Yaliyojiri katika Ziara ya Rais Samia Mkoani Morogoro

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wakuu salaam,

Leo Julai, 7 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili katika maeneo ya Msamvu manispaa ya Morogoro, Dumila wilayani Kilosa na wilaya ya Gairo.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw. Martin Shighela alisema ziara hiyo ya Samia Suluhu Hassan atakutana na Wananchi na hivyo akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wao.

Pia Rais Samia anatarajiwa kushiriki mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania utakao fanyika Julai 8 katika manispaa ya Morogoro.

Tutakuwa hapa sote kuwaeleza yanayojiri.
 
Kila la kheri ziara hiyo vipi mpango kuumega Mkoa Morogoro? Vipi kuzungukia Kilombero Mahenge Malinyi Ulanga etc ? Karibu Morogoro Mama.....msisahau kujikinga Corona hali sio nzuri
 
Mnapopata bahati ya kuongea na Rais, muwe mnafikisha kero zinazoikabili jamii husika.

Mfano hapo Morogoro JPM alifanya ubabe kwa mwekezaji wa kile Kiwanda cha Tumbaku (TTPL) hadi wakasusa wakafunga kiwanda. Hivyo zaidi ya wakazi 10,000 wakajikuta wanakosa ajira sasahivi wapo mtaani.

Hivyo tumieni fursa hiyo mwambieni Mama amrudishe huyo mwekezaji.
 
Kila la kheri ziara hiyo vipi mpango kuumega Mkoa Morogoro ? Vipi kuzungukia Kilombero Mahenge Malinyi Ulanga etc ? Karibu Morogoro Mama.....msisahau kujikinga Corona hali sio nzuriJoj
Kwa kweli mkoa wa Morogoro unapaswa kumegwa.
 
Hivi huyo mzee wa Msoga hajastaafu?

Nina mashaka kuwa ana fanya kazi ya urais kwa mara maana ya kuwa hajastaafu
Anampango wa kugombea uchaguzi ujao jiandae. Katiba sio msa..fu..
 
Mama aende na style yake tu aliyoanza nayo: awezi kuwa kama Magufuli wakati team Magufuli keshaifumua.

Watu washaacha kumfananisha na Magufuli aina maana awezi kumzidi..
Ziara za Rais mikoani zilianzishwa na Magufuli?

AMA kweli mahaba nibabue...
 
Kila la kheri ziara hiyo vipi mpango kuumega Mkoa Morogoro? Vipi kuzungukia Kilombero Mahenge Malinyi Ulanga etc ? Karibu Morogoro Mama.....msisahau kujikinga Corona hali sio nzuri
Hiyo ziara ya mkoani Morogoro??
Viongozi waaende Malinyi, Mlimba, Mahenge, Mgeta Kisaki warranted ziara za kwenda na kurudi Morogoro mjini, ndiyo wataelewa Morogoro, siyo barabara tu ya Dar Morogoro.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hivi inasababishwa na na nini?, unakuta au unajikuta ghafla unamchukia mtu uliyekutana nae mara ya kwanza, na ukiulizwa huna sababu au hana sababu kwanini anakuchukia.
Ni tendo la kiasili sana ambalo liko juu ya nguvu ya kibinadanu kuweza kuli control ..hapa kanuni ya mvutano na ukinzani inahusika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu salaam,

Leo Julai, 7 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili katika maeneo ya Msamvu manispaa ya Morogoro, Dumila wilayani Kilosa na wilaya ya Gairo.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw. Martin Shighela alisema ziara hiyo ya Samia Suluhu Hassan atakutana na Wananchi na hivyo akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wao.

Pia Rais Samia anatarajiwa kushiriki mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania utakao fanyika Julai 8 katika manispaa ya Morogoro.

Tutakuwa hapa sote kuwaeleza yanayojiri.
Maza vijijini hafiki. Amewaachia chadema
 
Apitie na kukagua kiwanda cha miwa cha Mbigiri ambacho kimewatia hasara wakulima.

Atoe amri ya kukimaliza ili wakulima wapate kuuza miwa yao.
 
Back
Top Bottom