Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Nimeilenda Hii, Lakini, Kama Mkiwapa UKAWA Wabunge, Magufuli Si Atashindwa Kuendesha Serikali? Hiyo Ni Sawa Na Kupewa Mbuzi Unaambiwa Kula Nyama, Huku Kisu Huna. Hata Hivyo, Acha Ukawa Waongeze Idadi Ya Wabunge, Manake Wamekuwa Wakiburuzwa Buruzwa... UKAWA, Tumaini Jipya!
 
Dr. Magufuli

Atapata Waziri Mkuu mzuri na baraza la mawaziri wazuri. Ondoa hofu. No body is perfect.

Queen Esther
 
Shame, mimi sihitaji speech tamu tu halafu utendaji tofauti. Kama speech za JK zingetekeleka, leo tungekuwa mbali zaidi. Mimi sitaki ornamental speech kama za kumtongoza mwanamke, nataka honest and serious speech zinazonipa matarajio ambayo nitayaona wakati wa utekelezaji.
 
Matokeo ya mgombea urais kwa tiketi ya CCCM!
 

Attachments

  • 1436685623114.jpg
    1436685623114.jpg
    28.2 KB · Views: 432
JK kapewa za uso, Lowasa za mbavu sasa wote wanahuguzia maumivu. Jana JK kasahau kama yeye bado M/Kiti. Kiwewe chote hicho
 
Apunguze mihemko na mijaziba isiyo na msingi kuwa raisi si jambo dogo. Kule alizoea command ila huku kwingine inabidi ajitafakari na awe na hekima kabla ya kuzungumza.
 
Ni katika mkutano mkuu wa taifa jana ambapo mikoa na kanda kadhaa zilionekana kufadhaishwa na matokeo ya mchujo wa tano bora na tatu bora. Mikoa hiyo haikuweza kutoa ushirikiano kwa mheshimiwa mwenyekiti kwa kuwa ilitawaliwa na huzuni huenda na chuki. Mikoa mingine iliyonuna ni Mtwara na Lindi kwani nao hawakuipokea salam ya JK kama ilivyozoeleka .Membe alitarajia sana ,Lowasa alitaraji sana. Mwandosya alidhani kama ya kikwete kuwa safari hii watamuonea aibu wakala kichwa Tanga walikua na ndoto za ghafla zikatoweka. Mfumo wa vyama vya siasa kuketi kikanda na kimikoa unabidi kutazamwa ki-great thinking
 
Kwa kanda ya Ziwa ilivyozizima jana usiku na sms kutembea sana usiku baada ya Magufuli kuwa 3 bora!?UKAWA tunayo kazi
 
Jamaa ni mkabila lakini pia ni fisadi..pale kwao lubabangwe kajenga nyumba zaidi ya 60 kawapingisha viongozi wote wa wilayani..pia kajimegemea eneo kubwa kaweza uzio..kajamaa ni kafisadi tunakajua

Nyumba 60 mnapiga kelele fisadi wakati watu wameamua kuweka vitega uchumi wazi, wakificha hela napo mtasema fisadi maana mtaanza jamaa na vyeo vyote ana nyumba moja ya kawaida. Kwa level ya Magufuri yaani umri wake na nyadhifa alizoshika nyumba 60 ni kawaida kwake, kama mbunge wa eneo lile itakuwa ajabu kama alikomaa bungeni Chato iwe wilaya alafu asiwe miongoni mwa wananchi wa Chato wanaojenga nyumba kwa ajili ya kupangisha watumishi wa serikali na wengine (fursa ya kibiashara). Tuamke watz wenzangu si kila mtu anapofanya kitu kikubwa ni fisadi na hii ipo hata maifisini yaani mnalipwa mshahara mmoja mwingine kajenga na mwingine kajaza shelf la viatu alafu baadae aliejenga anaambiwa fisadi
 
Mtajikomba sana safari hii. Kumbuka maneno kuwa chama hakitawaangusha mwaka huu. Kitawaletea mgombea anayekubalika kwa wananchi na anauzika. Kwamba chama hakitateua mtu anayewakilisha mambo yanayowachukia wananchi. Na huyo si mwingine ni huyu hapa
image.jpg
 
Back
Top Bottom