Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 3, 2021: Shahidi Upande wa Mashitaka ashindwa kutokea Mahakamani, kesi yaahirishwa hadi Novemba 4, 2021

Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 3, 2021: Shahidi Upande wa Mashitaka ashindwa kutokea Mahakamani, kesi yaahirishwa hadi Novemba 4, 2021

Ujumbe uliotaka kufikishwa ni upi kwa maoni yako?
Alitaka kunyooka kwamba ushahidi wa sabaya ni wa kunyooka ila wa Mbowe ni wa kuunga unga na sote tunaona ushahidi wa Mbowe, huyu ndugu alisema kinyume chake.. ndivyo nilivyo muelewa.. kwa maoni yangu...
 
ila wafuasi wa mbowe mnaroga sana![emoji1787].
nashauri idadi ya wanao ingia kwenye ukumbi wa mahakama ipunguzwe au wasichiwe vilivyo.
washirikina kibao wanaingia, nimewashuhudia kwa macho yangu.
 
Mungu yupo upande wa chadema ndio maana Mara nyingi upande wa mashahidi wa upande wa pili huwa wanaumwa kwa hofu ya kutunga ushahidi wa uongo Kama mbowe hakuwahi kumiliki line ya tigo
Ivi walio moshi wameshindwa kabisa kumpata yule muuza mbege
 
Tunamwamini Mungu kutenda jambo la ajabu katika kesi hii asante Mkuu Replica kutuunganisha na Mahakama.

Jamii Forum imekuwa mahali salama kwenye usiri kuliko Tigo
Na Kwa nini tusiwashauri JF waanzishe kampuni yao ya simu ili sote tulioko huku Tigo tuhamie mahala salama!
 
Mkuu replica nikupongeze kwa kazi nzuri ya moyo wa kujitolea kutuanikia kila kinachoendelea hapo mahakamani hakika unafanya kazi kubwa na ngumu kwa watanzania ambayo inastahili mshahara mkubwa kuliko ule wanaolipwa wale mazuzu kule uzuzuni shukrani pia kwa mkuu erythrocyte,G day!!!
Naunga mkono. Hasa hilo la mazuzu kule mjengoni. Ni hasara tupu kwa nchi.
 
Wana CDM wengi watahama sana......kwa ujinga huu
 
Baada ya jana kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani. Jana kesi ilisikiliza shahidi ambae ni mwanasheria wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo. Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=========

Jaji ameingia..

Kesi inatajwa..

Robert Kidando anatambulisha Jopo la mawakili wa serikali Peter Kibatala anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi Jaji anawaita washtakiwa na wote wanaitika kwa kusimama

Wakili wa Serikali: Shauri lina kuja kwa ajili ya Kusikilizwa. Mpaka Jana Jioni tulipata Shahidi ambaye tulipanga Kuja naye Leo. Lakini Asubuhi amepata Tatizo la Ki Afya lililosababisha Kushindwa Kuja Mahakamani. Kwa sababu hiyo tunaomba Hairisho Mpaka Kesho

Wakili wa Serikali: Na Kwamba Kwa sababu hii ipo Nje ya Uwezo Wetu pia tunaweza Kupata Shahidi Mwingine

Jaji: Wakili wa Utetezi, Kibatala: Kwa Kufuata amri ya mahakama Iliyokuwa imetolewa Jana, sisi kwa upande wetu tulikuwa tumejiandaa vizuri, Lakini kama wenzetu wanasema hivyo ndiyo Ilivyo tunaomba wenzetu kesho wajitahidi, tuweze kuendelea ili tuweze kumalizia kwa wakati

Jaji: umezungumzia Kwa niaba ya wote au!? Kibatala: kwa niaba ya wote Mheshimiwa Jaji anainama, anaandika. Mahakama ipo kimya wakati Jaji akieendelea kuandika Sura za watu wengi zimeweka makunyanzi Washtakiwa wanacheka na kunong'onezana Jambo fulani, hatuwasikii.

Jaji: kuzingatia maombi yalitolewa na wakili mwandamizi Robert Kidando shahidi kushindwa kufika mahakamani Na kuzingatia ukweli kwamba maombi hayo hayajapingwa na utetezi Nahairisha Shauri mpaka kesho saa 3 ambapo upande wa mashtaka mnaaelekezwa kuleta mashahidi

Jaji anatoka!
Shahidi roho imemsuta
 
ila wafuasi wa mbowe mnaroga sana![emoji1787].
nashauri idadi ya wanao ingia kwenye ukumbi wa mahakama ipunguzwe au wasichiwe vilivyo.
washirikina kibao wanaingia, nimewashuhudia kwa macho yangu.
Gambosh siku hizi wameokoka wote? Lumumba kuna budget ya kamati ya ufundi.
Hakuna siri ya wawili.....shahidi wa leo aligoma,amejitoa...wamemtishia.... Kaka wasomi wanafahamu nini kimetokea
 
Gambosh siku hizi wameokoka wote? Lumumba kuna budget ya kamati ya ufundi.
Hakuna siri ya wawili.....shahidi wa leo aligoma,amejitoa...wamemtishia.... Kaka wasomi wanafahamu nini kimetokea
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Inabidi Tigo wamfukuze kazi yule pimbi..kwenda mahakamani kuongea maneno mazito kama yale. Kwamba kampuni haiwajibiki kutunza siri za wateja... wanataka nani sasa atunze?

Mpaka leo TIGO hawajasema kitu Wala kukana tamko alilotoa mwanasheria wao na hii Ina maana wanakubaliana nae kuwa Tigo hawana jukumu la kutunza siri za wateja wao
 
ila wafuasi wa mbowe mnaroga sana![emoji1787].
nashauri idadi ya wanao ingia kwenye ukumbi wa mahakama ipunguzwe au wasichiwe vilivyo.
washirikina kibao wanaingia, nimewashuhudia kwa macho yangu.
Wakala wa shetani ,kumbe na uchawi umo.Kanisa limeingiliwa Kwa kweli.
 
Shahidi either kaingia mitini, au wanasheria wa jamuhuri wamegundua ni muendelezo wa aibu. Kwahiyo wanataka muda zaidi wa rehearsal.

Siyo muuza mbege tu pekee ndiye aliyeleta aibu kwa jamuhuri, pia yule mtaalam wa forensic aliyekuwa akijinasibisha na usomi pamoja na mwanasheria uchwara wa Tigo ambaye naye ushahidi wake ulikuwa wa ki tigotigo tuu!😄

Kesi ya kubambika kama story haijakaa fresh, huwa haibambi hata kidogo. Watunzi wa hovyo kabisa. Kuna kesi moja ambayo mtuhumiwa eti alitokea kuwa mkenya, kisha akaibukia kanisani kwa Gwajima. Polisi walisema! Nimesahau kesi yenyewe. Lakini ilikuwa high profile na polisi wakawa wanakuja na story za kutungatunga tu kama ilivyokuwa issue ya Mo Dewji kutekwa.
Huyo Mkenya aliyeibukia kwa Gwajima ndio tuliambiwa alimteka na kumtesa Dr Ulimboka.

Kali zaidi ya Mo Dewji suspect eti ni Tax driver na gali iliyotumika ni Toyota surf ilitelekezwa maeneo ya ocean road, prime area kwenye maximum security.😄😄
 
Nashukuru kwa kunikumbusha mkuu😂

Sijawahi kuona polisi mwenye akili.
 
ila wafuasi wa mbowe mnaroga sana![emoji1787].
nashauri idadi ya wanao ingia kwenye ukumbi wa mahakama ipunguzwe au wasichiwe vilivyo.
washirikina kibao wanaingia, nimewashuhudia kwa macho yangu.
Mchawi wao namba moja ni yule Askofu Mwamakula, ndio ana tunguli zote, mzuieni asiingie mahakamani.
 
Back
Top Bottom