Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KAULI HII YA KINGUNGE MCHANA INASHTUA KIDOGO
![]()
KINGUNGE Ngombare Mwiru, ambaye ni kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametabiri anguko na mpasuko mkubwa ndani chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, endapo chama hicho kitaacha kumpitisha mgombea urais anayekubalika kwa wananchi wengi.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya jina la Edward Lowasa, aliyekuwa anasaka urais kwa udi na uvumba, kuenguliwa kutoka majina matano yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC- NEC).
Kutajwa kwa majina ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Amina Salum Ali, January Makamba na Dk. Asha-Rose Migiro na Kamati kuu kwamba ndio watajadiliwa na Halmashauri Kuu (NEC), kumemfedhehesha Kingunge hata kusema, "…hatua ya kwanza itakuwa kumweka mgombea ambaye hakubaliki ndani ya chama na hakubaliki nje ya chama. Itakuwa ni kura ya hasira."
Kingunge ametoa kauli hiyo kwa kusitasita huku akionekana kuwa na huzuni wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha luninga leo mchana.
Japo Kingunge hakutaja jina la Lowassa lakini ni muungwa mkono katika mbio zake za kuusaka urais hata wakati wa mkutano wa kutangaza nia mjini Arusha Kingunge alisema, "…Lowassa ndiye pekee anasifa za kuwa rais wa Tanzania."
"Utaratibu wa mwaka huu una matatizo. Kilichotokea ni mazingira yanayotia shaka. Kwa sababu ya muda hakuna atakae kata rufaa. Inaonesha kwamba uongozi umeshakuwa na msimamo juu ya mgombea wanaemtaka," amesema Kingunge.
Amesema kazi ya CC-NEC ni kuyapitia, kuangalia sifa, kuwapima, kuyalinganisha na kisha kutoa mapendekezo. Hawana madaraka ya kuamua.
Kuhusu kukubalika kwa majina hayo na NEC, Kingunge amesema, "…wajumbe wa NEC wanaweza kukubaliana nayo, wanaweza kusema hapana, wanaweza kusema wote waliopendekezwa hawafai na wanaweza kutoa mapendekezo waletewe majina mengine."
Amesema kuwa yanayotokea sasa na yatakayotokea baadae ni mazingira ambayo yamekuwa yakijengwa kwa muda mrefu.
Kuhusu sifa za mgombea anayemtaka, Kingunge amesema ni lazima: Aweze kupambana na nguvu ya upinzani; anayekijua chama; awe na uzoefu wa masuala ya ulinzi na usalama na mtu atakae watoa watanzani kwenye umasikini.
Haiwezekani mtu achaguliwe kwa sababu ya pesa zake bwana.uongozi haununuliwi.
Makamba anakwenda kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, JK alitaka kumuweka Bilal lakini akaona huyu kigogo kumnyofoa itakuwa ngumu kukubali matokeo.
Teh teh!Gwajima nae sijui yuko kwenye hali gani muda huu!!
Wala sijapanic nimekuuliza kiustaraabu kuna kipindi umenitukana nikakueleza kiustaraabu naona bado unaleta kejeli.
Mkuu nikuambie kitu hii ni ID yangu kama ya ya 20 hivi Invisible anajua nimetulizana sasa hivi mkuu usitake kunirudisha miaka ya 2009 wakati najiunga JF mimi nimeisha pigwa life ban mara tatu hizi ban za miezi 6 sijui miezi 3 nyingi tu achana na ban za siku hizi wiki.
Nadhani umenielewa na Mods mashaidi.
Naomba mechi na wewe mkuu
Katika harakati ya kuwapooza kundi la akina Lowasa.Ili chama kisije paraganyika.
Ninachoona kuna mchezo hapa unachezezwa Mkutano Mkuu watakuwa Rubber Stamp tu. Raisi atakuwa Kati ya Amina na Magufuli.
Ila kwa vile Watanganyika ni wengi basi Amina inabidi akae pembeni asubiri kuteuliwa kuwa Makamu wa Raisi.
Kama hiyo tetesi ni kweli kwamba ni Makamba ,Magufuli na Amina.
Ila Mwenyekiti angetamani Makamba-kwa masilahi Binafsi.
Msipoangalia sawasawa miaka kumi ijayo mtaongozwa na mwanamama