Yaliyojiri kesi ya Mbowe 01/02/2022. Luteni Denis Urio amaliza kutoa ushahidi wake. Shahidi wa 13 kuanza 04/02/2022

Yaliyojiri kesi ya Mbowe 01/02/2022. Luteni Denis Urio amaliza kutoa ushahidi wake. Shahidi wa 13 kuanza 04/02/2022

Urio anajua kujibu maswali. Na anajiamini😁😁
 
Ikupendeze Mh. SULEY koram yetu imekamilika na tuko tayari kuendelea lakini pia tumuombe shahidi aache kucheka mahakamani maana hatuelewi ni kicheko cha furaha au huzuni
... mwezi nchanga yule! Komandoo unachekacheka mbele ya wanaume sio! Funny enough hapakuwa hata na tukio la kuchekesha; ukumbi mzima ulibaki kumshangaa!
 
Ngoja tusikilize maswali yasiyokuwa na tija toka kwa mawakili wa utetezi.
 
Huyu luteni sio mjinga kiasi hicho, na nijuavyo mimi kati ya askari wote askari jeshi ni wako humbe sana tena sana ukizingatia huyu ambaye amefika mpaka rank za juu kiasi hicho sidhani kwamba jeshi lilimuona hamnazo likaruhusu afike mbali kiasi hiko.

Najaribu kufikiria hatma yake baada ya hii kesi, kwenye jamii, kwenye familia yake na kwao huko, kwenye utumishi wake jeshini, sijui itakuwaje kwa kweli lakini yupo kwenye nyakati ngumu mno ndio maana hata anacheka pasipo chekesha, nadhani pia ule ukakamavu wa kijeshi ndio umemfanya astahimili kusimama mpaka leo hii kuendelea kutoa ushahidi.

Ila jamuhuri na washauri tena, mwungwana akivuliwa nguo huchutama!
Kuteleza sio kuanguka semeni tu neno rahisi SORRY.
 
URIO
1. Hakwenda wa DCI - na ndiyo maana anakwepa kusema tarehe na muda
2. Kingai, DCI na URIO walifanya kikao kwa DCI, cha ajabu hakuna tarehe ya kikao hicho ambacho Mahakama imefahamishwa ili kujiridhisha.
3. URIO anajichanganya kuhusu miamala ya anayodai alitumiwa na Mbowe, sms pamoja na hiyo Telegraph - hazijaonyesha moja kwa moja ni Mbowe ndiye aliyekuwa anatuma na kuchati ya URIO.
4. Katika Ushahidi wote URIO anaonekana yeye ndiye mwanzilishi wa mada zote - vi sms vingi kavianzisha yeye kwa mfano - kaka ongeza fungu, kaka mtu tatu ana nne ni muhimu etc
5. URIO pamoja na kuwa ni Ofisa wa JWTZ, aliona ni muhimu sana kumtafuta DCI ali ampe riporti ya uhalifu wa Ugaidi badala ya kwanza kuliport kwa line commander wake - kutokana na UZITO wa jambo lenyewe - UGAIDI - na baada ya ktuoa report ndipo JWTZ iwasiliane na Police - DCI (Vyote ni vyombo vya usalama)
6. URIO kwa mara kadhaa ameiambia mahakama kwamba kina Adamoo si Magaidi, ni watu wazuri na alikuwa anawatafutia kazi ya Ulinzi - hadi wanatoka makwao walijua ni ULINZI na si UGAIDI.
7. URIO ameshindwa kuthibitisha UGAIDI wa Mbowe kwa kila kipengele - hii ni pamoja na kula njama wakiwa wawili - Mbowe na URIO - kwa sababu ni watu wawili tu wa kuthibitha hayo ni URIO ila kashindwa kabisa.
8. URIO ameshindwa kutoa mtiririko wa ushahidi wake, ni ushahidi wa kujichanganya changanya bila kuwa na uhakika wa anayoyatolea ushahidi Mahakamani.
9. URIO kasema hajui Bastola, Vifaa ya ulipuzi vyovyote ambavyo Mbowe angetumia - kifupi ni shahidi mzembe, yawezekana ana matatizo ya akili - mawakili wa utetezi waombe kibali akapimwe akili ili mahakama ijuridhishe ukizingatia huu ni mwezi mchanga na kicheko chake hapo mahakamani jana.
10. Mahakama itupilie mbali ushahidi huu, URIO kashindwa kui convice mahakama pasi na shaka kwamba Mbowe alitaka kutenda UGAIDi
 
Huyu luteni sio mjinga kiasi hicho, na nijuavyo mimi kati ya askari wote askari jeshi ni wako humbe sana tena sana ukizingatia huyu ambaye amefika mpaka rank za juu kiasi hicho sidhani kwamba jeshi lilimuona hamnazo likaruhusu afike mbali kiasi hiko.

Najaribu kufikiria hatma yake baada ya hii kesi, kwenye jamii, kwenye familia yake na kwao huko, kwenye utumishi wake jeshini, sijui itakuwaje kwa kweli lakini yupo kwenye nyakati ngumu mno ndio maana hata anacheka pasipo chekesha, nadhani pia ule ukakamavu wa kijeshi ndio umemfanya astahimili kusimama mpaka leo hii kuendelea kutoa ushahidi.

Ila jamuhuri na washauri tena, mwungwana akivuliwa nguo huchutama!
Kuteleza sio kuanguka semeni tu neno rahisi SORRY.
Ubarikiwe kwa maneno yako.
 
Mara tu nimekuwa mmoja wa wafuatiliaji wa kesi hii kupitia ninyi. Tunaomba kesi iendeshwe kwa haki na kila muhusika apate anachostahili.
 
Asante,tupo tayari

Naona shahidi ameanza kukasirika baada ya kukumbuka kipigo kutoka selo za Tazara ,japo anakataa kwamba hajawahi kuteswa[emoji28],Kibatala endelea tafadhali.
 
Back
Top Bottom