Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi - 27/09/2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi - 27/09/2021

Mashaidi wa utetezi (Chadema) wanajigongagonga kweli. Yaani anasema Jaji aandike aliteswa na hakuteswa, vyote kwa pamoja!!! Wahesabu maaumivu kwa ushahidi huu
wengi pamoja na wewe hamkuelewa nini maana ya mateso na kipigo. Je muda wa kusaini maelezo aliteswa?..jibu ni hapana. utashikaje pen wakati una pingu? utakaaje kwenye kitu ili u- sign wakati una pingu miguuni, au wakati upo utupu nk

Lazima tujue mateso ni nini lakini lazima pia tujue kuwa kipigo ni sehemu ya mateso.

so wakati wa ku-sign shahidi hakuwa na mateso yoyote na ndiyo maana aka-sign.
 
1. Kwanini iwe Jeshi? Kwani aliyekuwa mwajiri wa Adamoo (JWTZ) ambayo ni taasisi ya umma yenye taratibu za kisheria za ku - HIRE, FIRE and SUSPEND ingewezaje kumsimamisha au kumfukuza kazi mwajiriwa/askari wake bila kumtaarifu kwa maandishi na sababu za kufukuzwa kwake..?

2. That means, lazima lazima Adamoo ana barua ya kuachichwa kwake kazi ya uaskari jeshini. Kwa hiyo haihitajiki hata kuomba taarifa kwa CDF kwa sbb evidence kwamba Adamoo aliachichwa kazi kwa sababu yoyote anayo yeye anayejitetea...

Kama JWTZ lilimwachisha kazi Adamoo kwa sababu yoyote ile bila ya kumwandikia suspension/dismissal letter inayoeleza sababu ya kuachichishwa kwake kazi ya uaskari, basi hilo ni tatizo jingine kabisa na tena ni kubwa linaloweza kuathiri kesi yote hii na kuipa sura nyingine kabisa...!!!
Sorry, unadhani inaweza kuleta sura gani
 
Nilichojifunza ni kwamba kuwa Shahidi kwa kitu ulichokiona na kukishuhudia kwa macho ama kutendewa ni kazi rahisi mno mno, usiombe kufundishwa ushahidi ni lazima utachemka tu mbele ya safari..
Utetezi sidhani kama Kuna aliyefundishwa la kusema. Wànasema yaliyotokea kweli
 
Kwa wale ambao hamjui shahidi alivyosema "killing zone" ndiyo hii - mateso yake ni ya namna hiii - ukivumilia dakika 30 we ni kidume kweli kweli.. Nafikiri kati yao Adamoo atakuwa kapitia mateso makali mno.

FAEtVWGUYAoEc2Z.jpg
 
Jamaa wanamtengenezea inshu nyingine alikuwa anatumia madawa ya kulevya hko, hawakawii kumpeleka kwa mkemia mkuu wa serikali wapate positive findings, maana wanadai eti hakua na battle confusion ila nadawa ya kulevya!
Naona kama wameidrive vizuri- maana kama alikuwa na battle confusion asingweza kutafuta ajira maana hawezi kuajirika.
pili mtu mwenye battle confusion siyo rahisi kumdhibiti- rejea ffilamu ya Rambo- wale polisi walipomletea za kuleta - alikula nao sahani moja.
 
Hapa jamaa wanapiga nyayo maumivu unayasikia kichwani kupitia nerve za mgongo - balaa!!
FAEYRR5XEAEbdcN.jpg
 
Siri ya Tazara inafichuka na hii kesi.

Wameweka watu mahabusu miezi nane bila kuwafikisha mahakamani.

Tazara ni Guantanamo ya Tz
Hicho kituo Ogopa sana,ukipita pale kwanza ni mgeni huwezi kujua kama kuna kituo cha Polisi na hata kama unajua utashangaa kuona kituo hakina harakati nyingi kama vituo vingine,kipo kimya sana. Halafu hiki kituo kina history na vinasaba na watu wasiojulikana,watuhumiwa na wahalifu wengi wanaotolewa Mikioani kuletwa Dar hukifia pale.
 
Kutoka mahakamani

Shahidi(Mshitakiwa) :

Sijakishika Vizuri lakini kama Shaba Nzito

Wakili Mallya: nini Kilifuata?

Shahidi(Mshitakiwa) :
Ilikuwa Jioni Kigiza Kimeingia, nikamwambia tupumzike Ndugu yangu

akajibu haya

Mpaka kesho yake wakaja kutuchukua kuelekea Dar

Wakili Mallya;
Mimi na mheshimiwa Jaji tunaweza tusielewe

ukisema Huyu mafuta siyo Mengi maana yake nini..?

Shahidi(Mshitakiwa) ;?Ninkwamba kwa wao walivyonipoga walifikiri sitoweza Kutembea,Lakini Mimi walipomaliza Kunipiga niliweza Kutembea na palepale Walipomaliza Kunipiga nikiwa Nekaa chini niliwaomba waniruhusu nirukeruke kutuliza Maumivu

Wakati wanajitoa Nje Afande Jumanne akaropoka " Mwenzako amepigwa Sana,Bahati yako Ulipata Mtetezi"

Wakati mimi nikiwa tayari ndani ya gari tayari nilimuona Adamoo anatolewa kwakukokotwa,Wakaniwahi Mahita akapa Goodluck Shuka wakanifunga Kichwani

nikawa nimetulia, Nikaona Mlango wa gari umefunguliwa,na Mtu akaingia na Kuanza Safari

Wakili Mallya:
Baada ya akumuona Adamoo wakakuzuia na kukufunika usoni, Je ulimuona akiwa na Hali gani?

Shahidi(Mshitakiwa) : Nilimuona akiwa anakokotwa hawezi hata kutembea

Wakili Mallya:
Baada ya kuinamishwa kichwa na akufungwa Shuka usoni kitu gani Kilifuata?

Shahidi(Mshitakiwa) :
Nilikuwa kimya wakati huo gari ikawa wakati wote inatembea

Wakili Mallya: Wakati huo nini Kilifuata?
 
Kesi ndogo inayofuata Ni kingai na mahita kuiba pesa za watuhumiwa.
Adamoo 260000
Mohamedi 300000
Shaidi wa tatu 40000
Jumla 600000.Kibatala ninekuelewa dawa yao ndiyo hiyo kuwa shahidi anageuka kuwa mtuhumiwa.

Sasa hapo tutaona Kama tuna mahakama za kutoa haki au kuna vijiwe ili watu waanze kutafuta haki kwa staili nyingine.
 
Naona kama wameidrive vizuri- maana kama alikuwa na battle confusion asingweza kutafuta ajira maana hawezi kuajirika.
pili mtu mwenye battle confusion siyo rahisi kumdhibiti- rejea ffilamu ya Rambo- wale polisi walipomletea za kuleta - alikula nao sahani moja.
Does it persist lifetime? Alitibiwa siyo? Nini maana ya kutibowa? Meaning healing or some relief.....
 
Mshtakiwa No. 2 kaipa mwanya Serikali, kawega ugumu wa kesi kwa Mbowe, amedhiilisha kuwa wamekaririshwa tena akihojiwa na wakili wake! Wampange vizuri ama sivyo upande wa mashtaka watakapo mchalange atayumba sana.
 
Back
Top Bottom