Yaliyojiri kesi ya Mbowe 24/01/2022: Shahidi wa 11, H4347 Goodluck amaliza ushahidi wake. Shahidi wa 12 kuendelea tarehe 26/01/2022

Yaliyojiri kesi ya Mbowe 24/01/2022: Shahidi wa 11, H4347 Goodluck amaliza ushahidi wake. Shahidi wa 12 kuendelea tarehe 26/01/2022

Shahidi yupo jijini Dar tangu J2, sema kila akimezeshwa desa anatema halikai mukichwa...... ndo kesho anaendelea na kumeza madesa! uongo wa kupambana na kina Kibatala ni kazi Ngumu mno, najua mashahidi washashtuana ila watafanyeje ikiwa maboss ndo washapika ngoma na imetoka mbichi, kutwa kujikanyaga kama migambo!!!
Unasema kama unauhakika hivi- soma hiyo
1643037355912.png
 
Leo hii nimekuwepo mahakamani kusikiliza muenendo wa kesi inayo mhusu mh Mbowe.

Hakika nimepatwa na uzuni mkubwa sana mara baada ya kushuhudia umati wa kina mama waliojazana mahakamani kumuona na kumjulia hali mh Mbowe.

Wakati wa kutoka mahakamani umati huo wa watanzania wapenda amani na umoja walimwimbia wimbo mh Mbowe hadi nikajisikia huruma sana na kupata ujasili kuwa ukiwa kuongozi wa watu lazima uwe na roho ngumu kama chuma.
 
inatakiwa yaitishwe maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima..na wananchi kwa wingi wao washiriki..Tofauti na hapo huu ni unafiki kama unafiki mwingine
 
... falme za kuzimu tabu tupu. Shetani husimika vibaraka wake pia.
 
Kwahiyo siku zote hizo hukuwahi kwenda kumuunga mkono mwenyekiti unapiga tarataraa tu hapa JF.

Kama ulikua huna nauli si ungewaambia tu makamanda wenzako wapitishe mchango.
 
inatakiwa yaitishwe maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima..na wananchi kwa wingi wao washiriki..Tofauti na hapo huu ni unafiki kama unafiki mwingine
Wapenzi wa Mbowe sio wajinga kama wewe wanaotaka kudaka Risasi kwa mikono.

Ra

Mh Tundu Lissu Tar 30 Oct 2020 angekuwa na mawazo ya kijinga kama hayo tusingekuwa naye leo.
Angejifanya mjanja kukomaa ma wachawi wa siku zile angekuwa shujaa wa kijinga. Leo mchawi hayupo.
 
Labda ni kipofu, umati wa hawa akina mama na magauni yao huuoni [emoji28][emoji28][emoji28] View attachment 2094341
Chadema mnajitahidi sana kumtoa mwenyekiti kabla ya hukumu.

Kama hana hatia na mnao uhakika,mbona mnatafuta huruma mitandaoni?

Pia kesi inaelekea ukingoni,je kwa nini msiache hukumu itoke?

Hao kina dada wa kutoka BAWACHA ni moja ya mikakati mahsusi iliyoandaliwa na ofisi kule KINONDONI - UFIPA.

Ni sawa na wale mliowakusanywa kule Arusha kutokea Sanawari na kupewa posho ya 15,000/=@
Na usafiri
Kisha wakakusanyika kumzomea na kushangilia kwenye mahakama ya RAMS Siku ya kesi ya Sabaya ilipotajwa mara ya kwanza.

Wamekusanywa na wakakusanyika,nauli ya kurudi pamoja na posho ya Lunch, wanayo vibindoni mwao.

Tusiyumbishe mahakama kila uchao,mnakuja na kituko kipya Mara keki,Mara wazungu mahakamani,mara mapambio na leo BAWACHA.
 
inatakiwa yaitishwe maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima..na wananchi kwa wingi wao washiriki..Tofauti na hapo huu ni unafiki kama unafiki mwingine
Mkuu mbona unasema wananchi washiriki kwa wingi WAO?

Wewe mbona unajitoa?Huoni kuwa zinahitajika pia nguvu zako kulifanikisha hili?
 
Back
Top Bottom