Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

aende akajiunge na cha kingine yeye si anajimini raia wengi wanamkubali kwani lazima awe raisi kupitia ccm?!
 
Akiwa anahojiwa na Charles Hilali Kingunge amesema mazingira ya kuwakata baadhi ya wagombea yalijengwa mapema,na viongozi waliopo serikarini mapema kabisa.

Sasa maamuzi yanayo tokea na yatakayo tokea,yatatokana na kile ambacho kiliandaliwa toka mwanzo.

KAULI HII YA KINGUNGE MCHANA INASHTUA KIDOGO

kingunge2-620x308.jpg



KINGUNGE Ngombare Mwiru, ambaye ni kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametabiri anguko na mpasuko mkubwa ndani chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, endapo chama hicho kitaacha kumpitisha mgombea urais anayekubalika kwa wananchi wengi.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya jina la Edward Lowasa, aliyekuwa anasaka urais kwa udi na uvumba, kuenguliwa kutoka majina matano yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC- NEC).

Kutajwa kwa majina ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Amina Salum Ali, January Makamba na Dk. Asha-Rose Migiro na Kamati kuu kwamba ndio watajadiliwa na Halmashauri Kuu (NEC), kumemfedhehesha Kingunge hata kusema, "…hatua ya kwanza itakuwa kumweka mgombea ambaye hakubaliki ndani ya chama na hakubaliki nje ya chama. Itakuwa ni kura ya hasira."

Kingunge ametoa kauli hiyo kwa kusitasita huku akionekana kuwa na huzuni wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha luninga leo mchana.

Japo Kingunge hakutaja jina la Lowassa lakini ni muungwa mkono katika mbio zake za kuusaka urais hata wakati wa mkutano wa kutangaza nia mjini Arusha Kingunge alisema, "…Lowassa ndiye pekee anasifa za kuwa rais wa Tanzania."

"Utaratibu wa mwaka huu una matatizo. Kilichotokea ni mazingira yanayotia shaka. Kwa sababu ya muda hakuna atakae kata rufaa. Inaonesha kwamba uongozi umeshakuwa na msimamo juu ya mgombea wanaemtaka," amesema Kingunge.

Amesema kazi ya CC-NEC ni kuyapitia, kuangalia sifa, kuwapima, kuyalinganisha na kisha kutoa mapendekezo. Hawana madaraka ya kuamua.

Kuhusu kukubalika kwa majina hayo na NEC, Kingunge amesema, "…wajumbe wa NEC wanaweza kukubaliana nayo, wanaweza kusema hapana, wanaweza kusema wote waliopendekezwa hawafai na wanaweza kutoa mapendekezo waletewe majina mengine."
Amesema kuwa yanayotokea sasa na yatakayotokea baadae ni mazingira ambayo yamekuwa yakijengwa kwa muda mrefu.

Kuhusu sifa za mgombea anayemtaka, Kingunge amesema ni lazima: Aweze kupambana na nguvu ya upinzani; anayekijua chama; awe na uzoefu wa masuala ya ulinzi na usalama na mtu atakae watoa watanzani kwenye umasikini.


 
Makamba anakwenda kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, JK alitaka kumuweka Bilal lakini akaona huyu kigogo kumnyofoa itakuwa ngumu kukubali matokeo.

kupitia serikali ya Chama kipi?

Nyoo!! mmevimbiwa mkamwaga chakula na kuteketeza maghala mkizani matumbo yatabaki hivyo hivyo.

Sasa subirini Serikali ya Ukawa alafu mwangalie huyo mnayesema kuwa atakuwa waziri wa mambo ya nje atapitia mlango gani.

Mmelikoroga wenyewe na nilazima mlinywe na bahati mbaya mnanyweshwa.

mani**#*nazenu##@%$#*
 
Mkutano umefunguliwa na Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete na kuahirishwa baada ya Dakika saba kwa kile wanachodai ni kuruhusu watu wakapate Chakula cha mchana. Wakati Mwenyekiti wa Chama anaingia, Wajumbe wa NEC walimpokea kwa wimbo wa "Tuna imani na Lowassa" hadi rais anakaa wameendelea kuimba.


Raisi nae pia alikuwa anaimba.
 
hakuna kitu kama hicho. mabomu huwa wanapigwa raia wa kawaida wasio wanaccm
 
Wala sijapanic nimekuuliza kiustaraabu kuna kipindi umenitukana nikakueleza kiustaraabu naona bado unaleta kejeli.

Mkuu nikuambie kitu hii ni ID yangu kama ya ya 20 hivi Invisible anajua nimetulizana sasa hivi mkuu usitake kunirudisha miaka ya 2009 wakati najiunga JF mimi nimeisha pigwa life ban mara tatu hizi ban za miezi 6 sijui miezi 3 nyingi tu achana na ban za siku hizi wiki.

Nadhani umenielewa na Mods mashaidi.

mkuu hebu kuwa specific nimekutukana wapi? ni quote kwenye hilo tusi

Isijekuwa una refer mtu mwingine

Acha kukurupuka......relax....onesha tusi ulilotukanwa

Ebooooooooooooooooooooooo...Hii ni ID yangu ya 700
 
Wakuu mkutano unakaribia kuanza na wajumbe wameshaingia ukumbi mpya wa mikutano wakisubiri wajumbe walio kwenye mkutano wa NEC waje na majina matatu. Hii link tayari imeanza kuonyesha

[video]http://livestream.com/CCM/Uchaguzi2015[/video]


UPDATE:

Nape ametangaza kuwa Top 3 itasomwa saa tatu usiku na moja kwa moja mkutano mkuu utaanza.
 
Katika harakati ya kuwapooza kundi la akina Lowasa.Ili chama kisije paraganyika.

Ninachoona kuna mchezo hapa unachezezwa Mkutano Mkuu watakuwa Rubber Stamp tu. Raisi atakuwa Kati ya Amina na Magufuli.

Ila kwa vile Watanganyika ni wengi basi Amina inabidi akae pembeni asubiri kuteuliwa kuwa Makamu wa Raisi.
Kama hiyo tetesi ni kweli kwamba ni Makamba ,Magufuli na Amina.

Ila Mwenyekiti angetamani Makamba-kwa masilahi Binafsi.

Mkuu JK ana uwezo mkubwa sana, usisahau kwamba yeye bado ni Rais wa nchi hii, huyo magufuli atapozwa kwa uPM, Amina ni Makamu kwa kuzingatia gender na uzanzibar wake. Makamba ni mtoto wa JK chochote atakachoamriwa na JK yeye atakubali tu. After all yeye ni naibu waziri, hata akipewa kawizara kanamtosha.

Rais ni Mwanausalama Bernad Membe.
 
kuna tetesi nimezipata kwamba kura zimekuwa ngumu ndani ya NEC,asilimiq 90 wamepiga hapana,kura zinarudiwa mara ya tatu sasa na mijadala ni mikali,wajumbe ni kama hawamwogopi jk,labda kwa vile muda wake umekwisha,mkutano mkuu unaweza kufanyika kesho kitu ambacho kitayapa makundi muda wa kuzungukia wajumbe wa mkutano mkuu na kujiimarisha zaidi
 
Back
Top Bottom