wassira ndio waliopitishwa na kikao hicho.

Kikao cha Kamati Kuu kitakachoanza saa kumi na moja kitajadili majina matano hayo..
 
Wanabodi kulikuwa na kamati ya maridhiano ambayo imefanya vikao inje ya vikao rasmi kwa nia ya kufikia mwafaka kabla ya kikoa cha kamati kuu CC kuanza.

Kikao hiki wamepalulana tu hakuna mwafaka wowote uliofikiwa sasa kikao cha kamati kuu kinaanza hivyo hivyo

Sababu ya kutofikia mwafaka imesemekana ni mwenyikiti is so week in decision making anayumbishwa na majumbe hata wale wajinga wajinga

Maridhiano CCM wameyafahamu lini?

Kama CCM wangekuwa wanafahamu maridhiano basi wasingetuharabia rasimu ya Warioba kwenye BMK.

Hivyo sishangai hiyo kamati inayojiita ya maridhiano kushindwa kufikia muafaka.
 
Kuna mtu kanitumia text ofisini kwamba niangalie Channel 10 is like wamesema kitu kwenye taarifa zao za habari, anybody aliyecheki huko please hebu atupe updates tafadhari
 
Haina mamlaka ya kuchuja watu hiyo inapitia kuangalia kama kuna waliokiuka kanuni.
 
Hahaaa ngoja nisuke mkeka 5top (Augustino Ramadhani, Asha rose Migiro, Magufuli, Makongoro Nyerere, Mark Mwandosya .

Top 3 Augustino Ramadhani, Magufuli, Mark Mwandosya.

Na mwisho watakuwa hawa Augustino Ramadhani na mgombea mwenza Magufuli namaliza kufunga mkeka tuonane Jumapili.

kuliko kumweka Magufuli awe mtembea na mkasi,bora wamwache hivihvi tuje tumpe tena uwaziri
 
Back
Top Bottom