Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Hivi UKAWA mnataka mgombea gani ambaye mnaona mtamuweza.

CCM hata wampitishe yule mkulima bado atamuacha mbali sana Dr.Slaa.

UKAWA wanamuogopa sana Lowassa sijui kwa nini.
Malizeni kwanza ya kwenu. Nyinyi wenyewe ya kwenu yanawashinda mnageukia UKAWA
 
Mpaka sasa nimegundua watanzania wengi tu misukule ya ccm.
 
Wakuu habari,

Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.

Karibuni sana.

===================

Updates;

1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano
na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.


-------

soma mwanahalisi online kuna hot news
 
CCM msifanye kosa la kutomteua LOWASSA,Hata Vyama vya upinzani vinashupalia sana asiteuliwe kwa sababu ni Mwiba kwao. Lowassa anakubalika duniani hata Mbinguni, ndio maana hata wapinzani wa CCM wanamuogopa sana.
 
Lowasa kua mgombea mwenza wa agustino ramadhani
Huu ndio uamuzi wa busara na hekima kukinusuru chama
 
Na Haswa Kipindi Hiki Ambacho Wengi Wetu Akili Zimepotea Kidogo Juu Ya Pressure Ya Nini Kinaendelea Jijini Dodoma. Tuvumiliane Tu!

Nimekuvumilia mkuu wala sioni shida kwa kua naamini kua kila asemacho mtu basi ni mawazo yake na ana haki ya kusema asemavyo. Basi tuendelee na mchakato wa uteuzi
 
Back
Top Bottom