Kata rufaaNilidhani mtuhumiwa anaingia Mahakamani dakika chache kabla hakimu hajakaa. Yaani mtuhumiwa anapewa saa nzima kupiga kelele? Mahakama ijitatjmini uendeshaji wa mashauri na shughuli zake.
Ungeomba ukae kwenye kiti uendeshe shauri hilo.Nilidhani mtuhumiwa anaingia Mahakamani dakika chache kabla hakimu hajakaa. Yaani mtuhumiwa anapewa saa nzima kupiga kelele? Mahakama ijitatjmini uendeshaji wa mashauri na shughuli zake.
Hakuna kesi hapo zaidi ya blabla za kiccm tu.
Nchi inahitaji ukombozi wa pili dhidi ya hawa wakoloni weusi.
Kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Mei 19.2025 kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Wakili Tundu Lissu ililetwa kwa ajili ya kutajwa, ambapo upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika
Jamhuri imesema mpaka sana shauri hilo linaendelea na uchunguzi chini ya mamlaka za Kipolisi, na kwamba kwakuwa upelelezi haujakamilika hivyo wanaiomba Mahakama kuhairisha kesi husika kwa siku 14 zaidi, jambo ambalo limeonekana kupingwa vikali na Mawakili wa utetezi
Jopo la Mawakili wa utetezi likiongozwa na Mawakili waandamizi Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala na Peter waliwasilisha maombi kadhaa Mahakamani hapo, ambapo miongoni mwake wameiomba Mahakama 'kulazimisha' upande wa Jamhuri ueleze nini hasa kinachokwamisha upelelezi kwa sababu mwanzo ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa ushahidi wote kuhusiana na shauri hilo upo mtandaoni
Jambo la pili walilowasilisha Mawakili wa utetezi Mahakamani hapo ni kwamba, hawafurahishwi namna ambavyo mteja wao anavyokuwa amezungukwa na maafisa wa Jeshi la Magereza (askari), ambapo wameishawishi Mahakama kutoa amri ya kuwaondoa askari wote 'wanaomlinda' Lissu ndani ya chumba cha Mahakama, kwakuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 Mahakama haimtambui mtuhumiwa kama 'mkosaji' na kwamba kitendo cha mteja wao kuzungukwa na askari wengi haikubaliki
Ukijibu hoja hizo, upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa licha ya kwamba Katiba imeeleza hivyo, lakini haijatoa maelekezo ya aina gani ya ulinzi inahitajika kwa mtuhumiwa pindi anapokuwa ndani ya chumba cha Mahakama, hivyo kuiomba Mahakama kutupilia mbali maombi hayo na kwamba ikiwezekana wanaomba ulinzi huo uongezwe
Mawakili hao wa serikali wameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa suala la ulinzi lina faida kwa mtuhumiwa mwenyewe, Mahakama na maafisa wa Mahakama kwa ujumla wake
Kuhusu suala la kueleza sababu inayopelekea upelelezi kutokamilika kwa wakati, Mawakili wa serikali wamejibu kuwa hakuna sehemu yoyote ya kisheria na Kikatiba inayowalazimisha kueleza hatua ya upelelezi iliyofikiwa, na kwamba mambo ya upelelezi sio ya kuwekewa hadharani, kikubwa kilichosisitizwa ni kwamba ndani ya muda waliiomba wa siku 14 wanaamini watakuwa wamefikia hatua nzuri ya upelelezi
Jambo lingine lililoibuka Mahakamani hapo ambalo limeletwa na upande wa utetezi, na ambalo halikupingwa na upande wa Jamhuri ni kuiomba Mahakama kutumia 'busara' zake kuondoa amri ya shauri hilo la uhaini kusikilizwa kwa njia ya mtandao badala yake mtuhumiwa awe anafikishwa Mahakamani moja kwa moja kama ilivyokuwa leo
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Mahakama imesisitiza Jamhuri kukamilisha upelelezi kwa wakati na tarehe ijayo Mahakama ipate mrejesho wa hatua iliyofikiwa, kuhusu suala la ulinzi wa Mahakama imesema mshtakiwa ni kweli anatakiwa kuwa huru akiwa kizimbani, hivyo tarehe ijayo Mahakama imeagiza vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kutosha kama hakuna sababu zozote za vitisho vya usalama wake basi mtuhumiwa awe huru peke yake akiwa kizimbani
Kuhusu suala la shauri hilo kuendelea kuendeshwa kwa njia ya mtandao, Mahakama imesema sheria inaipa Mahakama mamlaka ya kusikiliza au kuendesha shauri kwa njia itakayoona inafaa ikiwemo mtandao, na kwamba kwakuwa shauri hilo ni kubwa na linagusa hisia za wengi hivyo Mahakama imeona hoja za utetezi zina mashiko, hivyo Mahakama imeamuru tarehe ijayo shauri liendelee kwa mtuhumiwa kuletwa Mahakamani moja kwa moja kama ilivyokuwa leo
Baada ya kutoa maamuzi hayo, Mahakama imeahirisha shauri hilo kwa siku 14 hadi 02/06/2025 na mtuhumiwa amerejeshwa rumande
Ikumbukwe kuwa kesi hiyo ya uhaini kwa kawaida inasikilizwa kwa njia ya mtandao, leo imesikilizwa kwa njia ya kawaida kutokana na busara ya Mahakama kwakuwa mtuhumiwa anakabiliwa na shauri jingine Mahakamani hapo (shauri la uchochezi na kuchapisha taarifa za uwongo kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube)
======
Update Saa Nne Asubuhi: Kibatala aomba kesi ya Uhaini pia iendeshwe kwa njia ya mahakama ya wazi - Kwa kuwa kesi ya uhaini aliyopewa Tundu Lissu ina maslahi ya umma, mawakili wa utetezi wameomba mahakama kwamba mahakama itoe amri isiendeshwe kwa njia mtandao na kwamba itenganishe siku na kesi ya uchochezi na siku ya kesi ya uhaini na kesi zote mtuhumiwa aletwe mahakamani.
- Upande wa Jamhuri - Nassoro Katuga WSM, Job Mrema WKM, Tawabu Issa WS, Harrison Lukosi WS, Cuthbert Mbilinyi WS. Jopo la watu watano, linaiwakilisha Jamuhuri
- Upande wa Utetezi - Mpare Mpoki naongoza Jopo la Mawakili Akisaidiwa na; Wakili Alute Mugwai, Lugemeleza Nshala, Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya (will join later)Hekima Mwasipu, Gaston Garubindi, Michael Mwangasa, Jebra Kambole, Pasta Kang'oke, Emmanuel chengula, Deogratius Mahinyila, Michael Lugina, Deus Singa, Edward HecheSisty, MasaweJacob, Mugendi Ferdinand, MakoePaul KisaboIkoti, LissuDickson Matata. Maria Mushi, Elisa Kiiza Prosper, Dorice Kafuku, Mathias Mndimi, Andrew Chima, Happiness Michael, Meshack Makadede, Nashon Nkungu.
- Nassoro Katuga; Mheshimiwa hakimu Mkazi, Mshtakiwa yupo mbele ya Mahakama hii tukufu. Shauri hili linakuja kwa ajili ya Kutaja ,upelelezi bado lakini zipo hatua za mwisho. Ili kuitaarifu Mahakama yako ni hatua gani tumefikia tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa..
- Mpale Mpoki; kuhusiana ombi la Upande wa Mashitaka Kesi ilipokuja mara ya mwisho palikuwa na order ya Mahakama kwamba waeleze kitu gani kinakwamisha upeleleziWenzetu kwa kusahau wameshindwa kueleza kwanini upelelezi bado haujakamilika.
- Lugemeleza Nshala; ikupendeze Mheshimiwa hakimu, Msingi wa Makosa ya Jinai. Mshtakiwa anachukuliwa kwamba hana hatia mpaka atiwe hatiani na Mahakama
Unaweza kuona mshtakiwa anakuwa amezungukwa na maaskari, ni kweli mshtakiwa yupo mahabusu lakini hatakiwi anapokuwa katika kizimba kuzungukwa na askari
Askari waliomzunguka watoke nje wamuache akae pekee yake kizimbani. Tunaomba mahakama mshtakiwa apewe haki yake katika kizimba kwa kuheshimu ibara ya 16 (a) katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Peter Kibatala; Mheshimiwa hakimu tulipokuja mbele yako mara ya mwisho Mahakama hii,tulitoa ombi mbele yako. Mahakama hii tukufu iliamuru kwamba kesi itasikilizwa ana kwa ana (Mahakama ya Wazi). Mshtakiwa yupo katika kizimba by-default not by-desire.
Peter Kibatala; Hatuoni sababu kwamba katika kesi hii kutofautiana na ile ambayo halimu alisema itakuwa kwa njia ya mtandao.
Kifungu cha 392 CPA ya 2022 pamoja na kanuni ya 13(6b) ya Sheria ya Uendeshaji wa kesi kwa njia ya mtandao (GN 627 ) ya 2021 kanuni hiyo inaipa mamlaka Mahakama kubadili uamuzi huo kama Mazingira mbele yake yamebadilika
Inaipa mamlaka Mahakama hoja ni kwamba tupate hairisho. Kwa vyovyote vile hairisho litakuja. Tunaomba Mahakama baada ya Kusikiliza hoja ya hairisho isikilize hoja yetu.
- Peter Kibatala; Nakumbuka ulisema uamuzi wa kuendesha kesi kwa njia ya mtandao ulisema hoja ile siyo ya Kudumu.
Mazingira ya Kibadilika inaweza Kuendelea ktk Mahakama ya wazi. Tuna Maamuzi ya Mahakama kadhaa ,Mahakama ya rufaa
Civil appeal namba 421 kati ya Kareem S.S Vs Mahesh K.Patel
Mahakama inapaswa kutumia common sense katika kufikisha maombi ya haki
Kwa kuwa mshitakiwa ameletwa kwa kesi nyingine tunaomba Mahakama yako iridhie pia kuendesha kesi hii kwa njia ya wazi
- Hakimu; upande wa Jamhuri
Nassoro Katuga; Mheshimiwa hakimu Mkazi Mkuu, Tumesikia hoja za wenzetu. Tunaanza hoja ya Mahakama kutoa amri kuhusiana na suala la Upelelezi
Kusema hatua gani imezuia upelelezi hatuwezi kusema hadharani. Upelelezi una mambo mengi ikiwepo mambo ya siri
- WS Nassoro Katuga; Bahati mbaya sheria inaturuhusu hatupaswi kusema katika upelelezi tumepata nini na tumekwama nini..
Tunatumia nguvu za Kipolisi kufanya Upelelezi huo. Bado Mamlaka ya Kipolisi haijashindwa na hiyo ndiyo hatua tumeieleza Mahakama
- WS Nassoro Katuga; Hoja ya suala la Kikatiba ni kweli Kwamba mshtakiwa itachukuliwa kuwa yupo huru mpaka ahukumiwe na mahakama.
Kwa Bahati mbaya katiba haisemi alindwaje na kuletwaje. Katiba haisemi kwamba mshtakiwa halindwi. Kwamba Walinzi wakae nje, practically haijawahi Kuwepo. Kwamba Walinzi wakae nje, wakupokea order hawapo
Na bahati nzuri sana kaka zetu mawakili wasomi hawajaiambia Mahakama kwamba hawa Askari wamemzuia nini. Wamekaa naye na kuwa ndiyo Ma bodyguards wake
Tundu Lissu anatikisa kizimbani kuonesha kwamba hakubaliani kabisa na jambo hilo.
- WS Nassoro Katuga; Tunaona Mahakama ili iende vizuri, wenzetu wa Ulinzi na Usalama waendelee kumlinda Mshtakiwa wetu kizimbani, Mahakama na sisi Maafisa wa Mahakama.
Upande wa Jamhuri tunaendelea kusema ulinzi ungeimarishwa zaidi ya hapo.
- WS Nassoro Katuga; Kuhusu hoja ya 3, ni kweli order yako ilisema shauri hili lisikilizwe kwa njia ya mtandao..
Lakini Mahakama yako inaweza kutumia busara Kwamba Mahakama irudi kuwa kawaida au kuendelea kuwa ya wazi. Sisi kwa upande wa Jamhuri tunaiachia Mahakama yako tukufu kwa sasa ione inatakaje
- WS Nassoro Katuga; Lakini kwa sasa kuhusu Proceedings za leo kwamba inakuwaje leo shauri linaendelea kwa njia ya mtandao tofauti na amri yako
Hatuoni ni kosa kwa Mahakama kutumia njia ya Mahakama ya wazi kama mshtakiwa alikuja Mahakamani kwa kesi nyingine. Hatujaona Mahakama imeathiri nini kwa mshtakiwa ikizingatiwa ombi la mshtakiwa lilikuwa ni kuletwa
Hivyo Mheshimiwa tunaiachia Mahakama yako tukufu, itaamua inatakaje. Tunaomba hairisho mpaka siku zingine 14 tuweze kuendelea
Mheshimiwa ni hayo tu
- Hakimu; Mpale
Mpale Mpoki; nitaomba Mheshimiwa Nshala afanye Rejoinder
Lugemeleza Nshala; tunazungumzia mtu kupoteza haki yake ya Uhuru. Kama amri inavyosema, tulitakiwa tuambiwe ni hatua gani wamefikia
Badala yake tunasikia wanaomba siku 14 na yenyewe wanaleta maneno maneno tu. Tunapenda kusema kwamba Mahakama inatakiwa kuingia hatua ya kuchunguza
- Lugemeleza Nshala; Mahakama itoe amri ya mwisho na kwamba wasipofanya hivyo Mahakama itumie mamlaka yake kamili
WS Nassoro Katuga; Mheshimiwa wanaleta maombi mapya
Hakimu; maombi gani?
WS Nassoro Katuga; tunaona hafanyi Rejoinder anafanya maombi mapya
Hakimu; hajafanya hivyo
- Lugemeleza Nshala; Mshtakiwa anajiheshimu na kuheshimu utawala wa sheria. Mshtakiwa akiwa kizimbani anatakiwa hata pingu zifunguliwe.Hii ni common sense tu.. haya tulijifunza mwaka wa kwanza chuoni..Mshtakiwa hawezi hata kuwasiliana na mawakili wake kwa sababu ya kuzungukwa na maaskari
Update Saa Tatu Asubuhi: Lissu afikishwa mahakama ya Kisutu, awapunguia wananchi na wananchama waliokuja kufuatilia kesi hiyo, pia Godbless Lema, Boni Yai na viongozi wengine wa CHADEMA wafika kwenye mahakama ya Mkazi Kisutu
Update Saa Mbili Asubuhi: Foleni ndefu nje ya Mahakama ya Kisutu, wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusikiliza kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu.
======
Update Saa Moja Asubuhi: Jaji Mkuu Mstaafu Kenya, Willy mutunga, waanasiasa, baadhi ya waandishi wa habari na wananchi kutoka kenya washikiliwa uwanja wa Nyerere.
=====
Update Saa Moja Asubuhi: Hali ilivyo Mahakama ya Kisutu, polisi waonekana huku hali ikionekana kuwa shwari
=====
Leo ndio siku iliyokuwa inasubiriwa na wengi ambapo umma umeruhusiwa kwenda kusikiliza kesi ya Lissu na kujua yatakayojiri, ikiwepo na kumuona kwa wale ambao walinyimwa fursa hiyo walipokwenda kumuona.
Mara ya kwanza ilitokea virugu, waandishi, wananchama na wananchi wakapigwa na kupelekea kesi kuendeshwa mtandaoni.
Nini kitajiri siku ya leo? Muda utaamua!
Hivi ndivyo hali ilivyo nje ya Mahakama ya Kisutu muda huu saa 12 asubuhi Polisi wakionekana kuimarisha ulinzi.
===
Pumbavu la LumumbaNilidhani mtuhumiwa anaingia Mahakamani dakika chache kabla hakimu hajakaa. Yaani mtuhumiwa anapewa saa nzima kupiga kelele? Mahakama ijitatjmini uendeshaji wa mashauri na shughuli zake.
Japo naona ukakasi kutumia neno "UJINGA" lakini acha nilitumie tuuu! Kuendelea kumshikilia huyu LISU ni kumpa umaarufu asiostahili! Labda kama mamlaka za kipolisi na zinazomshitaki zimeamua kumpa umaarufu huo basi na ifahamike hivyo.
hakuna kesi halafu mtu anasota korokoroni hadi saa zingine eti anatishia kugomea kula msosi? sasa sijui anagomea njaa ya nani?🤣Hakuna kesi hapo zaidi ya blabla za kiccm tu.

Nilidhani mtuhumiwa anaingia Mahakamani dakika chache kabla hakimu hajakaa. Yaani mtuhumiwa anapewa saa nzima kupiga kelele? Mahakama ijitatjmini uendeshaji wa mashauri na shughuli zake.
Vp umebeba radi la kumtandika mtu!? Maana Hawa wahuni inabidi kutumia mbinu mbadala kuwakabili. Ifanywe kama wale wa mererani.Toka sumbawanga, ndo napita checkpoint iringa
Unajenga hofu kwa jamii ambayo inatumia haki ya kikatiba kujiandaa kwenda kisutu kusikiliza case ya kisu. Unachochea uvunjifu wa amani.Ulemavu anaweza kuupata MTU yeyote Mkuu acheni hizi tabia za kuhisi mpo salama
Mkuu sa autaki wenzio wapokee maelekezo kutoka juu?Yaani mtuhumiwa anapewa saa nzima kupiga kelele?