Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa. Shauri kuendelea kesho Nov, 2, 2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa. Shauri kuendelea kesho Nov, 2, 2021

leo wafuasi wa Mbowe hamjaroga?

naona shahidi anatiririka kweli, sindano zinaiingia sawasawa!

siku ile mliloga sana hadi shahidi akashindwa kutofautisha kati ya "utalii" na "ugaidi".

Wafuasi wa mboe acheni kuloga.
 
leo wafuasi wa Mbowe hamjaroga?
naona shahidi anatiririka kweli, sindano zinaiingia sawasawa!!
siku ile mliloga sana hadi shahidi akashindwa kutofautisha kati ya "utalii" na "ugaidi".
Wafuasi wa mboe acheni kuloga.
Bila shaka wewe ni shabiki wa Simba Mkuu
 
Ujinga mtupu! Yaani Askari from nowhere ataje namba za silaha?

Huyu nae poyoyo! Na huyu shahidi yaani RAIA wa kawaida akazikariri faster hadi Leo?
Yote ni “staged”, tatizo shahidi ni kilaza na waliobambika kesi nao ni vilaza wahed.

Kesi ya kubambika ina “loopholes” za kutosha. Maneno anayoyaongea leo mahakamani, ni yakukaririshwa na wanasheria. Na hiyo ni baada ya wanasheria kuona maelezo waliyoyatoa na kuandika huko kwenye eneo la tukio pamoja na kituoni polisi hayana mashiko, na wala PGO haikufuatwa!

Aibu kubwa kwa Taifa.
 
Shahidi: Nikiwa Nimekaa ndiyo zinafanana

Mtobesya: Ukiwa Umekaa umesaini Mara Ngapi na Nyaraka zipi

Shahidi: Zile ambazo nilikuwa kituoni kutoa Maelezo.

Mtobesya: Zote ambazo ulisaini Ukiwa Umekaa Zina fanana..?

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Zote ulizoSaini Ukiwa Umesimama Zinafanana au hazifanani

Shahidi: Zinafanana


😂😂😂🤦🏾‍♂️🤦🏾‍♂️
 
Maelezo ya shahidi kwenye statement na mahakamani anavyoelezea anajipinga mwenyewe

Mahakamani anasema alikuta kete 25 wakati kwenye statement kasema kete 21
hawa mashahidi huwa hawapewi kuyasoma maelezo yako kabla ya kupanda kizimbani? naomba nijuzwe.
 
Back
Top Bottom