Yaliyojiri kesi ya Mbowe 01/02/2022. Luteni Denis Urio amaliza kutoa ushahidi wake. Shahidi wa 13 kuanza 04/02/2022

Dogo Urio kateseka sana. Kasahau mke, mtoto, baba, mama, paroko, makomando wenzake.

Kuna tatizo kubwa sana.

Bado anashikiliwa lkn anawaamini police?

Mie naamini angetumia mahakama kuwamwaga police na aseme mbele ya jaji kuwa nimekaririshwa na kulazimishwa tu.

Angekuwa poa sana
 
Malize mchezo tu yaishe
 
Sahihi na maisha yanaendelea
 
HII HAJAKUWA EDITED WALA HAINA UCHADEMA

Kidando: Shauri linakuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi kwa shahidi kuhojiwa na upande wa utetezi nasi tupo tayari

Jaji: Upande wa utetezi?

Kibatala: Nasi tupo tayari Mheshimiwa jaji

Kibatala: Shahidi habari za tangu Jana

Shahidi: Nzuri

Kibatala:Uliwahi kufahamishwa kuwa kuliwahi kufanyika kesi ndogo mbili ndani ya kesi kubwa ya msingi?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Adamu na Lingw'enya walisema wewe ulikuwa ni sehemu ya watu waliokamatwa, ni sahihi?

Soma zaidi: Kibatala amng’ang’ania Luteni Urio kesi ya kina Mbowe

Shahidi: Nasikia kutoka kwako.

Kibatala: Uliwahi kukutana na mawakili wa Serikali ikiwemo Mr Kidando kabla ya kuja kutoa ushahidi mahakamani hapa?

Shahidi: Kwa maelekezo niliambiwa nieenda kuripoti kwa DCI ndio nikaletwa hapa.

Kibatala: Kwa maelekezo yako hujasema kama uliwahi kukamatwa na maafisa wa Polisi hasa Jumanne Malangahe na Goodluck?

Shahidi: Sasa nitasemaje wakati sijakamatwa?

Kibalata: Relax shahidi

Kibatala: Katika ushahidi wako hujawahi kusema kuwa hujawahi kutifikishwa kituo cha Polisi cha Tazara tarehe 8 au 9 ya mwezi wa Saba, mwaka 2020?

Shahidi: Sijawahi kufikishwa

Kibatala: Pia hujawahi kusema Kama ulifikishwa kituo cha Polisi Mbweni katika tarehe hiyo.

Shahidi: Sijawahi kufikishwa kituo chochote cha Polisi, narudia tena mimi sijawahi kufika kituo chochote cha Polisi Mbweni

Kibatala: Wewe una ugomvi na Adamoo na? Lingw'enya?

Shahadi: Sijawahi kuwa na ugomvi nao.

Shahidi: Narudia tena sijawahi kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni, mbona unaniwekea maneno mdomoni?

Kibatala: Shahidi usikasirike

Kibataka: Unafahamu sababu ya mimi kukuuuliza maswali kuhusu wapi unasali na paroko wako ni nani?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Sasa baada ya kukamatwa Adamo na Lingw'enya na kuteswa walipohojiwa walikutaja kuwa wewe ndio uliwaunganisha kwa Mbowe na wewe ulikamatwa ni sahihi?

Shahidi: Sijawahi kukamatwa

Kibatala: Katika ushahidi wako ulimtaja komando aitwaye Gabriel Mhina?

Shahidi: Sifahamu

Kibataka: Una ugomvi na watu niliyokutajia?

Shahidi: Sina ugomvi nao

Kibatala: Afande Kingai aliwahi kukuambia kuwa kuna komando wengine walikamatwa?

Shahidi: Hajawahi kuniambia

Kibatala: Ex- Komando Halid alimuuliza Bwire nani aliyekuunganisha katika kazi hii ya ulinzi? Akasema ni wewe ni sahihi?

Shahidi: Halid ni nani? Mimi simfahamu Halid na wala hapa katika ushahidi wangu sijamtaja

Kibatala: Huyo halidi pia, baada ya kukutafuta kwenye mtandao wa Facebook, ulimwambia utamuunganisha na kazi ya ulinzi migodini, ni sahihi?

Shahadi: Simfahamu Halidi wala sina Access huko migodini

Kibatala: Unamfahamu baba yako mdogo mzee John Urio?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu mke wako ndio aliyefanya juhudi za kuitoa gari yako Rav4 rangi ya silver pale kwenye parking na kwenda kuipark Kihonda ni Sahihi? Kwa sababu wewe mpaka sasa upo chini ya ulinzi, ni sahihi?

Shahidi: Sio sahihi? Gari haijawahi kuzuiliwa na hata nakuja hapa kutoa ushahidi gari nilipaki.

Kibatala:Tukitaka kuangalia upo kwenye active duties kwenye Military Service tunatakiwa kuangalia nyaraka zipi?

Shahidi: Ni kuangalia identity card na kuhakiki kwa mwajiri wake.

Kibatala:Ni kweli ili kudhibitisha kuwa wewe hujafukuzwa kazi unatakiwa kuangalia duties Roster?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Kama tunafikiria kuiomba ahirisho kwa Mahakama kwa ajili ya kukupa nafasi ya kufuatilia nyaraka ya udhibitisho kuwa wewe upo kazini, unaweza kufahamu mchakato huo utachukua siku ngapi? Ili upate nyaraka hiyo?

Shahidi: Sijui itachukua muda gani.

Kibatala: Ni sahihi mtoto wako mdogo Jackson wakati anazaliwa wewe ulikuwa mafichoni umefichwa?

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla ananyanyuka na kumueleza Jaji kuwa suala la mtoto, lisiwekwa kwenye rekodi kwa sababu hajalitolea ushahidi.

Jaji: Sawa

Shahidi: Hili swali nimeshakujibu wakili halafu wewe ni wakili msomi....Sasa sitaki uniulize tena? Sawa? Wewe ni wakili msomi? Alaah

Mahakama: Kichekoo hahaha hahaha hahaha

Kibatala: Shahidi hebu Relax basi

Shahidi: Mimi nimelax

Kibatala: Ni kweli shahidi hata mama yako mzazi ilibidi aje kukuona ukiwa kizuizini?

Shahidi: Narudia tena sijawahi kuwekwa kizuizini.

Kibatala: Ni kweli au sio kweli kwa kuwa upo kizuizini kwa sasa unasindikizwa na maofisa usalama wenye silaha?

Shahidi: Kwanza naomba uondoe neno kizuizi kwa sababu unanichafulia...mimi sijawahi kuletwa na maofisa usalama wenye silaha.


Shahidi: Mimi nakuja na mawakili wangu (wa upande wa mashtaka) ambao hunipitia hotelini na magari yao.

Kibatala: Kwa magari ya Serikali? Usinitajie namba zake kwa sababu ni masuala ya kiusalama.

Shahidi: Labda unipe task nikayakague

Kibataka: Hivi hizo dhana mbili zinaoana kweli?

Shahidi: Dhana zipi?

Soma zaidi:Luteni Urio: Sikuona umuhimu kurekodi mazungumzo yangu na Mbowe

Kibatala: Ulisema uliripoti kwa DCI ndio ukaletwa hapa mahakamani na leo umetueleza kuwa unapitiwa na mawakili wako kuletwa hapa mahakamani.

Shahidi: Hujanielewa ...siku ya kwanza nililipoti kwa DCI na baada ya hapo nikawa nachukuliwa na mawakili wa Serikali kuletwa mahakamani.

Kibatala: Shahidi Ndio utaratibu wako wa kila siku unapitiwa na mawakili wako?

Shahidi: Ndio wenyeji wangu.

Kibatala: Okay

Shahidi: Karibu

Kibatala: Unafahamu DCI, IGP na wengine wamehamia Dodoma?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Sasa unafahamu kwa sababu ofisi mama ya DCI imehamia Dodoma?.

Shahidi: Siwezi kuzungumzia ofisi ya DCI

Kibataka: Shahidi unafahamu kitu kiitwacho Civico?

Shahidi Nafahamu.

Kibatala: Cimico ni Civic and Military Coordination?

Shahidi: Ndio,

Kibatala: Hii maana yake ni mahusiano ya kubadilishana taarifa kati ya taasisi za Jeshi na jamii.

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Unafahamu Presence Patrol?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Shahidi ni sahihi zimeshawahi kufanyika Presence Patrol hapa Tanzania inapofanyika uchaguzi au kunapotokea matukio tata?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Shahidi limetoka tishio la kuripua madaraja makubwa hapa nchini, ni kweli Jeshi letu haliwezi kufanya Presence Patrol?

Shahidi: Sijaelewa unaenda wapi.

Kibatala: Nisikilize swali langu.

Shahidi: Nimelielewa swali.

Kibatala: Shahidi nakuuliza spry ya sumu, je Uliwahi kuiongelea katika ushahidi wako?

Shahidi: Sijasema...halafu usinilishe maneno mdomo..vipi wewe rafiki yangu bwanaa...hebu relax

Kibatala: Una mfahamu Bwire.

Shahidi: Namfahamu.

Kibatala: Unafahamu jukumu la Bwire lilikuwa ni kwenda kumlinda Tundu Lissu?

Shahidi: Hata raisi mwenyewe halindwi na Komando.

Kibatala: Unafahamu Tundu Lissu Kama mgombea urais alitaka mlinzi Maalum kwa kuwa alishashambuliwa na risasi?

Shahidi: Kila mgombea anapewa mlinzi

Kibatala: Unafahamu mgombea urais anapewa walinzi wangapi?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi kwenye viwanja vya bunge ?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu hadi leo Jeshi la Polisi halijakama mtu hata mmoja, alihusika na kumshambulia Lissu.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni kosa mtu kujiimalisha kwa kuwa na walinzi wake?

Shahidi: Sio kosa

Kibatala: Unafahamu Ben Sanane alikuwa ni msaidizi binafsi wa Mbowe amepotea na hajajulika alipo hadi leo?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Kwa mujibu wa kanuni za Jeshi na miongozo ya jeshi,ofisa wa Jeshi anaruhusiwa kuwa na mahusiano na kiongozi wa chama cha upinzani? Ni kosa au sio kweli?

Shahidi: Si kosa kama ni mahusiano ya Kawaida lakini sio ya siasa.

Kibatala: Ulimfahamu ama hufahamu ...moja wapo ya majukumu ya Bwire na Lingw'enya ni kumsindikiza Mbowe kwenye mikutano yake ya kisiasa ikiwemo ule uliofanyika ukumbi wa kanisa Katoliki.

Shahidi: Sifahamu, nachojua walienda kutekeleza uhalifu.

Kibatala: Unafahamu Julai 26, 2020 Adamoo na Lingw'enya siku hiyo walipanda magari ya Chadema yenye nembo za M4C kwenda kwenye mikutano?

Shahidi: Walishawishiwa kuingia katika uhalifu na kukataa mawasiliano na mimi.

Kibatala: Kabla ya kukataa mawasiliano baina ya Adamoo na Lingw'enya, hukuwauliza?

Shahidi: Waliniambia wanataka kuajiliwa.

Soma zaidi: Shahidi muhimu kuhojiwa siku ya tatu kesi ya kina Mbowe

Kibatala: Big answer

Shahidi: Ndio ulikuwa unataka hilo.

Mahakama: Kicheko.

Kibatala: Shahidi ulipoongea na Mbowe alijicommit akisema anapanga kushiriki uchaguzi?

Shahidi: Alisema chama changu kimejipanga kuchukua dola

Shahidi: Alisema chama changu kimejipanga kuchukua dola kwa njia yoyote.

Kibatala: Unafahamu chama cha Chadema kilisimamisha wagombea katika ngazi zote?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu alifanya kampeni?

Shahidi: Sikufuatilia sana.

Kibatala: Hata kama ulifuatilia kwa mbali ulijua?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu zile pesa ulizotumiwa na Mbowe zilikuwa ni za Mbowe au za chama?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu jukumu la kutafuta walinzi ni jukumu lililoidhinishwa na chama?

Shahidi: Sifahamu.

Soma zaidi:Luteni Urio asoma mawasiliano yake na Mbowe mahakamani

Kibatala: Mtu alishtakiwa discharge ana mipaka ya kufanya kazi?

Shahidi: Ili mradi afuate sheria.

Kibatala: Unafahamu hata kina Diamond Platinum ana bordguard?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Shahidi naomba utusaidie kwanini ulichagua kukutana na Moses Lijenje eneo la Morogoro na sio sehemu nyingine?

Shahidi: Kwa sababu ndio center

Kibatala: Center ya Nini?

Shahidi: kwa sababu ndio sehemu ya karibu.

Kibatala: Uliwahi kufahamu Mbowe alisafiri nje ya nchi?



Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unamfahamu Godless Lema?

Shahidi: Namsikia

Kibatala: Unafahamu Lema anaishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya maisha ya usalama wake?

Shahidi: Sijui Kama anaiishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya maisha yake.

Kibatala: Unafahamu Kama Tundu Lissu anaishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya usalama wa maisha yake?

Shahidi: Sijui kama ni uhamishoni au amekwenda kitalii.

Soma zaidi: Urio aeleza alivyomtafutia Mbowe makomandoo na kuahidiwa cheo

Kibatala: Unafahamu kama hawa vijana wasingekamatwa, Lissu asingeondoka hapa nchini?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kama hawa vijana wasingekamatwa, Lema asingeondoka hapa nchini?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapa...yangu ni hayo tu.

Kibatala amemaliza kumhoji Luteni Urio na sasa upande wa mashtaka wanatakiwa kumfanyia re- examination ( mawakili wa Serikali kumuuliza shahidi kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusiana na ushahidi alioutoa wakati anahojiwa na mawakili wa upande wa utetezi).

Wakili Chavula: Hebu ifafanulie mahakama ni Kwanini ulimwambia Freeman Mbowe atumie wakala au msaidizi wake kutuma pesa bada ya kutumia namba yake ini salama zaidi

Shahidi: Nilimwambia atumie Wakala au msaidizi wake ili niweze kuwini Trust.

Wakili: Kuna swali uliulizwa kuhusu kukamatwa kwa kina Bwire ukasema hukushangaa ulivyosikia wamekamatwa.

Shahidi: Sikushangaa kwa sababu walinipa taarifa wakiwa wameshapanga.

Wakili: Licha ya wewe kuwa na cheo na kumwambia Freeman Mbowe kuwa huna cheo hebu ifafanulie mahakama kwanini ulisema jibu hilo wewe ulikuwa mkweli.

Shahidi: Kwa mara ya kwanza ndio nakutana na Freeman Mbowe anataka kujua cheo changu nilimjibu hivyo kwa ajili ya usalama.

Wakili: Ulisikika uliieleza mahakama ukisema uliwaambia washtakiwa wakafanye kazi ya ulinzi na kuambatana nae katika kuchukua dola ulikuwa unamaanisha nini

Shahidi: Dhumuni kubwa la Mbowe kuwahitaji hao watu ilikuwa ni kwa ajili ya kukata miti, kuchoma vituo vya mafuta pamoja na kumdhuru viongozi.

Wakili Chavula:Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.



Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna shahidi mwingine kwa leo tunaomba ahirisho la siku mbili Shahidi tuliyekuwa tunategemea hadi jana tulikuwa hatujampata alikuwa kasafiri.

Katika mazingira hayo hata kama tutakuwa hatujampata tutaendelea na Shahidi mwingine.

Ni hayo tu.

Wakili Kibatala: Bila kuwakosea wenzetu hatujaona sababu ya kuahirisha katika mashahidi kadhaa waliotajwa hata kibinadamu yenyewe tunaomba wenzetu kesho walete Shahidi kwa kuwa tumebrek mapema muda wa kumuandaa upo.

Wakili Kidando: Tumewasikia wenzetu kuita mashahidi hata kama ni wengi kiasi gani inacost kusubiri na wengine hawapo Dar es Salaam.

Jaji: Tujikite hiyo hoja ya siku mbili hao wamesema kwa nini iwe hadi Ijumaa.
Jifunze namna ya kuanzisha thread kijana naona threads zako mods wanazifuta kwakuwa unaandika ujinga ujinga mwingi.
ACHA UMBEYA
 
Yes. Kibatala hakutaka kuingia sana ndani. Labda sheria hairuhusu kuhoji sana private issues. Lakini kaweka foundation ambayo anaweza baadaye akaleta ushahidi wa kumbana zaidi Urio.
Itakuwa lini sasa hapo maana Urio kesha maliza
 
Huyu shahidi anatupa tabu sana akina sisi tusokuwa na uelewa wowote....yaan kuwa Freemn alitaka kuchukua nchi kwa kukata miti 🀭🀭🀭 na hiyo ndo huitwa terrorism..kheee! Haya mambo yangefanyw kule vijijn na raia wakigombea shamba ingetia sense. Lkn kwa wakubwa kabsa wa nchi aaah cyooo!! Ilitupasa hata ss kuwa tunatawaliwa,tena na waarabu mizee ya kutufunga minyororoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚labda tungetia akil kichwan
 
Kama kawaida ya watanzania

Ukiishiwa hoja unabakia kulilia kuchukiwa.

Nani ana chuki na wakili wa upande wa utetezi.

Anyways ngoja nijikalie kimya hapa maana kuna watu hawataki kukosolewa .

Hakuna mtu perfect kila mtu anakosea hata mimi nakosea.

So unapokosolewa angalia hoja inayotumika kukukosoa kuifanyia kazi.
 
Sasa ulitaka Alie.?
wanachojaribu upande wa utetezi ni kupindisha ukweli.
Lakini mbowe Alisha kosea
Hujui sheria mkuu. Urio kachemka vibaya mno, mchongo umeonekan wazi.

Halafu hao mawakili wa serikali ni hewa kabsa
 
Shahidi anaenda kuchongwa aje zamu yake kulikoroga zaidi.
 
Wakili wa Serikali: Ulionyeshwa Hapa Maelezo ambayo Uliyaandika Ukiwa Polisi, Kuna Maeneo ambayo katika Maelezo Umezungumza Kifupi ila hapa Umezungumza Kirefu, Kwanini imetokea.

Shahidi: Kwa Sababu aliyekuwa anaandika siyo Maneno Yote alikuwa anaandika hapa Naongea Sababu nipo Free, Kwa hiyo siyo Maneno Yote Kaandika Mle.

Mawakili wa Serikali Wanateta Kwa Chini chini

Maswali Yamesimama hapa kwa muda

Mawakili wa kiserikali Wanamuomba Jaji Samahani Kidogo Asubirie, wanajadiliana.

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji sisi hatuna Maswali sanaaaa, Nafikiri Yanatosha. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Jibu la mwisho la shahidi wa 12 wa Jamhuri. Luteni Denis Urio leo wakati
wa Re-examination akifanyiwa n wakili
wa serikali. Jibu limefanya maswali yakaishia hapo. Maana yake ni kwamba, Urio alitoa maelezo yake ya onyo akiwa chini ya ulinzi. Leo alikuwa free. kashikiliwa mateka?


WS: Ulionyeshwa Hapa Maelezo
ambayo Uliyaandika Ukiwa Polisi, Kuna Maeneo ambayo katika Maelezo Umezungumza Kifupi ila hapa Umezungumza Kirefu, Kwanini imetokea

Shahidi: Kwa Sababu aliyekuwa anaandika siyo Maneno Yote alikuwa anaandika hapa Naongea Sababu nipo Free, Kwa hiyo siyo Maneno Yote
Kaandika Mle.
 
Huyu Shahidi wa leo ndio alikuwa Shahidi Tegemeo Namba 1 wa Jamuhuri maana Kwa mujibu wa hii kesi yeye ndio alianzish hii kesi lakini kajichanganya sana kwasababu kalishwa

Shahidi wa 12 wa Jamhuri, ambaye
ndiye mtoa taarifa, Luteni Denis Urio
anasema wakati anatoa taarifa kwa DCI
alimueleza Mbowe alikula njama za
ugaidi kati ya 1-10 July 2020 lakini hati
ya mashtaka wameandika matukio hayo
yalitokea 1 May 2020. Hii kesi ina ujinga
na uonevu sana.

Kibatala: Wakati Unatoa Taarifa
ulimwambia Kuwa Matukio yalitokea
tarehe ngapi ya Wewe na Mbowe
Shahidi: Kati ya Tarehe 1 July mpaka
Tarehe 10

Kibatala: Sasa Kwenye Hati Ya Mashtaka
Wenzetu wameandika Tarehe 1 May,
hujamwambia Wewe

Shahidi: Sijasema hivyo mimi
 
ina maana Urio ni mateka aliyeteseka siku nyingi... wameona mengi yatafichuka heri waustiri utupu wao japo kwa manyasi!!
 
Uzi umeingiliwa na vijana wasio na ustarabu,ni mwendo wa lugha mbovu tu
Hao si suala la ustaarabu Tena. Ni wajinga ambao wameadvance na kuwa wapumbavu wa viwango vya juu.

It's aju nini na mtu km Comte, sijui Elitwege, mwingine anajiita mjinga mimi lkn hajui tyari ni mpumbavu.

Ni majitu tu ya hovyo hovyo yasiyo na tija kwa jamii wala familia zao.
 
"Hapa naongea niko free"

Halafu akiambiwa aliteswa kituo cha polisi ni kina Adamoo anakataa, sasa kitu gani kilichomfanya asiwe free wakati anatoa maelezo yake mwanzoya kama sio alitishwa?

Ameshaambiwa truth shall set him free, lakini namuona bado anajipotezea muda tu wa kuwa huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…