PreGE2025 Yaliyojiri Kesi ya Lissu: Mahakama imeahirisha shauri hadi 02/06/2025, mtuhumiwa amerejeshwa rumande

PreGE2025 Yaliyojiri Kesi ya Lissu: Mahakama imeahirisha shauri hadi 02/06/2025, mtuhumiwa amerejeshwa rumande

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwenye Shauri la kwanza la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Tundu Lissu wakitoa hoja kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Hata hivyo upande wa utetezi wametoa hoja wakiomba Mahakama kuwataka upande wa Jamhuri kueleza sababu zinazokwamisha upelelezi kukamilika huku wakitoa hoja kwa Mahakama wakiomba kesi hiyo iendelee kusikilizwa kwa utaratibu wa kawaida hata upelelezi ukiwa bado haujakamilika kama ilivyodaiwa.

Sanjari na hilo utetezi wamehoji sababu za Lissu kuzungukwa na ulinzi mkubwa wa askari wengi akiwa kizimbani mahakamani licha ya kuwa hajatiwa hatiani, ambapo wameiomba Mahakama askari hao watoke kizimbani ambapo anakuwa mshtakiwa wakidai kwamba mazingira hayo yanapoka uhuru wake.

Wakijibu hoja hizo upande wa Jamhuri, wamesema hawawezi kueleza kinachokwamisha upelelezi kukamilika kwa kuwa kwenye upelelezi kuna mambo mengi ikiwemo ya siri, ambapo wamedai kwamba hata Sheria haiwabani katika hilo.

Kuhusu suala la ulinzi wa askari waliomzinguka Lissu kizimbani, Jamhuri wameeleza kwamba Sheria haijaeleza mshtakiwa alindweje, lakini wametoa hoja kwamba ulinzi huo ni kwa faida ya mshtakiwa mwenywe, Mahakama pamoja na umma uliopo ndani ya ukumbi wa Mahakama.

Lakini Jamhuri wamesisitiza kwamba wanatamani ulinzi ungeimalishwa zaidi ya ilivyo na wanatamani kuendelea kushirikiana ili kuimarisha ulinzi.

Mahakama baada ya kusikiliza hoja za pande zote, imeelekeza upande wa Jamhuri tarehe ambayo kesi itakuja kutajwa tena wakamilishe upelelezi au kueleza hatua za mwisho za upelelezi kama walivyodai zimefikia hatua ipi.

Katika hoja ya pili kuhusu askari waliomzinguka Lissu kizimbani, amesema ni sahihi kabisa mashtaka anatakiwa kuwa huru anapokuwa kizimbani, hivyo ameelekeza Jamhuri kupitia vyombo vya usalama kufanya tathimini ya kina kuhusu suala la ulinzi kama kuna viashiria vya usalama dhidi ya mshtakiwa, ambapo ameelekeza kesi itakapotajwa tena Jamhuri waeleze kama kuna sababu kulingana na tathimini itakayokuwa imefanyika.

Aidha Mahakama imeelekeza kwamba Mshtakiwa ataendelea kuletwa mahakamani tofauti na Jamhuri walivyokuwa wameomba katika shauri hilo liendelee kusikilizwa kwa mfumo wa kimtandao. Hivyo Mahakama imesema kwamba Kesi hiyo itatajwa tena June 2, 2025.

Jopo la Mawakili wa Utetezi wameongozwa na Wakili Mpale Mpoki, Peter Kibatala, Dkt. Rugemeleza Nshala, Hekima Mwansipu, Jebra Kambore, Jeremiah Mtobesya, Kisabo, Dickson Matata pamoja na wengine huku jopo la Mawakili wa Jamhuri wakiwa watano.
 

​
Kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Mei 19.2025 kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Wakili Tundu Lissu ililetwa kwa ajili ya kutajwa, ambapo upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika

Jamhuri imesema mpaka sana shauri hilo linaendelea na uchunguzi chini ya mamlaka za Kipolisi, na kwamba kwakuwa upelelezi haujakamilika hivyo wanaiomba Mahakama kuhairisha kesi husika kwa siku 14 zaidi, jambo ambalo limeonekana kupingwa vikali na Mawakili wa utetezi

Jopo la Mawakili wa utetezi likiongozwa na Mawakili waandamizi Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala na Peter waliwasilisha maombi kadhaa Mahakamani hapo, ambapo miongoni mwake wameiomba Mahakama 'kulazimisha' upande wa Jamhuri ueleze nini hasa kinachokwamisha upelelezi kwa sababu mwanzo ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa ushahidi wote kuhusiana na shauri hilo upo mtandaoni

Jambo la pili walilowasilisha Mawakili wa utetezi Mahakamani hapo ni kwamba, hawafurahishwi namna ambavyo mteja wao anavyokuwa amezungukwa na maafisa wa Jeshi la Magereza (askari), ambapo wameishawishi Mahakama kutoa amri ya kuwaondoa askari wote 'wanaomlinda' Lissu ndani ya chumba cha Mahakama, kwakuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 Mahakama haimtambui mtuhumiwa kama 'mkosaji' na kwamba kitendo cha mteja wao kuzungukwa na askari wengi haikubaliki

Ukijibu hoja hizo, upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa licha ya kwamba Katiba imeeleza hivyo, lakini haijatoa maelekezo ya aina gani ya ulinzi inahitajika kwa mtuhumiwa pindi anapokuwa ndani ya chumba cha Mahakama, hivyo kuiomba Mahakama kutupilia mbali maombi hayo na kwamba ikiwezekana wanaomba ulinzi huo uongezwe

Mawakili hao wa serikali wameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa suala la ulinzi lina faida kwa mtuhumiwa mwenyewe, Mahakama na maafisa wa Mahakama kwa ujumla wake

Kuhusu suala la kueleza sababu inayopelekea upelelezi kutokamilika kwa wakati, Mawakili wa serikali wamejibu kuwa hakuna sehemu yoyote ya kisheria na Kikatiba inayowalazimisha kueleza hatua ya upelelezi iliyofikiwa, na kwamba mambo ya upelelezi sio ya kuwekewa hadharani, kikubwa kilichosisitizwa ni kwamba ndani ya muda waliiomba wa siku 14 wanaamini watakuwa wamefikia hatua nzuri ya upelelezi

Jambo lingine lililoibuka Mahakamani hapo ambalo limeletwa na upande wa utetezi, na ambalo halikupingwa na upande wa Jamhuri ni kuiomba Mahakama kutumia 'busara' zake kuondoa amri ya shauri hilo la uhaini kusikilizwa kwa njia ya mtandao badala yake mtuhumiwa awe anafikishwa Mahakamani moja kwa moja kama ilivyokuwa leo

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Mahakama imesisitiza Jamhuri kukamilisha upelelezi kwa wakati na tarehe ijayo Mahakama ipate mrejesho wa hatua iliyofikiwa, kuhusu suala la ulinzi wa Mahakama imesema mshtakiwa ni kweli anatakiwa kuwa huru akiwa kizimbani, hivyo tarehe ijayo Mahakama imeagiza vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kutosha kama hakuna sababu zozote za vitisho vya usalama wake basi mtuhumiwa awe huru peke yake akiwa kizimbani

Kuhusu suala la shauri hilo kuendelea kuendeshwa kwa njia ya mtandao, Mahakama imesema sheria inaipa Mahakama mamlaka ya kusikiliza au kuendesha shauri kwa njia itakayoona inafaa ikiwemo mtandao, na kwamba kwakuwa shauri hilo ni kubwa na linagusa hisia za wengi hivyo Mahakama imeona hoja za utetezi zina mashiko, hivyo Mahakama imeamuru tarehe ijayo shauri liendelee kwa mtuhumiwa kuletwa Mahakamani moja kwa moja kama ilivyokuwa leo

Baada ya kutoa maamuzi hayo, Mahakama imeahirisha shauri hilo kwa siku 14 hadi 02/06/2025 na mtuhumiwa amerejeshwa rumande

Ikumbukwe kuwa kesi hiyo ya uhaini kwa kawaida inasikilizwa kwa njia ya mtandao, leo imesikilizwa kwa njia ya kawaida kutokana na busara ya Mahakama kwakuwa mtuhumiwa anakabiliwa na shauri jingine Mahakamani hapo (shauri la uchochezi na kuchapisha taarifa za uwongo kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube)
======
​
Update Saa Nne Asubuhi: Kibatala aomba kesi ya Uhaini pia iendeshwe kwa njia ya mahakama ya wazi - Kwa kuwa kesi ya uhaini aliyopewa Tundu Lissu ina maslahi ya umma, mawakili wa utetezi wameomba mahakama kwamba mahakama itoe amri isiendeshwe kwa njia mtandao na kwamba itenganishe siku na kesi ya uchochezi na siku ya kesi ya uhaini na kesi zote mtuhumiwa aletwe mahakamani.

Update Saa Tatu Asubuhi: Lissu afikishwa mahakama ya Kisutu, awapunguia wananchi na wananchama waliokuja kufuatilia kesi hiyo, pia Godbless Lema, Boni Yai na viongozi wengine wa CHADEMA wafika kwenye mahakama ya Mkazi Kisutu


Update Saa Mbili Asubuhi: Foleni ndefu nje ya Mahakama ya Kisutu, wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusikiliza kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu.


======

Update Saa Moja Asubuhi: Jaji Mkuu Mstaafu Kenya, Willy mutunga, waanasiasa, baadhi ya waandishi wa habari na wananchi kutoka kenya washikiliwa uwanja wa Nyerere.

=====

Update Saa Moja Asubuhi: Hali ilivyo Mahakama ya Kisutu, polisi waonekana huku hali ikionekana kuwa shwari


=====

Leo ndio siku iliyokuwa inasubiriwa na wengi ambapo umma umeruhusiwa kwenda kusikiliza kesi ya Lissu na kujua yatakayojiri, ikiwepo na kumuona kwa wale ambao walinyimwa fursa hiyo walipokwenda kumuona.

Mara ya kwanza ilitokea virugu, waandishi, wananchama na wananchi wakapigwa na kupelekea kesi kuendeshwa mtandaoni.

Nini kitajiri siku ya leo? Muda utaamua!

Hivi ndivyo hali ilivyo nje ya Mahakama ya Kisutu muda huu saa 12 asubuhi Polisi wakionekana kuimarisha ulinzi.

===

ni vizuri wananchi kua wastahimilivu na wenye subra, uchunguzi ukamililika jambo hili litakua limefikia hatua nzur zaidi 🐒
 
Upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwenye Shauri la kwanza la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Tundu Lissu wakitoa hoja kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Hata hivyo upande wa utetezi wametoa hoja wakiomba Mahakama kuwataka upande wa Jamhuri kueleza sababu zinazokwamisha upelelezi kukamilika huku wakitoa hoja kwa Mahakama wakiomba kesi hiyo iendelee kusikilizwa kwa utaratibu wa kawaida hata upelelezi ukiwa bado haujakamilika kama ilivyodaiwa.

Sanjari na hilo utetezi wamehoji sababu za Lissu kuzungukwa na ulinzi mkubwa wa askari wengi akiwa kizimbani mahakamani licha ya kuwa hajatiwa hatiani, ambapo wameiomba Mahakama askari hao watoke kizimbani ambapo anakuwa mshtakiwa wakidai kwamba mazingira hayo yanapoka uhuru wake.

Wakijibu hoja hizo upande wa Jamhuri, wamesema hawawezi kueleza kinachokwamisha upelelezi kukamilika kwa kuwa kwenye upelelezi kuna mambo mengi ikiwemo ya siri, ambapo wamedai kwamba hata Sheria haiwabani katika hilo.

Kuhusu suala la ulinzi wa askari waliomzinguka Lissu kizimbani, Jamhuri wameeleza kwamba Sheria haijaeleza mshtakiwa alindweje, lakini wametoa hoja kwamba ulinzi huo ni kwa faida ya mshtakiwa mwenywe, Mahakama pamoja na umma uliopo ndani ya ukumbi wa Mahakama.

Lakini Jamhuri wamesisitiza kwamba wanatamani ulinzi ungeimalishwa zaidi ya ilivyo na wanatamani kuendelea kushirikiana ili kuimarisha ulinzi.

Mahakama baada ya kusikiliza hoja za pande zote, imeelekeza upande wa Jamhuri tarehe ambayo kesi itakuja kutajwa tena wakamilishe upelelezi au kueleza hatua za mwisho za upelelezi kama walivyodai zimefikia hatua ipi.

Katika hoja ya pili kuhusu askari waliomzinguka Lissu kizimbani, amesema ni sahihi kabisa mashtaka anatakiwa kuwa huru anapokuwa kizimbani, hivyo ameelekeza Jamhuri kupitia vyombo vya usalama kufanya tathimini ya kina kuhusu suala la ulinzi kama kuna viashiria vya usalama dhidi ya mshtakiwa, ambapo ameelekeza kesi itakapotajwa tena Jamhuri waeleze kama kuna sababu kulingana na tathimini itakayokuwa imefanyika.

Aidha Mahakama imeelekeza kwamba Mshtakiwa ataendelea kuletwa mahakamani tofauti na Jamhuri walivyokuwa wameomba katika shauri hilo liendelee kusikilizwa kwa mfumo wa kimtandao. Hivyo Mahakama imesema kwamba Kesi hiyo itatajwa tena June 2, 2025.

Jopo la Mawakili wa Utetezi wameongozwa na Wakili Mpale Mpoki, Peter Kibatala, Dkt. Rugemeleza Nshala, Hekima Mwansipu, Jebra Kambore, Jeremiah Mtobesya, Kisabo, Dickson Matata pamoja na wengine huku jopo la Mawakili wa Jamhuri wakiwa watano.
Jamhuri ya ujuha
 
Nimewaona hao wanaojiita G_55 mahakamani
Hawa waliasi No reform no election'

Nashangaa Bado wapo wanafuatilia mambo ya chadema

Naamini hii campaign ya G_55 ni mfu, hawa watu hawako organized watarudi Chadema tu
 
Back
Top Bottom