Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa. Shauri kuendelea kesho Nov, 2, 2021

Yaani majibu ya kutunga yana furahisha sana. Unaona kabisa majibu ya ajabu ajabu.
 
Usimjibu mpumbavu kipumbavu, usije ukafanana naye. Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi. Kumtuma mpumbavu ujumbe, ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida. Methali mdomoni mwa mpumbavu, ni kama miguu ya kiwete inayoninginia. Kumpa mpumbavu heshima, ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali, ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi, ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima? Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.
 
Walikuwa wanakunywa hapo hapo wanaongea na simu wakiwa wanatembea duh! Hivi mawakili wa sirikali hawaoni haya kupeleka mashaid wa dizaini hii

Kutoka alipo hadi eneo la tukio ni kama hatua 2 hivi, lakini Anita anaendelea na usafi..!!
 
Wewe umejuaje wa uongo, ulikuwa eneo la tukio..acha ushabiki huu ushahidi upo wazi kuliko hata ule Sabaya wa kuunga unga na gundi
 
Makamani hapa wakili wa serikali Esther Martin anaupiga mwingi sana


Shahidi: Wakati wanaongea na Simu Walitokea watu wawili wakaongea kwa sauti kali "Mpo chini ya Ulinzi Mnahusika na Mambo ya Kigaidi, chuchumaa Chini Mikono Juu"

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine ulisikia

Shahidi: Chuchumaa Chini Mnahusika na Mambo ya Kigaidi Wakili wa Serikali: Ni watu gani sasa hao

Shahidi: Ni Askari

Wakili wa Serikali: Ulikuwa unafanya nini wakati huo

Shahidi: Nafanya Usafi

Wakili wa Serikali: Pana umbali gani kutoka Walipo na Mpaka Ulipokuwa unafanya Usafi

Shahidi: Hatua 05

Wakili wa Serikali: Ulisikia nini Kingine

Shahidi: Sikusikia Kingine zaidi ya Chuchumaa Chini Nyoosha Mikono Juu

Wakili wa Serikali: Walikuwa Askari wangapi

Shahidi: Wawili

Wakili wa Serikali: Hali ya Pale ilikuwaje

Shahidi: Ilikuwa ni Utulivu

Wakili wa Serikali: Nini Kilifuata

Shahidi: Walitokea Askari Wengine watatu wakawa wamefika eneo la Tukio

Wakili wa Serikali: Ongeza Sauti

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kuwa Askari watano alitokea Mmoja akaniambia anaomba nisogee anahitaji Kuwafanyia Upekuzi
 
Wewe umejuaje wa uongo ..ulikuwa eneo la tukio..acha ushabiki huu ushahidi upo wazi kuliko hata ule Sabaya wa kuunga unga na gundi
Tutajie was sabaya umeungwaungwa vipi wakati hata huyo mtoto was mwisho was humour unamokaaa anajua kwamba sabaya alikuwa jambazi.

Muuza mbege ni askari na ni malaya sana.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake itaendelea leo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, ambapo upande wa mashitaka utaleta shahidi mwingine...
Mbowe et al anapelekewa moto
 
Hii kesi iwe fundisho kwa vyama vingine ambavyo badala ya kufanya kazi za siasa, vinajigeuza kuwa Genge la kihalifu.
inapaswa kujitathimini kila wakati.
Ni MUNGU yupi unaye mwabudu katika kanisa la WA-ADVENTIST WASABATO?Jumamosi ulikuwa kanisani kufanya nini?Kwanini unashuhudia jirani yako uongo?

Vyeo vya CCM, fedha za CCM na fahari zote za CCM kwanini zikutenge na MUNGU wa kweli.Unatofauti gani na wakala wa shetani ndani ya kanisa letu la SDA?
 
Ngoja akutane na Kibatala huyu atapoteana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…