PreGE2025 Yaliyojiri Kesi ya Lissu: Mahakama imeahirisha shauri hadi 02/06/2025, mtuhumiwa amerejeshwa rumande

PreGE2025 Yaliyojiri Kesi ya Lissu: Mahakama imeahirisha shauri hadi 02/06/2025, mtuhumiwa amerejeshwa rumande

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
#HABARI:Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha hadi Juni 2,
FB_IMG_1747681510233.jpg
2025 kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu baada ya upande wa Mashtaka kusema kuwa uchunguzi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine.

Upande wa Serikali katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa zipo hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Hata hivyo, Mahakama pia imetoa uamuzi mdogo kwamba kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa njia ya kawaida na si kwa njia mtandao, huku wanaoudhuria kesi wakitakiwa kuacha mihemko ya kelele mahakamani.

Kesi hiyo ya uhaini ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franko Kiswaga ambapo awali Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga aliieleza Mahakama kwamba kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania
 
Huyu jamaa ni chaguo la Mungu kwetu na CCM inajuwa hivyo, ndiyo maana wanamfanyia figisu ili tu aonekane kuwa gaidi.....kwa kweli CCM ni washenzi mno.
 
"Ndoto" zangu na instincts zangu zinaniongoza hivyo na ndivyo ilivyo!
 
Huwezi jua.Ameanza kuangalia nyama za binadamu kwa uchu mkali.Baadaye anaweza kuomba aonjeshwe kipande amaizi kama kina chumvi ya kutosha.Kitakachofuata mimi sijui!
 
Huwezi jua.Ameanza kuangalia nyama za binadamu kwa uchu mkali.Baadaye anaweza kuomba aonjeshwe kipande amaizi kama kina chumvi ya kutosha.Kitakachofuata mimi sijui!
Boss, hakuna kichaa anaweza mnyonga kwa hizo tuhuma. Wala hakuna hata haja ya kulizungumza.
 
Siku tukijua kuingilia mahakama ni pamoja na kumwamba Rais amwqchie Lissu au yeyote aliyekamatwa tutaacha kulalamika serikali inaingilia mahakama.
 
Siku tukijua kuingilia mahakama ni pamoja na kumwamba Rais amwqchie Lissu au yeyote aliyekamatwa tutaacha kulalamika serikali inaingilia mahakama.
Sijaelewa unataka kutenganisha kipi na kipi kwenye nchi za Afrika kama Tanzania!?
 
Back
Top Bottom