Wakili wa Serikali: Ulionyeshwa Hapa Maelezo ambayo Uliyaandika Ukiwa Polisi, Kuna Maeneo ambayo katika Maelezo Umezungumza Kifupi ila hapa Umezungumza Kirefu, Kwanini imetokea.
Shahidi: Kwa Sababu aliyekuwa anaandika siyo Maneno Yote alikuwa anaandika hapa Naongea Sababu nipo Free, Kwa hiyo siyo Maneno Yote Kaandika Mle.
Mawakili wa Serikali Wanateta Kwa Chini chini
Maswali Yamesimama hapa kwa muda
Mawakili wa kiserikali Wanamuomba Jaji Samahani Kidogo Asubirie, wanajadiliana.
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji sisi hatuna Maswali sanaaaa, Nafikiri Yanatosha. 😀😀😀😀
updatea zingine zinaeleza tofauti
Kibatala amemaliza kumhoji Luteni Urio na sasa upande wa mashtaka wanatakiwa kumfanyia re- examination ( mawakili wa Serikali kumuuliza shahidi kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusiana na ushahidi alioutoa wakati anahojiwa na mawakili wa upande wa utetezi).
Wakili Chavula: Hebu ifafanulie mahakama ni Kwanini ulimwambia Freeman Mbowe atumie wakala au msaidizi wake kutuma pesa bada ya kutumia namba yake ini salama zaidi
Shahidi: Nilimwambia atumie Wakala au msaidizi wake ili niweze kuwini Trust.
Wakili: Kuna swali uliulizwa kuhusu kukamatwa kwa kina Bwire ukasema hukushangaa ulivyosikia wamekamatwa.
Shahidi: Sikushangaa kwa sababu walinipa taarifa wakiwa wameshapanga.
Wakili: Licha ya wewe kuwa na cheo na kumwambia Freeman Mbowe kuwa huna cheo hebu ifafanulie mahakama kwanini ulisema jibu hilo wewe ulikuwa mkweli.
Shahidi: Kwa mara ya kwanza ndio nakutana na Freeman Mbowe anataka kujua cheo changu nilimjibu hivyo kwa ajili ya usalama.
Wakili: Ulisikika uliieleza mahakama ukisema uliwaambia washtakiwa wakafanye kazi ya ulinzi na kuambatana nae katika kuchukua dola ulikuwa unamaanisha nini
Shahidi: Dhumuni kubwa la Mbowe kuwahitaji hao watu ilikuwa ni kwa ajili ya kukata miti, kuchoma vituo vya mafuta pamoja na kumdhuru viongozi.
Wakili Chavula:Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.